Mahakamani kuna siri gani? Niliwahi kwenda kwa Mganga wa Kienyeji ili Hakimu na mashahidi washindwe kuongea au kuzungumza Mahakamani

Mahakamani kuna siri gani? Niliwahi kwenda kwa Mganga wa Kienyeji ili Hakimu na mashahidi washindwe kuongea au kuzungumza Mahakamani

Niliwahi kuwa na kesi ya jinai miaka 6 imepita. Aisee ile kesi ulikuwa wazi kabisa na ushahidi wa kutosha, kwa vyovyote vile lazima ningefungwa.

Nikiwa nje kwa dhamana, Kuna mtu akaniambia acha uboya dogo twende mahala. Jamani jamani dawa zipo tusibishe. Nilienda kule nikafanyiwa mambo na kupewa dawa za kuoga na kupaka siku ya hukumu.

Siku ya hukumu. Hakimu akasema nimefungwa kifungo cha nje kwa muda wa mwaka mmoja. Kila siku natakiwa kureport mahakamani hadi mwaka uishe.

Nilivokuwa naondoka karani akaja ananikimbilia akaniambia mhe. Kasema uandike namba yako ya simu nimpelekee. Nikampa no nikasepa.

Jioni nikaona simu inaita namba ngeni. Kupokea mtu akajitambulisha ni ... hakimu wa...... (Nimekupigia kukwambia kwamba ile kusema uwe unareport mahakamani kila siku ni geresha tu, we endelea na maisha yako biashara imeisha).

Sikuamini sana ile simu isije ikawa mtego. Kesho asubuhi nikareport pale mahakamani. Karani akaniambia ina maana hakimu alivyokupigia hukumuamini? We ondoka mbona ishu yako ushaisha.

Ni miaka 6 sasa imepita
Duu hii ni kiboko 😂🤣
 
We mkuu unasemaje?Wakati fulani nilienda field mahali nikakutana na mzee moja yule mzee ni Botanist by proffesion tena kasoma mpaka Germany kahudumu Kuanzia Nyerere mpaka kastaafu sio muda tu..Haya mambo mengi alituambia yapo
Nyinyi mnachanganya karama ya Mtu na miti Shamba!! Kuna watu wamejaliwa karama kubwa sana,akikutkia meme kwenye jambo lako linakua fresh,hata Kama ni kesi nzito inakukukabili!!
 
Niliwahi kuwa na kesi ya jinai miaka 6 imepita. Aisee ile kesi ulikuwa wazi kabisa na ushahidi wa kutosha, kwa vyovyote vile lazima ningefungwa.

Nikiwa nje kwa dhamana, Kuna mtu akaniambia acha uboya dogo twende mahala. Jamani jamani dawa zipo tusibishe. Nilienda kule nikafanyiwa mambo na kupewa dawa za kuoga na kupaka siku ya hukumu.

Siku ya hukumu. Hakimu akasema nimefungwa kifungo cha nje kwa muda wa mwaka mmoja. Kila siku natakiwa kureport mahakamani hadi mwaka uishe.

Nilivokuwa naondoka karani akaja ananikimbilia akaniambia mhe. Kasema uandike namba yako ya simu nimpelekee. Nikampa no nikasepa.

Jioni nikaona simu inaita namba ngeni. Kupokea mtu akajitambulisha ni ... hakimu wa...... (Nimekupigia kukwambia kwamba ile kusema uwe unareport mahakamani kila siku ni geresha tu, we endelea na maisha yako biashara imeisha).

Sikuamini sana ile simu isije ikawa mtego. Kesho asubuhi nikareport pale mahakamani. Karani akaniambia ina maana hakimu alivyokupigia hukumuamini? We ondoka mbona ishu yako ushaisha.

Ni miaka 6 sasa imepita

Huyo aliekwambia twende mahala ulimpa kiasi gani?
 
