Maharage Chande: Tuache kupeana maneno tamutamu; bei ya Tsh 27,000/= haitoshi kuunganisha umeme

Hoja yako ni ya kijinga sana! Unaposafiri kwa chombo cha umma nauli yako inagharimia bei ya hicho chombo na gharama za uendeshaji au ni michango ya abiria wengine tena kwa muda mrefu!
Wewe ndio mjinga hapa, ingawa sio kawaida yangu kuita watu hivyo humu.
Hivi hujui kabla hao abiria kuchangia collectively hizo gharama za uendeshaji kuna tathmini fulani imefanyika kuamua wachangie kuanzia kiwango gani ili hilo lengo lifikiwe?! Pamoja na kufugia nywele, kichwa ni cha kufikiria pia.
 
Leo tarehe 23.02.2022 mkurugenzi wa TANESCO, MAHARAGE CHANDE ameongea na vyombo vya habari kwa kueleza umma kuwa hakuna umeme wa tsh 27, 000/= tuache kupeana maneno matamu matamu katika kuendesha shirika hilo. Amesema ni vigumu sana kutofautisha mjini na vijijini kwani wote wanahitaji huduma hiyo kitu ambacho inasababisha shirika hilo kujiendesha kwa hasara kubwa!

Aidha kwa maoni yangu waziri wa nishati na Naibu wake je wakati wakiwasilisha taarifa mbalimbali za utendaji wa shirika hilo hawakai na wataalamu wakaambiwa kuhusu bei hizo za kuunganishiwa umeme?

Kutokana na kauli hizo kati ya waziri na mkurugenzi wa Tanesco ni kauli zipi ambazo umma utakuja kuziamini kutokana na mkanga'nyiko huo ambao hauleweki wa umeme wa tsh 27,000/=?

Ni hatari sana kwa mkurugenzi wa Tanesco kuambia umma kuwa unawezaje kununua tv ya sh 1,000,000/= halafu uhitaji umeme wa tsh 27000/= akumbuke kuwa hii nchi ni ya kwetu sote hata hivyo kutokana na nyakati tulizopo tulihitaji umeme wa gharama ya chini na siyo kukatisha tamaa umma kuwa hakuna umeme wa tsh 27,000/=.

Kwa hali hiyo Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ana kila sababu kufatilia kwa karibu utendaji wa shiraka hilo na Wizara ya Nishati kwa ujumla kwani tayari wananchi wameshaanza kutokuwa na imani na watendaji wa Tanesco na wizara husika.
Hiyo 60b waliyomlipa mhindi ingetosha kuunganisha wateja 170,000.

Tanesco ni shirika la hovyo, mnaingiza 150b kwa mwezi, mishahara inakula 100b. Kwa maana nyingine almost 67% ya mapato ya Tanesco yanaenda kulipa wafanyakazi.
 
Kwahiyo wewe usiye maharage unaamini kuna umeme wa 27,000/=!

Tupe mchanganuo wa huo umeme kuanzia generation mpaka distribution ili tuone.
Sijui kwa nini Watanzania mnaelezwa ila hamuelewi. Kuweka umeme nyumbani kwa mtu/mtumiaji ni uwekezaji wa TANESCO. Ni kuisaidia Tanesco kuwekeza kwenye biashara yake ya kuuza umeme; ili mtumiaji aweze kununua nishati na kuiingizia TANESCO mapato. Sasa hoja ya kusema tzs elfu 27 inatoka wapi wakati Tanesco inasaidiwa kuwekeza? Hizo elfu 27 ni mchango wa mwananchi/mtumiaji anayeweka umeme wa Tanesco nyumbani kwake. Kwa nini Tanesco ione mchngo hautoshi wakati ni uwekezaji wake (Tanesco)? Kwa nini Tanesco isiende kwenye soko la mitaji (DSE) kupata mtaji wa kutosha kusambaza (kuwekeza) umeme nchi nzima? Hoja ya Maharage imekaa kimaharage kweli. Ni mipasho tu. Sijui mzaramo huyu ndugu?!
 
