USSR
JF-Expert Member
- Jul 15, 2015
- 10,904
- 26,184
Mjane wa aliyekuwa mfanyabiashara maarufu Reginald Mengi, Jacqueline Ntuyabaliwe Mengi ameangukia pua baada ya mahakama kutupilia mbali rufaa yake.
Ntuyabaliwe aliitaka mahakama iutambue waraka wa wosia wa marehemu Mengi ambao ulikataliwa na mahakama kuu.
USSR
---
Mahakama ya Rufani imetupilia mbali shauri la maombi ya marejeo lililofunguliwa na mjane wa Reginald Mengi, Jacquiline Ntuyabaliwe na wanawe wawili, ambao wamekuwa wakipambana kutetea wosia unaodaiwa kuandikwa na Mengi ambao Mahakama Kuu iliubatilisha.
Katika shauri hilo, Jacquiline na wanawe anaowasimamia, Jayden Kihoza Mengi na Ryan Saashisha Mengi walikuwa wanaiomba mahakama irejee na hatimaye itengue uamuzi uliotupilia mbali shauri la maombi ya mapitio, walilolifungua awali mahakamani hapo wakipinga hukumu ya Mahakama Kuu, iliyoukataa wosia huo.
Hata hivyo, katika shauri hilo la maombi ya marejeo namba 748/01 la mwaka 2022, mahakama hiyo katika uamuzi imewakatalia maombi ya kuurejea uamuzi huo ikisema sababu zilizotolewa hazina mashiko.
Katika uamuzi huo uliotolewa na jopo la majaji watatu waliosikiliza shauri hilo, Rehema Mkuye (kiongozi wa jopo), Abraham Mwampashi na Zainabu Muruke, mahakama imesema sababu walizozitoa si miongoni mwa zile za kuomba mahakama kufanya marejeo ya hukumu yake, bali zinahusu rufaa.
Uamuzi huo ulioandikwa na Jaji Muruke kwa niaba ya jopo hilo, ulitolewa Agosti 5, 2024 na unapatikana katika tovuti ya Mahakama iitwayo Tanzlii.
PIA SOMA
- Jacqueline Mengi aendelea kudondokea pua rufaa, mahakama yaondoa maombi yake ya kutaka kuurudisha wosia