Maharage Chande: Treni ya umeme itatumia umeme wa TANESCO

Maharage Chande: Treni ya umeme itatumia umeme wa TANESCO

Vituko vitakuwa vingi, kuna lijamaa litamtumia nauli ashura nauli ya kwenda dar kwa treni umeme ukikatika wanalala njiani huku simu zimezima , treni nayo imezima, nyuzi za malalamiko humu zitakuwa nyingi kuliwa nauli kumbe tanesco ndo shida.
 
Maharage yenyewe kuiva kwa mkaa tabu ndio itakuwa umeme....Ndio maana tunasema ukila maharage mchana lazima usinzie tu....
 
Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO), Maharage Chande amesema kuwa usafiri wa Treni ya Umeme unaotarajiwa kuanza Nchini utatumia umeme wa shirika hilo.

Amesema hayo alipokuwa akizungumza na Wanahabari Ijumaa ya Desemba 16, 2022, Dar es Salaam ambapo ametoa ufafanuzi huo baada ya kuulizwa swali na mwandishi wa habari kuhusu umeme utakaotumika kuendesha usafiri huo.

Maharage amesema: “Unapozungumzia umeme unaohitaji kuendesha mradi kama huo unatakiwa kujiuliza unatosha? Ubora wake upoje na ni umeme wa uhakika?

“Kwa treni yetu ya umeme mfano itakayokuwa inatoka Dar es Salaam kwenda Moro na Dodoma, hiyo ina njia yake, hivyo masuala ya uhakika, kutosha na ubora yamezingatiwa ndio maana nasema umeme wa TANESCO ndio utakaotokea.”
Mbona bei ya usafiri huo ni kubwa na umeme ni wa Tanesco?
 
Hospital zinasimama kutoa huduma umeme unapokatika, kama umezidiwa Mungu tu ndo atakusimamia. Tren tajwa sasa, usafiri wa muda na usio wa uhakika maana muda wowote maharage akikorofishana na bb wake hasira zake zikahamia umemeni, wale wa tren mnalala maporini🤣🤣. Sababu aagh mabwawa yamekauka.😂😂😂
 
Kwani tuna umeme mwingine zaidi ya wa Tanesco...
 

Attachments

  • 2C83B7C8-871E-42FE-86B3-320761D523EF.jpeg
    2C83B7C8-871E-42FE-86B3-320761D523EF.jpeg
    34.6 KB · Views: 5
Back
Top Bottom