Mahakamani: Aliyemchoma mkewe kwa magunia mawili ya mkaa anatajwa kuwa mlemavu wa akili


Tatizo la insanity inapimwa kwa observation ya behaviors tu, hamna empirical test au biological test ya kupima akili kwa kuwa akili sio physical. So plotting inaweza kufanyika na deliberate planned recording inawezekana tu then conclusion ikafanyika then judge atachukua expert opinion na akamaliza. But km kuna mauaji lazima mtu atakaa Isanga muda wa kutosha tu hata kama atakuwa acquitted
 
Mahakama imfutie mashitaka aachiwe huru mara moja kwaajili ya matibabu
Sasa unataka Mahakama imrudishe mtu mwenye tatizo la afya ya mtaani, si atauwa na wengine huko kitaani kwao!? Bora ishi milembe for life! Maana once a kichaa,always a kichaa,ni swala la muda tu!!
 
Akili ya miaka iliyopita,inapimwaje mwaka huu!? Na unazitofautisha vp akili za mwaka jama na mwaka huu!!?
generally ili mtu aweze kuwa na hatia lazima tujiridhishe kama kosa alifanya akiwa na akili timamu au la
Na vile vile hata kuhukumiwa hatuweI kumhukumu mtu ambaye akili yake haipo timamu, anatakiwa apeleke akatibiwe ,kwa sababu mtu aliyekuwa hayupo sawa kichwani hata kujitetea hawezi
 
Kumuhukumu mtu yeyote kwa makosa ambayo hujui chanzo,hali ya mtuhumiwa au kichocheo chake ni ubatili sana wa fikra.Tuombe yasitukute.

Kwahiyo mtu akifanya kosa kama mauaji asihukumiwe hadi mjue chanzo chake kwa lugha nyingine kuua ni sawa so long as chanzo ni halali?
 
Tupe hizo tofauti tuzijuwe wote pls!!
Chukulia kwa mfano wakati wa makaburu wa Afrika kusini kulikuwa na Sheria ya waafrika weusi kutokutembea mitaa ya wazungu. Ukishikwa unakamatwa na kushtakiwa. Hiyo siyo haki lakini sheria inasema usipite.
Hata Tanzania Kuna sheria nyingi zenye kunyima wananchi haki
 
Ndo chimbo jipya la kujinasua kwenye kesi za mauaji.

Hivyo siyo ajabu.

Vyombo vya habari vililipoti hivi,,l

Aliandaa mashimo siku tofauti,

Akaandaa tanuru la kumchomea mke wake, Akaenda akatafuta magunia mawili ya mkaa akatanguliza gunia Moja la mkaa Kisha mwili wa mkewe Kisha gunia jingine, Kisha akamchoma, na baada ya siku chache Kubeba mabaki na kwenda kuyafukia shambani kwake na kupanda mgomba.

Haikutosha na alienda polis kuripoti mkewe kapotea.

HIVI HUO MLOLONGO WOTE HUO BADO TUAMINI ALIKUWA NA UGONJWA WA AKILI?
 
Mipango yoote matayarisho yoote yale, mpaka kuzika vipande kule shamba. Mmh sidhani akili iliruka labda huko gerezani ndiyo ilifyatuka.
Unadhani waliorukwa akili wote hawavai nguo? Hawakwepi magari barabarani? Hawajitafutii kipato?

Anyways, sitetei upande wowote. Najaribu kuwaza kumsauti tu, mkuu.
 
Duh
 
Tuwe waangalifu sana tunaenda kuoana na nani. Ndoa nyingi zimekuwa sehemu ya kufanya mambo ambayo ni ya kikatili kupitiliza
Wakati mwingine hata uangalifu hausaidii kwani watu hubadilika kitabia au huficha tabia. Sikupingi suala la uangalifu ila naweka tu angalizo. Na kuongezea: ukishaona kwenye ndoa vi-ugomvi haviishi ni bora mkaachana mapema. Kwa experince yangu, hivi vi-ugomvi vidogo vidogo vya kila siku vinapalilia jambo baya sana. Hasa ikiwa ni juu ya mwanamke kuwa na kiburi au kuchepuka.
 
Ajabu huu ugonjwa wa akili, unatambulika baada ya tukio la mauaji, kabla hakuna alietambua, na alikua anaendesha biashara yake vizuri tu.
Tule hela ila tuhurumie Dunia, wakati mwingine tuwe tayari kukosa, kwa ajiri ya amani ya kesho, dah inasikitisha sana.
Naskia aliemdhulumu nafsi mtoto, Asimwe nae anapimwa akili.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…