Mahamoud Ali wa Djibouti ashinda nafasi ya Uenyekiti wa Kamisheni ya Umoja wa Afrika (AUC) dhidi ya Raila Odinga kutoka Kenya

Raila Odinga alikuwa anaungwa mkono na Samia,Jakaya na wana ccm wengine kama Jesca Magufuli. Marais wote wa Africa mashariki pamoja na Jakaya walimpigia kampeni Raila Odinga lakini ameangukia pua.
 
Mimi binafsi sioni faida yoyote ile ya kuwepo kwa hiyo Taasisi inayoutwa African Union (AU). Je, ina faida gani hasa kwa Wananchi wengi zaidi wa kawaida waliopo katika bara hili la Afrika? A toothless institution, hopeless kabisa!

AU kwa sasa imekuwa Kama Kusanyiko tu la wazee Madikteta wanaolihujumu bara hili kwa kujineemesha wao wenyewe binafsi, familia zao pamoja na Vibaraka wao wa karibu.
 
Jamaaa anarudi kumsumbua Ruto.......alitulia kidogo akisikilizia hii nafasi.......kwa sasa kaikosa anarudi kumpelekea shido Ruto
 
Basi mlikuwa mmepata cheo ambacho hakustahili! Baba wa mageuzo Afrika Mashariki ni Mwai Kibaki!
Mkuu aligeuka juzi tu. Kabla ya hapo alikuwa anastahili kabisa. BTW Mwai Kibaki na kuna ule uchaguzi waliokufa watu wengi kwa sababu aligeuza matokeo ambayo Raila ndiye alishinda. Japo walikuja kukubali kuunda katiba mpya lakini doa la ule uchaguzi halitafutika.
 
Raila Odinga alikuwa anaungwa mkono na Samia,Jakaya na wana ccm wengine kama Jesca Magufuli. Marais wote wa Africa mashariki pamoja na Jakaya walimpigia kampeni Raila Odinga lakini ameangukia pua.
Huwezi tokea Nchi ya ma snitch ukashinda,hata upigiwe kura na Malaika
 
Non sense excuses
Mtu kama wewe Hujui chochote kwenye siasa za kimataifa.
Niliwahi fanya kazi na taasisi za AUC nchi zinazoongea kifaransa ambazo nyingi ni za Africa magharibi za kislamu ndio zimetawala AUC hata wapiga kura ndio wengi na wanaumoja kuliko nchi zinazoongea kingereza...
Tafuta gazeti la leo wamechambua vitu

 
Mlikatazwa na nani nyie wengine kuwa na umoja?
 
Pole yake na hongera kwa aliyeshinda!
 
Mlikatazwa na nani nyie wengine kuwa na umoja?
Ndio maana nakuambia hujui chochote kafutilie siasa za ufaransa barani Africa.
Pia fuatlia kwanini Rais wa Kenya alimpigia simu Rais wa ufaransa kabla ya uchaguzi
 
Ndio maana nakuambia hujui chochote kafutilie siasa za ufaransa barani Africa.
Pia fuatlia kwanini Rais wa Kenya alimpigia simu Rais wa ufaransa kabla ya uchaguzi
Wewe unaejua Kwa nini hamkuungana mshindwe? 😁😁
 
..Rais Samia Suluhu ameshindwa kuwashawishi viongozi wenzake wampigie kura Raila Odinga.

..enzi za Nyerere, Mwinyi, Mkapa, na Kikwete, mgombea aliyeungwa mkono na Tanzania ilikuwa lazima ashinde.
Kimataifa Sasa hivi tuko hoi , Rais hana ushawishi pia Waziri wake Hana ushawishi
 
Mbona salim Ahmed hakuwa katibu wa UN licha ya kutakiwa na Hyyo unayemwita ana yshawishi lakini koffi Annan aliweza justify your comment
Hujui lolote ushawishi ulikuwa mkubwa sana tulishindwa kwa kura ya veto Toka Marekani
Lakini Salim alishinda
 
Wewe unaejua Kwa nini hamkuungana mshindwe? 😁😁
Nani kakuambia nahitaji ushindi
Si kila anayekupa mawazo tofauti yupo upande fulani mimi siko upande wowote na wala hainisaidii chochote..

Nimekupa uhalisia wa ya AUC na taasisi zake ufaransa Ina nguvu mno kwenye hiyo taasisi Hilo ni jambo halisi na wala halipingiki
 
Raida Odinga "baba" ameshindwa kupata kura za kutosha kushinda nafasi tajwa hapo juu
Ila kilichonifanya niandike hapa, sio habari ya kushindwa BALI ni Mshikamano walio onesha Wakenya wakati wote wa kugombe na hata baada ya kushindwa.
Yaani mtu wao akienda kutetea uwakilishi Nje wanakuwa na mshikamano wa hali ya juu hadi raha.
Iwe ni kwenye uwakilishi wa Riadha, mpira, masumbwi, siasa nk nk wanashikamana Wakenya wote kumpa sapoti. Nafikiri kuna namna Elimu yao inawapa maono (exposure) au inawasaidia kuondoa ujinga na husuda ya kutotaka mwingine apate/afanikiwe.
Hapa kwetu Simba/Yanga inacheza Nje wengine wanatumia hata fedha za kuihujumu...
Niliumia sana mchezaji wetu wa mpira alivyocheza ulaya watu wakawa wanatuma meseji za hovyo hadi huko kilabuni kwake...Inasikitisha sana!
Tuna la kujifunza!
 
Hujui lolote ushawishi ulikuwa mkubwa sana tulishindwa kwa kura ya veto Toka Marekani
Lakini Salim alishinda

..kulikuwa na upotoshaji mwingi.

..tafuta taarifa za vyombo vya kimataifa kuhusu uchaguzi huo.

..Usitegemee propaganda za Uhuru na Daily News wakati ule.

..Salim Salim hakuwa na nafasi ya kushinda UN.

..veto ya Marekani ilikuwa sababu mojawapo, lakini kura za Salim Salim zilikuwa zinapungua, na sio kuongezeka, kadiri zoezi lilivyokuwa linaendelea.
 
Inafurahisha sana hohohoho hoooooo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…