Mkuu,

Unapaswa kujifunza tena mwandiko, na jinsi ya kujenga hoja.
☝🏾Umekusudia kuniambia mie au umwkosea?
Ujenzi wako wa hoja huko kwenye forum zingine ndo reflection ya uwezo wako. Kazi ya makusudi inahitajika.
Sijui hoja gani nimeileta hadi nionekane kwenye mada za dino uwezo wangu mdogo?.

Up to All; Acha utoto ila ukitaka habari kamili au kutaka mdahalo wa dini funguo wayo wako twende kazi mwanangu!.
 
☝🏾Umekusudia kuniambia mie au umwkosea?

Sijui hoja gani nimeileta hadi nionekane kwenye mada za dino uwezo wangu mdogo?.

Up to All; Acha utoto ila ukitaka habari kamili au kutaka mdahalo wa dini funguo wayo wako twende kazi mwanangu!.
Kuambiwa ukweli ndo utoto? Acha ikae hivyo.

Mapungufu hayakimbiwi mkuu, bali yanakabiliwa.

Hata sasa bado mapungufu ni yale yale.

1- Uandishi mbovu.
2-Ujenzi wa hoja ni dhaifu.
3-Hueleweki unalenga kumaanisha nn hasa.

Simple.
 
AtaKuwa alimdanganya ili asisogelee tunda, Huu nakumbuka Mkuu wa shule Miaka hyo, walifika Watu wa damu salama shuleni, Baada kipindi kupita akaja twambia eti wale maduu wakali ktk Ile shule wameathirika, wajuba wakanywea... Wabishii wakaendelea ikaja kugundulika ni uongo... Yule mistress alikuwa Konyo sana
🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣
 
Mie Kuna mshenzi alinikausha sauti kabisa, kesi ya kufukuzwa kazi, ninawakilisha shirika, jamaa aliyefukuzwa akaniomba tuonane mie nilipofika jioni maana kesi ilikuwa Tanga nikaona huyu mtu anataka kunicompromise uonekane nilikuwa nae hotel.

Nikahama hotel nikahamia Nyumbani Hotel jamaa akanisaka sikuonana nae maana alitaka anipe hela na niliona kesi yake ipo straight Hana haki na procedure zilifuatwa sikuwa na namna ya kumsaidia .

Ile naingia mahakamani akaanza kunilaumu nikamwambia mie sio Wakili wake na asinipigie tena sababu Sina mpango wa kumsaidia kesi yake ni nyoofu ajiandae kusepa kwanza hakuwa na hela ya maana mteja wangu amenilipa vizuri sana na malazi na safari ananilipa hela nzuri sana .

Jamaa akasema tutaona mie mtoto wa kidigo mie nikamshangaa tu, nikamwambia ukiniroga mie utakuwa unapoteza muda maana Sina ugomvi nawe, kazi umeharibu mwenyewe, aliyekufukuza kazi ni HR na umeshindwa kumroga HR uniroge mie .

Babu Ile naingia kwa Jaji marehemu Lugaziya J sauti ikakata, nikaahirisha kutafuta dawa pharmacy, nikakimbia Bombo hospital pale nnje Kuna pharmacy nikapiga dawa naona naongea fresh kabisa.

Basi nikarudi nikamwambia Karani nipo tayari akitoka kusikiliza anipangie tuingie, Ile nimeingia tena sauti ikakata tena.

This time Jaji nae akaogopa anaongea mambo mengi kwa yule mshtakiwa akamwambia yeye amekaa mahakamani zaidi ya miaka 30 anaijua vizuri akasema aache uhuni wake.

Kesi iliahirishwa but ananiambia Kama unasafiri usiondoke leo [emoji2] nami nikaona heri nifuate maneno ya wazee.nikaondoka kesho yake. Jamaa siku kesi inaitwa tena anashangaa nipo akajisemea confession aliweka kitu barabarani nisingepona nikamwambia kesi hii nachoweza kukusaidia ni ulipwe kidogo sitabishia [emoji2][emoji2][emoji2][emoji2] Ila hakurudi kazink.

