Mahakama yashindwa kusoma kesi ya Masogange; adaiwa kuwa mgonjwa

Mahakama yashindwa kusoma kesi ya Masogange; adaiwa kuwa mgonjwa

MumbaZ

Senior Member
Joined
Jan 28, 2018
Posts
133
Reaction score
124
MAHAKAMA YASHINDWA KUSOMA HUKUMU YA MASOGANGE
Hata hivyo, mdhamini wa Masogange ambaye hakutaja jina lake alisimama na kuiambia mahakama kuwa Masogange hakufika mahakamani kwa sababu anaumwa.

Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imeshindwa kumsomea hukumu msanii Agnes Gerald maarufu kama Deal ama Masogange anayekabiliwa na kesi ya kutumia dawa za kulevya kwa sababu anaumwa, amewekewa dripu na hawezi kutembea.

Hukumu hiyo ilitarajiwa kutolewa na Hakimu Mkazi Mkuu, Wilbard Mashauri mara baada ya upande wa mashtaka ukiwakilishwa na Wakili wa Serikali, Costantine Kakula kuwaita mashahidi watatu kutoa ushahidi dhidi ya Masogange na kuufunga na mshtakiwa mwenyewe kujitetea.

Ilipofika saa 3:46 asubuhi leo Jumatano Machi 21, 2018 kesi hiyo iliitwa kwa Hakimu Mashauri na wakili wa Serikali, Adolf Mkini alieleza kuwa kesi ilipangwa kwa ajili ya hukumu ila mshtakiwa Masogange anayewakilishwa na wakili Ruben Simwanza hakuwapo.

Hata hivyo, mdhamini wa Masogange ambaye hakutaja jina lake alisimama na kuiambia mahakama kuwa Masogange hakufika mahakamani kwa sababu anaumwa na akawasilisha nakala za vyeti vya hospitali mahakamani hapo. Soma: Masogange asimulia kortini namna alivyodakwa na polisi (Masogange asimulia kortini namna alivyodakwa na polisi) Mdhamini huyo amedai kuwa Masogange amewekewa dripu na hawezi hata kutembea mwingine anayemtetea Masogange ni Nehemiah Nkoko.

Masogange wakati akijitetea katika kesi hiyo aliiomba mahakama imuachie huru kwa sababu hana kosa lolote. Masogange ambaye anakabiliwa na kesi ya kutumia dawa za kulevya aina ya Heroin na Oxazepam, katika utetezi wake amedai kuwa yeye hajawahi kutumia dawa za kulevya hata siku moja.

Akijitetea Masogange meidai kuwa mbali ya kuwa msanii pia alikuwa ni mfanyabiashara wa nguo. Masogange katika kesi hiyo anadaiwa kuwa kati ya Februari 7 na 14,2017 katika maeneo yasiyojulikana ndani ya jiji la Dar es Salaamalitumia dawa za kulevya aina ya Heroin (Diacety Imophine). Pia anadaiwa kuwa kati ya Februari 7 na 14, 2017 alitumia dawa zakulevya aina ya Oxazepam.

Mfululizo wa kukamatwa, kesi, hukumu na kuachiwa huru kwa Agnes Masogange kwenye kesi ya Madawa ya kulevya

Masogange ajisalimisha mwenyewe Mahakama a Kisutu

Kupandishwa kizimbani na kusomewa shitaka

Yaliyojili wakati wa kesi ya Masogange

Masogange kupelekwa kwa Mkemia Mkuu

Kesi kusikilizwa

Tetesi za kuachiwa huru

Hukumu

 
Hakuna Kesi hapo kwanza Kesi yake inaendeshwa kiupendeleo Mbona wauzaji wajikamatwa na kupandishwa mahakamani kisutu hawapewi dhamana wanasota ndani tu.......

Ova
 
Hakuna Kesi hapo kwanza Kesi yake inaendeshwa kiupendeleo Mbona wauzaji wajikamatwa na kupandishwa mahakamani kisutu hawapewi dhamana wanasota ndani tu.......

Ova
Kuna tofauti kubwa kati ya muuzaji na mtumiaji wa madawa ya kulevya.Muuzaji anafanya kosa la jinai ,mtumiaji ni muathirika/mgonjwa anayetakiwa kutibiwa na sio kushtakiwa.Ndio maana serikali imejenga vituo kwa ajili ya kuwatibu waathirika wa madawa ya kulevya(Sober House)!
 
Back
Top Bottom