Maharage Chande: Tuache kupeana maneno tamutamu; bei ya Tsh 27,000/= haitoshi kuunganisha umeme

Hoja yako ni ya kijinga sana! Unaposafiri kwa chombo cha umma nauli yako inagharimia bei ya hicho chombo na gharama za uendeshaji au ni michango ya abiria wengine tena kwa muda mrefu!
Wewe ndio mjinga hapa, ingawa sio kawaida yangu kuita watu hivyo humu.
Hivi hujui kabla hao abiria kuchangia collectively hizo gharama za uendeshaji kuna tathmini fulani imefanyika kuamua wachangie kuanzia kiwango gani ili hilo lengo lifikiwe?! Pamoja na kufugia nywele, kichwa ni cha kufikiria pia.
 
Hiyo 60b waliyomlipa mhindi ingetosha kuunganisha wateja 170,000.

Tanesco ni shirika la hovyo, mnaingiza 150b kwa mwezi, mishahara inakula 100b. Kwa maana nyingine almost 67% ya mapato ya Tanesco yanaenda kulipa wafanyakazi.
 
Kwahiyo wewe usiye maharage unaamini kuna umeme wa 27,000/=!

Tupe mchanganuo wa huo umeme kuanzia generation mpaka distribution ili tuone.
Sijui kwa nini Watanzania mnaelezwa ila hamuelewi. Kuweka umeme nyumbani kwa mtu/mtumiaji ni uwekezaji wa TANESCO. Ni kuisaidia Tanesco kuwekeza kwenye biashara yake ya kuuza umeme; ili mtumiaji aweze kununua nishati na kuiingizia TANESCO mapato. Sasa hoja ya kusema tzs elfu 27 inatoka wapi wakati Tanesco inasaidiwa kuwekeza? Hizo elfu 27 ni mchango wa mwananchi/mtumiaji anayeweka umeme wa Tanesco nyumbani kwake. Kwa nini Tanesco ione mchngo hautoshi wakati ni uwekezaji wake (Tanesco)? Kwa nini Tanesco isiende kwenye soko la mitaji (DSE) kupata mtaji wa kutosha kusambaza (kuwekeza) umeme nchi nzima? Hoja ya Maharage imekaa kimaharage kweli. Ni mipasho tu. Sijui mzaramo huyu ndugu?!
 
Kwanza gharama za kuunganisha umeme ilitakiwa zisiwepo kabisa.
Leta huduma nilipie huduma.
Nafikri sector hii ya umeme sector binafsi zingeruhusiwa kusingejuwa na upurusi huu.
 
Kwani sisi Wananchi ndo tulipendekeza hiyo bei?
 
Na tatizo lingine la sisi Watanzania ni ule ujuaji uliopitiliza na kuona wengine wote wako blank. Una uhakika kuna hiyo source ya kutoa mtaji wa kufanya yote hayo?!
Washauri basi na Dstv Na akina Azam wasiuze Decoders na Dishes wafunge tu tutalipa subscription..
 
Kww kukusaidia tu hiyo ni hela ya uhakika wao kuipata

Sent using Jamii Forums mobile app
 
27 000,kwakweli tusidanganyane.
Nilitumia 500,000+ mpk kuweka kwa bi mkubwa.
Acha hela ndogo za chai kwa wafanyakazi watanesco.
Na ni zamani tu.
Sasa 27 leo itawezekana vp?
Mkuu hata kwenye miaka ya nyuma 2000 - 2010 ilikuwa 600, 000/- lakini bado TANESCO ilikuwa ina lialia tu. Ni wakati sasa kwa Shirika hili kufumuliwa, ikiwa na pamoja na complimentally za kuwapatia baadhi ya watu unit za bure pamoja na wafanyakazi wake
Siyo bure. Ni kodi zinatumika
Mkuu watu kama hao ni wengi sana ambao hawajitambui kwamba tunalipa kodi nyingi sana. Nadhani TANESCO inaweza kuongoza kwa kukusanya fedha nyingi sana kutoka kwa mwananchi mnyonge kuliko shirika lolote kwa njia za kodi e.g VAT, REA, SERVICE LINE, RUZUKU na BAJETI YA SERIKALI hapo bado Luku, nguzo, survey na kuunganishiwa umeme. Wanamatumizi ya kifaghari na anasa kwa fedha za Watanzania wanyonge.
 
Mkuu Crocodile umekuje siku hizi? Kwani hujui kwamba TANESCO ni shirika la Umaa ambalo pamoja na kuwakamua Watanzania pia linatumia fedha zetu kutoka HAZINA? Hao akina Dstv na wa aina yake wao ni mashirika ya Watu binafsi, hawali kodi zetu kutoka HAZINA.
 
Mkuu tunaye mwongelea alipe 27, 000/- watu wa vijijini. Vitu ulivyo taja pamoja na bei zake wao hawana uwezo huo, sanasana tv inchi 14 ya 50 - 70, 000/- simu ya 10 - 12, 000/- hizo harusi kwa asilimia 90% - 99% ni MKEKA TU.
 
Ila kiuhalisia hiyo bei ni hasara kwa shirika
Kwanza elewa umeme ni huduma, huenda bei ni hasara, hivyo serikali inatakiwa kutoka ruzuku kwe Hali Kama hiyo,wkt wa Magu iliwezekana Leo pamoja na tozo za miamala na huu uombaomba inashindikanaje?
 
Kwahiyo wewe usiye maharage unaamini kuna umeme wa 27,000/=!

Tupe mchanganuo wa huo umeme kuanzia generation mpaka distribution ili tuone.
logically umeme kuingiziwa kwa tsh27000, ni siasa za mwendazake ili kujiandalia njia ya kukaa madarakani milele,
Ila kiuhalisia kuingiza umeme kwa elfu 27 ni impossible hata miradi ya REA wanaingiza umeme kwa tsh27000 kwa sababu gharama nyingi zinakuwa covered wanapofanya project estimation .
 
Bila shaka kichwa chako kimejaa kamasi! Unadhani hizi bili za umeme tinazolipa hazijumlishi hayo! Isitoshe miundombinu bado ni mali ya tanesco kwa hiyo wanapotoza nyaya na nguzo ni wizi wa mchana kweupe!
 
Mkuu Mundaliku uko poa kabisa, mbaya na kichekesho ni kwamba unalipia nguzo 2 na unawalipa ths. 600, 000/- na zaidi alafu (then) nguzo hizo wanakuambia sio zako bali ni za TANESCO na wanaanza kuzitumia kwa kuwaunganishia wengine wakati nguzo hizo nimenunua mimi, sasa hapo nani anaibiwa au ANADHURUMIWA?
 
Tunafanya kosa kusahau kuwa gharama haziko kwenye kuunganishia wateja wapya, tu, kuna ku-maintain na wale waliopo. Je hizo kodi zetu zinatosha au waongeze tozo?
 
Pamoja na shirika hili kutakiwa kujiendesha kwa faida lakini ijulikane kuwa umeme ni moja ya huduma za kijamii inayopaswa kutolewa kwa gharama nafuu.

Huduma za jamii hazipaswi kufanyika kibiashara.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…