Uchawi upo. Siku nyingine nitawasimulia yaliyonikuta Mahakama Kuu Tabora Kuna wachawi kule dah
Hahaha hebu tuhadithie
 
Unafahamu ndyeki wewe Bujibuji au wewe wa mjini

Hii ndyeki iliwamaliza watu wengi sana sana, Sitaki kuelezea huu ujinga wa watu wa Mbeya miaka hiyo

Wakati huo wa Ndyeki sisi wakinga tulikuwa wakulima hatujui hata biashara
Hivi Ndyeki mkuu ni nini maana kuna mlima kama unatoka Mbalizi kwenda umalila unaitwa Mlima Ndyeki una height ndogo tu ila zamani ulikuwa maarufu kwa kusababisha ajali.
 
Uongo wa kiwango cha Juu, hawakukumbuki wewe kabisa, Ila kuna records, kuna arrest order Na wewe ulichagua option two!

Uongo narudia tena uongo! Kuna watu Wenye fedha nyingi wamefungwa life time and mganga angekuwa an easy option!

Hakuna Mganga anayeweza kufuta Kesi, simply hayupo, Na hawa Ma police Nina uhakika wana fungu la kujiweka Sawa!

Uongo uongo uongo Na uzandiki
Inawezekana niuongo lakin ukisema kunawatu wenye pesa wamefungwa nataka nikwambie hivi so kila mtu anaamin uganga unaweza kuta mwenye pesa ailiamin pesa zake kea vile huyajui hayo mambo nyamaza, uliza watu tuliowahi kuhudhuria kesi mahakamani
 
Ni kweli ni kama wale wanaokosea namba wanapowatumia ujumbe wateja wao waliowatajirisha kupita kiasi. Unaambiwa Mizimu imeamua kukuongezea mabasi ya mikoani 100
[emoji38][emoji38][emoji38][emoji38][emoji38][emoji38]Wanataka ufanye overtake ili mabasi ukayachukue wewe
 
Wanabodi,

Nayaandika haya sio kwa kufurahisha bali ni mambo yaliyonikuta na sitaki kuyakumbuka kabisa lakini kwa yaliyomtokea shahidi namba 13 wa upande wa jamuhuri Kamanda Swilla kwa kuugua ghafla kizimbani na muda mwingi kuomba ruhusa kwenda washroom au maliwato siyo mambo ya kucheka huwa yanatokea.

Mwaka 2005 Katika purukushani za uchaguzi na kikiri kakala za hapa na pale nilishtakiwa mahakamani kwa kosa ya matumizi mabaya ya pesa yaani rushwa na kuharibu kumbukumbu za ushahidi.

Kwa kuwa Mimi Gussie ni Mkinga automatic Rafiki zangu wengi ni wakinga hivyo kwa kuwa kuna mambo mengi tunasimuliana nikaona isiwe shida kuomba msaada wa ushauri kwa wakinga wenzangu kuhusu kesi inayonikabili Mahakamani.

Wakinga wenzangu Walinipa machaguo mawili

1. Kuifuta kesi kwa njia ya giza yaani mafaili na kumbukumbu zote kwenye Kompyuta na Polisi zipotee kabisa na hata jina langu lisionekane kabisa

2. Watu walionishtaki wakiniona wanikimbie sehemu yeyote ili au washindwe kuzungumza kitu mbele yangu na mahakamani

Mimi nilichagua chaguo namba mbili kwani hawa watu walionishtaki Nilitaka hata Ikifika uchaguzi mwingine waniogope na kunikimbia kila wakiona sura yangu au Uwepo wangu au washindwe kuongea mbele yangu

Nilisafiri toka Dar es Salaam mpaka Mbeya kuelekea Malawi huko kwa Mganga wa Kienyeji, Mganga alinipatia chupa ndogo ukubwa wa chupa ya glycerine yenye mafuta ndani yake na yenye vipande vidogo dogo vya miti ndani yake pamoja na unyoya sijui unyoya wa ndege gani sikumuuliza Mganga, huu unyoya ulikuwa ndani ya hicho chupa unaelea elea tu.

