Mahakama yamwamuru Reginald Mengi afike kujieleza kwanini asifungwe kwa kupuuza hukumu ya Mahakama

Mahakama yamwamuru Reginald Mengi afike kujieleza kwanini asifungwe kwa kupuuza hukumu ya Mahakama

Status
Not open for further replies.
Katika hati ya kiapo ya wafanyabiashara hao, inadaiwa walifungua kesi dhidi ya Mengi na Kampuni ya K.M. Prospecting Limited, wakidai malipo yaliyokuwa yamebakia ya dola 428,750, 100,000 na 70,000, kwa kila mmoja.
Hiki kiasi ni sahihi kweli?! Mbona hata serikali ya TZ haina?
 
View attachment 384143

MAHAKAMA Kuu Kitengo cha Biashara imeamuru Mwenyekiti Mtendaji wa Makampuni ya IPP, Reginald Mengi afike mahakamani kujieleza kwa nini asifungwe gerezani kwa kushindwa kutekeleza hukumu inayohusu malipo ya Sh bilioni 1.2.

Mengi anatakiwa kufika mahakamani hapo Agosti 24, mwaka huu kujieleza kutokana na kushindwa kutekeleza hukumu iliyomtaka kuwalipa wafanyabiashara watatu, Muganyizi Lutagwaba, Eric Mshauri na Charles Mgweo, Sh bilioni 1.2.

Alitakiwa kuwalipa fedha hizo kutokana na mgogoro wa malipo ya uuzwaji wa hisa katika Kampuni ya Douglas Lake Minerals Ltd ambayo kwa sasa inaitwa Handeni Gold Inc.

Kwa mujibu wa hati ya wito wa kufika mahakamani, Mengi anatakiwa kufika mahakamani hapo Agosti 24, mwaka huu ili ajieleze kwa nini asifungwe gerezani kama mfungwa wa madai kama sehemu ya kukazia hukumu hiyo.

Mahakama imetoa hati hiyo kutokana na wafanyabiashara hao kuwasilisha maombi katika hatua ya kukazia hukumu iliyotolewa Januari 28, mwaka huu na Jaji Agathon Nchimbi wa mahakama hiyo.

Katika hati ya kiapo ya wafanyabiashara hao, inadaiwa walifungua kesi dhidi ya Mengi na Kampuni ya K.M. Prospecting Limited, wakidai malipo yaliyokuwa yamebakia ya dola 428,750, 100,000 na 70,000, kwa kila mmoja.
Kuna tatizo kwenye hii hukumu au mimi sijaelewa?
-utamfungaje mtu kwenye Limited Company?
- Mengi alikuwa kama shareholder tu au alikuwa na cheo kwenye kampuni ya Douglas Lake Minerals Ltd?
 
Kesi ya madai tena ya kuungunga hafungwi.Je kufungwa ndio jibu?hata akifungwa wadai watapata nini? Sana sana utafilisi mradi unazungumziwa,settle this out of court vinginevyo itachukua muda mrefu bila malipo.
 
Hivi kwenye limited kampuni utamfungaje mtu kama ni shareholder?
 
Yeye hataenda wala nini atamtuma wakili wake na kujitetea hajapata hukumu ya kesi hiyo.....na ukute kuna rufaa juu yake! Utashangaa!!
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom