Sokomoko
JF-Expert Member
- Mar 29, 2008
- 1,915
- 129
Mahakama yamwachia huru Mtikila katika kesi ya uchochezi
Na Tausi Ally
MAHAKAMA ya hakimu mkazi wa Kisutu jijini Dar es Salaam, imemuachia huru mwenyekiti wa Chama cha Democratic (DP), Mchungaji Christopher Mtikila aliyekuwa anakabiliwa na kesi ya kutoa maneno ya uchochezi dhidi ya viongozi wa serikali ya awamu ya tatu.
Mchungaji Mtikila aliachiwa huru jana baada ya mawakili wa serikali, Irene Resulia na Prosper Mwangasila kushindwa kuithibitishia mahakama kama mchungaji huyo ana kesi ya msingi ya kujibu.
Hakimu Msongo alisema amemuachia huru Mtikila kutokana na upande wa mashitaka kushindwa kuithibitishia mahakama kuwa ana kesi ya msingi ya kujibu dhidi ya shitaka namba 425 ya mwaka 2002.
Mara ya mwisho katika mahakama hiyo, mwendesha mashitaka wa Polisi, Nassoro Sisiwaya aliiomba mahakama kufunga ushahidi wa kesi hiyo baada ya mashahidi watatu wa upande wa mashitaka kumaliza kutoa ushahidi.
Kutokana na ombi hilo, Hakimu Msongo aliahidi kutoa uamuzi dhidi ya shauri la awali kama Mchungaji Mtikila ana kesi ya kujibu au la, uamuzi ambao umetolewa leo kwa Mchungaji huyo kuachiwa huru.
Katika shtaka dhidi yake lililosomwa mahakamani, Mtikila anadaiwa kutoa maneno hayo Julai 27, 2002 kwenye viwanja vya Jangwani. Ilidaiwa kuwa maneno hayo ni ya uchochezi na ambayo yangeweza kusababisha kuvunjika kwa amani.
Pia alidai kuwa rais wa awamu ya tatu, Benjamin W. Mkapa hakuwa raia wa Tanzania bali ni wa Msumbiji na kwamba hana uchungu na nchi hii kwa kuruhusu makontena ya mchanga wa dhahabu kupelekwa nje ya nchi.
Ilidaiwa kuwa pia alitoa maneno mengine ya uchochezi kuwa kuwa waziri mkuu wa wakati huo, Fredric Sumaye ni gabachori na mwizi mkubwa.
Source Mwananchi.