Mganga huyu wa Malawi pia alinikabidhi leso ndogo ambayo kona moja ameifunga ndani ya sehemu aliyofunga sikujua aliweka dawa gani, na Mimi sikuuliza

Kazi ya mafuta ilikuwa pale ninapoenda polisi najipaka kidogo tu usoni au kwenye paji la uso na kuongea maneno ninayotaka mimi mwenyewe, Siku niliporudi tu nikaelekea polisi kwa confidence kabisa kwani walikuwa wananitafuta sijaonekana Mahakamani na wala sijaripoti kwao Polisi, Mimi kabla ya kufika Nilitamka kuwa polisi wa Uchunguzi wanisahau kabisa.

Kweli nilipofika tu polisi, kila polisi pale kituoni alikuwa ananiuliza umekuja kufanya nini hapa, Moyoni nikawa nawaza ni hawa hawa au Wengine. Mwisho wa siku niliamua kuaaga mwenyewe na kurudi zangu nyumbani kwani hakuna polisi aliyenikumbuka au kushughulika na Mimi.

Niliamua kurudi tena pale polisi siku ya pili kwa kutumia ile leso niliyopewa ambayo niliambiwa kazi ya ile leso ni kufukuza nuksi na lolote baya juu yangu, Nilitakiwa kuweka ile leso mfukoni mahala popote kama nikihisi kutakuwa na tatizo au naenda kuonana na mpinzani au adui yangu au mtu yeyote aliye kinyume na malengo yangu, Kumbuka hii ni leso ya kawaida isipokuwa kwenye kona moja tu ndio imefungwa dawa kwa ndani ambayo sijui, Kwa kutumia hii leso pia natakiwa "kunuia" kwa lugha ya kiganga au natakiwa kusema lile ninalotaka lifanyike kwa wakati wowote ule kwa kuigusa leso mfukoni mwangu.

Nikiwa karibu na kituo cha polisi niliigusa leso yangu na kutamka wale wote polisi wanoko walionikamata na kunichunguza naomba wahamishwe kazi pale kituoni kwani wao ndio walikuwa vimbelembele kunisumbua, Nikaingia kituoni counter na kuwaulizia kama wapo nikawakuta, Nikaanza kuwaulizia kuhusu kesi yangu nikaona kila mmoja anamtupia Mwenzake mpira kuwa tuyamalize yaishe huku wakitaka mimi niondoke pale kituoni nirudi nyumbani, Wakanisihi wale polisi basi niwatafuta jioni tuyaongee kwani Mimi wakati huo nilikuwa nafahamika baadhi ya Pub nikila bata, Nikawaambia niwatafuta kesho.

Mambo yalibadilika badala ya polisi kuendelea kunitafuta Mimi, Ikawa mimi ndio nawafuatilia wao ili kujua mwisho wa kesi, Siku iliyofuata wale polisi walinipigia simu wamehamishwa kabisa Mkoa na kutupwa mikoa tofauti.

Baada ya hawa polisi kuhamishwa na hali kupoa kidogo, Nikasafiri tena kuelekea huko Malawi kwenda kutoa report na hatua iliyofikiwa, Kumbuka hizi connections zote za huko ni Mwanamke ndie aliyeniunganishia mpaka Malawi huko hivyo akawa sio rafiki tu ila zaidi ya Rafiki maana hakuna siri ambayo nilikuwa namficha hivyo alinijua ndani nje huyo Mwanamke, Na yeye alifika huko Malawi na kukufahamu huko huyo Dada baada ya watu kumroga akawa ana bleed kila siku karibu miezi mitano bila nafuu mpaka anaongezewa damu mwilini hivyo alidhoofu sana ni kutokana na yeye kuwa na mahusiano na Mume wa Mtu, Aliponea huko Malawi.