Kwanza gharama za kuunganisha umeme ilitakiwa zisiwepo kabisa.
Leta huduma nilipie huduma.
Nafikri sector hii ya umeme sector binafsi zingeruhusiwa kusingejuwa na upurusi huu.
 
Leo tarehe 23.02.2022 mkurugenzi wa TANESCO, MAHARAGE CHANDE ameongea na vyombo vya habari kwa kueleza umma kuwa hakuna umeme wa tsh 27, 000/= tuache kupeana maneno matamu matamu katika kuendesha shirika hilo. Amesema ni vigumu sana kutofautisha mjini na vijijini kwani wote wanahitaji huduma hiyo kitu ambacho inasababisha shirika hilo kujiendesha kwa hasara kubwa!

Aidha kwa maoni yangu waziri wa nishati na Naibu wake je wakati wakiwasilisha taarifa mbalimbali za utendaji wa shirika hilo hawakai na wataalamu wakaambiwa kuhusu bei hizo za kuunganishiwa umeme?

Kutokana na kauli hizo kati ya waziri na mkurugenzi wa Tanesco ni kauli zipi ambazo umma utakuja kuziamini kutokana na mkanga'nyiko huo ambao hauleweki wa umeme wa tsh 27,000/=?

Ni hatari sana kwa mkurugenzi wa Tanesco kuambia umma kuwa unawezaje kununua tv ya sh 1,000,000/= halafu uhitaji umeme wa tsh 27000/= akumbuke kuwa hii nchi ni ya kwetu sote hata hivyo kutokana na nyakati tulizopo tulihitaji umeme wa gharama ya chini na siyo kukatisha tamaa umma kuwa hakuna umeme wa tsh 27,000/=.

Kwa hali hiyo Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ana kila sababu kufatilia kwa karibu utendaji wa shiraka hilo na Wizara ya Nishati kwa ujumla kwani tayari wananchi wameshaanza kutokuwa na imani na watendaji wa Tanesco na wizara husika.
Kwani sisi Wananchi ndo tulipendekeza hiyo bei?
 
Sijui kwa nini Watanzania mnaelezwa ila hamuelewi. Kuweka umeme nyumbani kwa mtu/mtumiaji ni uwekezaji wa TANESCO. Ni kuisaidia Tanesco kuwekeza kwenye biashara yake ya kuuza umeme; ili mtumiaji aweze kununua nishati na kuiingizia TANESCO mapato. Sasa hoja ya kusema tzs elfu 27 inatoka wapi wakati Tanesco inasaidiwa kuwekeza? Hizo elfu 27 ni mchango wa mwananchi/mtumiaji anayeweka umeme wa Tanesco nyumbani kwake. Kwa nini Tanesco ione mchngo hautoshi wakati ni uwekezaji wake (Tanesco)? Kwa nini Tanesco isiende kwenye soko la mitaji (DSE) kupata mtaji wa kutosha kusambaza (kuwekeza) umeme nchi nzima? Hoja ya Maharage imekaa kimaharage kweli. Ni mipasho tu. Sijui mzaramo huyu ndugu?!
Na tatizo lingine la sisi Watanzania ni ule ujuaji uliopitiliza na kuona wengine wote wako blank. Una uhakika kuna hiyo source ya kutoa mtaji wa kufanya yote hayo?!
Washauri basi na Dstv Na akina Azam wasiuze Decoders na Dishes wafunge tu tutalipa subscription..
 
Mkuu, hakuna hasara yeyote kwa shirika. Nchi nyingi watu hata hawajui hizo bei za nguzo kwa kuwa ni sehemu ya huduma za kampuni. Yaani unaponunua kiwanja unakuta tayari kuna umeme na maji. Wewe gharama yako ni kuunginishiwa tu kutoka barabarani kuja nyumbani kwako. Miji mingi kwa sasa hata tu Africa hasa nchi za kusini wanatoa manguzo ya umeme mitaani. Umeme unapitishwa underground. Manguzo na manyaya kukatishakatisha mabarabara yanachafua miji tu. Sasa kama Tanesco wakiamua kupitisha umeme undeground kama nchi za wenzetu ina maana watadai mteja achimbe mtaro wa kupitisha hizo nyaya?

