Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 3,984
- 13,760
Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO), Maharage Chande amesema kuwa usafiri wa Treni ya Umeme unaotarajiwa kuanza Nchini utatumia umeme wa shirika hilo.
Amesema hayo alipokuwa akizungumza na Wanahabari Ijumaa ya Desemba 16, 2022, Dar es Salaam ambapo ametoa ufafanuzi huo baada ya kuulizwa swali na mwandishi wa habari kuhusu umeme utakaotumika kuendesha usafiri huo.
Maharage amesema: “Unapozungumzia umeme unaohitaji kuendesha mradi kama huo unatakiwa kujiuliza unatosha? Ubora wake upoje na ni umeme wa uhakika?
“Kwa treni yetu ya umeme mfano itakayokuwa inatoka Dar es Salaam kwenda Moro na Dodoma, hiyo ina njia yake, hivyo masuala ya uhakika, kutosha na ubora yamezingatiwa ndio maana nasema umeme wa TANESCO ndio utakaotokea.”