Baada ya kukamilisha shukrani huko Malawi, Nikauliza nini mwisho wa yale mafuta na ile lesso, Niliambiwa yale mafuta yakipungua niwe naongeza mafuta ya kawaida tu ya kupikia nayatikisa na kutumia kupaka pale nitakapohitaji kuyatumia

Ishu ya polisi ikawa imeisha sasa ikabaki ishu ya Mahakamani kujua mambo yamekaa vipi huko kwani tayari wambea wameshahamishwa vituo vya kazi hawapo tena

Ishu ya Mahakama Nikaamua kuelekea huko kwetu Ukingani, Nikaelezea hatua niliyofikia na nini kimebaki, Huko kwetu ndio nilikutana na funga kazi ya mwaka, Nilipewa dawa kamzizi kana urefu kama njiti ya kiberiti lakini kanene kidogo, Hiyo dawa kimatumizi haitofautiani sana na zile za Malawi kwani nayo lazima unuie yaani utamke maneno utakavyo nini kifanyike. Wazo langu hapa likanijia kichwani niwafanye watu wa mahakama kuanzia hakimu na Wengine wawe Mabubu yaani washindwe kuongea

Kujaribu uwezo wa huo mzizi kwanza kabla ya kufika kwa pilato yaani Mahakamani Nilitamka nipande gari bure toka Makete huko mpaka Dar bila kulipa nauli njiani, Wakati huo kulikuwa hakuna gari ya moja kwa moja toka Makete mpaka Dar es Salaam, Nilipanda gari toka Makete mpaka Njombe bure kabisa,

Nilifika kwa konda Nikamwambia sina nauli naomba msaada akajifanya kama anataka kuchomoa hivi mara paap akalainika kama bigijii na kwenda mwenyewe kunichukulia ticket kwa Wadada wanaokatisha sijui aliwaambia kitu gani, Nilifika Njombe usiku Nikaamua kutafuna tena kale kamzizi ili nilale guest pale bure kabisa pale Njombe nikisubiri ifike asubuhi nielekee Dar, Baada ya kufika Guest nikamkuta Dada kaunta Nikamwambia Nahitaji chumba lakini sina pesa ya kulipa, Dada akajibu hakuna chumba vimejaa, Nikamwambia sasa tunafanyaje mara paap akalainika kama bigijii akapiga simu guest inayofuata akaongea nao nikalala guest hiyo nyingine bure kabisa bila kulipa kitu

Nitaendelea tena baadae kuelezea

Wale wapambanaji hawawezi kushangaa ninachokisema hapa, Hakuna maisha ya mteremko hapa duniani you have to fight
Hilo la kijiti ni la kweli kabisa kuna mti porini ukiujua basi hakuna mahakama ya kukufunga hata The Hague,,kuna jamaa mwaka jana alipatikana na hatia ya kumtia mimba mwanafunzi wa form one,kesi ikapelekwa haraka haraka akapigwa mvua 30,,ndugu zake wakaungana kukata Rufaa wakafanikiwa kupata mtaalamu akawapa hicho kijiti bwana kesi ikapelekwa mahaka ya juu,,maana mwanzo alihukukiwa na mahaka ya wilaya,,kufika kule huwezi amini wale mashahidi wa mwanzo wote hadi hakimu wa kwanza walishindw toa ushahidi ulonyooka kama awali,,daktari mwenyewe alothibitisha binti ni mjamzito alipotea,,mtoto kufika mahamani akageuza maneno mwisho wa siku ikaoneka mtuhumiwa hana makosa yeyote ilikuwa ni mpango wa kumpotezaa tu,,,wakaamriwa wamlipe fidia,,jamaa yupo zake mtaani sasa hivi analea mwanae
 
Huyo mtaalamu yuko wapi?
 
wamehonga mahakama na Wazazi wa.mtoto then wanawadanganya.kuna kijiti. Wajinga ndio waliwao
 
Uongo wa kiwango cha Juu, hawakukumbuki wewe kabisa, Ila kuna records, kuna arrest order Na wewe ulichagua option two!

Uongo narudia tena uongo! Kuna watu Wenye fedha nyingi wamefungwa life time and mganga angekuwa an easy option!

Hakuna Mganga anayeweza kufuta Kesi, simply hayupo, Na hawa Ma police Nina uhakika wana fungu la kujiweka Sawa!

Uongo uongo uongo Na uzandiki
Usiongee kumaliza mkuu
 
Back
Top Bottom