Mahakama yawafutia kesi moja viongozi wa Uamsho Zanzibar

Mahakama yawafutia kesi moja viongozi wa Uamsho Zanzibar

uamsho.jpg

Baadhi ya viongozi wa uamsho wakipelekwa mahakamani.



Zanzibar. Mahakama ya Wilaya ya Mwanakwerekwe imeifuta kesi moja inayowakabili viongozi wa Jumuiya ya Uamsho na Mihadhara ya Kiislamu Zanzibar (Jumiki), kutokana na kuchukua muda mrefu bila ushahidi wake kukamilika.

Hakimu Ame Msaraka Pinja alisema jana kuwa, anaifuta kesi hiyo kwa kutumia kifungu cha 209 cha makosa ya jinai.

Washtakiwa wa kesi hiyo ambayo ilikuwa ni moja kati ya tatu zinazowakabili ikiwa kwenye Mahakama hiyo na nyingine Mahakama Kuu, walikuwa wanakabiliwa na kesi ya kuhatarisha amani kwa kutoa lugha kali.

Ilipotajwa mara ya mwisho, Machi 19 mwaka huu upande wa mashtaka ulidai kuwa, upelelezi haujakamilika na mawakili wa utetezi walimwomba hakimu kuifuta kwa vile washtakiwa wako ndani muda mrefu.

Wakili wa washtakiwa hao, Salum Toufik na Abdallah Juma walimwomba hakimu kutokana na taratibu za Mahakama hususan makosa ya jinai, kesi inapofikia miezi mitatu na kuendelea bila upelelezi kukamilika inapaswa kufutwa.

Upande wa mashtaka, ukiongozwa na Khamis Jafar waliomba Mahakama kuwapa muda zaidi kutokana na kuchukua kipindi kirefu bila upelelezi kukamilika.

Washtakiwa hao ni Masheikh Farid Hadi, Mselem Ali, Mussa Juma, Azza Khalid Hamdan, Suleiman Juma, Khamis Ali na Hassan Bakari. Washtakiwa hao bado wanakabiliwa na kesi iliyopo chini ya Hakimu wa Wilaya, Khamis Rashid na washtakiwa wanne wapo nje kwa dhamana, huku watatu wakiwa rumande kutokana na kukabiliwa na kesi nyingine Mahakama Kuu. Washtakiwa watatu ambao walikwenda katika kesi hiyo wakitokea rumande ni Masheikh Farid, Juma Suleiman na Mussa Juma.
Inaelekea kuna sentiments za udini upande wa wapelelezi. Ushahidi upo njenje inawezekanaje upande wa wapelelezi hawauoni? Umoja na amani vipo hatarini ni vema haki itendeke
 
Hao watatoka tu na target yetu ipo palepale,jamhuri ya watu wazbr kwanza,hatuuutakiiii....
 
Mahakama ya wilaya ya Mwanakwerekwe Zanzibar chini ya Hakimu Ame Msaraka Pinja imefutilia mbali kesi inayowakabili viongozi wa uamsho, hii ni kutokana na upande wa mashtaka kushindwa kukamilisha ushahidi wa kesi hiyo kwa muda mrefu.
source : Mtanzania
 
Ngoja warudi mtaani sasa tuone. Mungu inusuru tanzania
 
Kesi nyingi zimekuwa ni kupoteza muda na gharama tu!
 
Tanganyika ifungue ubalozi Zanzibar ili Watanganyika wapate pa kukimbilia kwa wao wanachukiwa na kunyanyaswa kuliko wageni wa nchi nyingine mfano Wakenya
 
Kesi za Riz1 alizomshauri babake kufungua hazina hata mashiko kisheria. Riz1 ni msanii
 
fact watu hawataki muungano kwa upande wa zanzibar matatizo yote haya ni ujinga wa ccm kulazimisha mfumo wao wa serekali mbili

sasa ccm hutafuta sababu ili wazime hoja za wapinga muungano ndio huwaita wahuni magaidi kisha hupandikuza Udini

ndi uamsho ni waisilam ni wengindio wanaunga mkono lakini hata wakristu walijitokeza katika mihadhara yao na kuungana na uamsho ili kudai mamlaka kamili ya zanzibar

sasa ccm wakaamuwa kutia watu tindi kali kuteka watu kupiga watu silaha na na kuwauwa mapadri

sasa wanalazimisha lazima kesi ipate mtu wa kumpa yaani wanatafuta mtu wa kumbebesha msalaba na kumshulubu kama yesu
sasa ndio wanalazimisha kesi zao za kisiasa ziwe zimepata watuhumiwa ccm magamba wamemalizika
 
Oh Yeah in UK lakini Umewasikia wakifurukuta furukuta HUKO? Wanafuata SHERIA na KATIBA za UK wapende wasipende; Wanasimama Majukwaani na kutukana serikali ya UK? La HASHA Wanainyenyekea...

Lakini Umewaona SAUD ARABIA wakimiliki ARDHI? HATA KIDOGO na hawataki kwenda HUKO...

Hawataki kufuata sheria lkn sheria ikiwafuata wanataka kuandamana. Hii inawezekana bongo tu kajaribuni kwingine muone
 
Hawataki kufuata sheria lkn sheria ikiwafuata wanataka kuandamana. Hii inawezekana bongo tu kajaribuni kwingine muone

FREEDOM of SPEECH; Kama kuna KIBALI cha KUANDAMANA sidhani ni VIBAYA KURUHUSU Wanachama wa CHAMA FULANI KUANDAMANA au KUKUSANYIKA ili KUTANGAZA HOJA ZAO; Lakini Sio kwenda na KUTUKANA na Kubaguana kwa MRENGO wa DINI; UKABILA au RANGI...

Tatizo kubwa ni UCHUMI kama kweli serikali tawala ingewza kumudu UNEMPLOYMENT ya VIJANA wengi NCHINI haswa MIJI MIKUBWA haswa Dar-es-salaam na kufungua viwanda vyote walivyoviuza ... SIDHANI kama tungekuwa na Matatizo haya ya UDINI DINI Nchini.... Hii yote ni UCHUMI na tunatafuta MNYONGE wa KUMLAUMU na MNYONGE wa KARIBU ambaye kila Mmoja anaweza kuelewa vizuri ni kulaumu UDINI...
 
Back
Top Bottom