Mahakama yasogeza mbele kesi ya aliyekutwa na sehemu za siri za kike

Mahakama yasogeza mbele kesi ya aliyekutwa na sehemu za siri za kike

BARD AI

JF-Expert Member
Joined
Jul 24, 2018
Posts
3,591
Reaction score
8,826
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imeutaka upande wa mashtaka katika kesi ya kukutwa na viungo vya binadamu inayomkabili Salum Nkonja (23) kuwa shauri hilo litakapokuja tarehe ijayo wahakikishe wanaleta mashahidi pamoja na vielelezo katika mahakama hiyo.

Inadaiwa kuwa mshtakiwa huyo alikutwa na viungo vya binadamu hususan sehemu za siri za kike, matiti, mafuvu ya kichwa cha binadamu na nyara za Serikali.

Hatua hiyo inakuja baada ya wakili wa Serikali, Mosie Kaima kuieleza Mahakama hiyo kuwa shauri lilikuja kwa ajili ya kuendelea na ushahidi na shahidi yupo mahakamani hapo lakini vielezo hawana.

Ndipo Wakili wa Utetezi, Hubert Mligo alidai kuwa Januari 4,2023 shauri hilo lilipangwa kwa ajili ya kusikilizwa lakini upande wa mashtaka hawakuwa na shahidi hivyo waliiomba mahakama hiyo itoe ahirisho la mwisho katika kuzingatia utendaji wa haki hivyo kama hawatakuwa na shahidi itolewe amri inayofaa.

Mligo alidai leo hii shahidi amefika mahakamani hapo lakini upande wa mashtaka wameeleza kuwa hawana vielelezo kutokana na hilo wameomba ahirisho na iwaelekeze upande wa Jamuhuri walete mashahidi wakiwa na vielezo ili shauri liweze kusikilizwa.

"Hii kesi imeshafutwa mara tatu na hii imeanza upya Mei 7, 2022 lakini kila wakija mahakamani shahidi hakuna na leo hii upande wa mashtaka wamemleta shahidi lakini hana vielelezo," alidai Mligo.

Hakimu Mwandamizi, Ramadhani Rugemalira alitoa amri kwa upande wa mashtaka katika tarehe ijayo wahakikishe mashahidi wanakuja mahakamani hapo pamoja na vielelezo viwepo.

Shauri hilo limeahirishwa hadi Januari 26, 2023 kwa ajili ya kuanza ushahidi.

Inadaiwa kuwa Oktoba 30, 2017 eneo la stendi Kuu ya zamani ya Mabasi yaendayo mikoani na nchi jirani (Ubungo) akiwa na viungo mbalimbali vya binadami na pamoja na nyara za Serikali.

Nyara hizo ni sikio na pembe ya nyati; mikia mitano ya Nguruwe; uume tatu za fisi; yai moja la mbuni; ndege mmoja mkavu na kichwa kimoja cha kobra.

MWANANCHI
 
Kutafuta utajiri kunavyo watesa watu,ridhika na upatacho huku ukiongeza juhudi ya kazi halali kama ipo ipo tu.
 
Huyo mtuhumiwa atakuwa ameiva sana kwenye masuala ya ushirikina. Yaani anawapumbaza apendavyo hao waendesha mashtaka.
 
Back
Top Bottom