SubiriJibu
JF-Expert Member
- Jun 26, 2009
- 1,805
- 1,876
Mahamud Zuberi ndiye anayeendesha kipindi ambapo ni kipindi mahsusi kwa wachezaji wa zamami kueleza historia yao mpira hadi wakaibuka kuwa maarufu. Hivyo, watazamaji tunakuwa na hamu ya kumsikia mchezaji anachosema.
Hivyo, tungetarajia muda mwingi autumie mchezaji kuongea yeye atumie muda kidogo. Kinachoshangaza ni kwamba Mahamud Zuberi anageuka kuwa muongeaji mkuu kuliko mchezaji anayehojiwa. Wakati mwingine mchezaji anapojibu swali humkatisha na kuingiza hoja isiyo ya swali lile.
Binafsi nilipenda vipindi alivyowahoji akina Zamoyoni Mogella, Mohamed Mwameja, Edibily Lunyamila, Juma Pondamali, Makumbi Juma. Vipindi vyote hivi ukifuatilia kwenye YouTube utaona kwamba muda mwingi wa kipindi anaongea yeye zaidi kuliko mchezaji tunayemsikiliza. Siku amemkaribisha Edibily Lunyamila Mahmud Zuberi maana alikuwa anaongea yeye tu karibu asilimia 85 ya kipindi.
Hata stori zenyewe anazotupotezea muda ni zile anazojikita kuonyesha anavyoijua vizuri historia ya soka la Tanzania. Mahmoud azingatie kwamba hatuhitaji kumsikiliza yeye, sisi tunahitaji kumsikiliza Zamoyoni Mogella na wachezaji wengine wanaoalikwa pale Azam TV.
Kama anataka tujue anavyojua historia basi atayarishe kipindi kwa ajili yake tu ili aielezee vizuri soka hiyo hata kama ni masaa mawili.