Yaani wanachofanya Tanesco ni sawa na Vodacom kusema kama watu wa let say Sinza wanataka huduma ya simu basi walipie gharama za antena kwenye hilo eneo. Hiyo umeiona wapi? Wao kama kampuni walitakiwa wapeleke umeme kila mahali labda kwa wale ambao wako mbali na wamejitenga. Charges zao zinatakiwa kuwa za kuunganisha umeme tu kutoka kwenye nguzo kuja nyumbani kwako. Hizo gharama za nguzo zitakuwa recovered na bill za umeme za kila mwezi overtime.

Tujiulize kidogo, faida wanayoipata Tanesco kwa mteja moja kwa miaka 10 ni sawa na nguzo ngapi? Wanachotakiwa kufanya hawa Tanesco siyo lazima warudishe hela yao siku hiyo hiyo kwa kila huduma wanayoitoa. Kila mteja wanayemuunganishia umeme wanauhakika atalipia hiyo huduma kwa miaka mingi ijayo (> 30 years) hivyo ni pesa nyingi wanategemea kuipata kwa kila mteja. Hata kwenye biashara ndogo tu faida haiji siku moja baada ya kuifungua.
Kww kukusaidia tu hiyo ni hela ya uhakika wao kuipata

Sent using Jamii Forums mobile app
 
27 000,kwakweli tusidanganyane.
Nilitumia 500,000+ mpk kuweka kwa bi mkubwa.
Acha hela ndogo za chai kwa wafanyakazi watanesco.
Na ni zamani tu.
Sasa 27 leo itawezekana vp?
Mkuu hata kwenye miaka ya nyuma 2000 - 2010 ilikuwa 600, 000/- lakini bado TANESCO ilikuwa ina lialia tu. Ni wakati sasa kwa Shirika hili kufumuliwa, ikiwa na pamoja na complimentally za kuwapatia baadhi ya watu unit za bure pamoja na wafanyakazi wake
Siyo bure. Ni kodi zinatumika
Mkuu watu kama hao ni wengi sana ambao hawajitambui kwamba tunalipa kodi nyingi sana. Nadhani TANESCO inaweza kuongoza kwa kukusanya fedha nyingi sana kutoka kwa mwananchi mnyonge kuliko shirika lolote kwa njia za kodi e.g VAT, REA, SERVICE LINE, RUZUKU na BAJETI YA SERIKALI hapo bado Luku, nguzo, survey na kuunganishiwa umeme. Wanamatumizi ya kifaghari na anasa kwa fedha za Watanzania wanyonge.
 
Na tatizo lingine la sisi Watanzania ni ule ujuaji uliopitiliza na kuona wengine wote wako blank. Una uhakika kuna hiyo source ya kutoa mtaji wa kufanya yote hayo?!
Washauri basi na Dstv Na akina Azam wasiuze Decoders na Dishes wafunge tu tutalipa subscription..
Mkuu Crocodile umekuje siku hizi? Kwani hujui kwamba TANESCO ni shirika la Umaa ambalo pamoja na kuwakamua Watanzania pia linatumia fedha zetu kutoka HAZINA? Hao akina Dstv na wa aina yake wao ni mashirika ya Watu binafsi, hawali kodi zetu kutoka HAZINA.
 
una
tv 2,500, 000/=umenuna kwa pesa taslimu
simu 1.500,000/=umenuna kwa pesa taslimu
unachanga na kwenda harusini mara 3 @ 70,000 kiwango cha double= 210,000/=

Halafu unamtisha mwanasiasa na kura yako akupe umeme kwa 27000 kwa kilio kikubwa kuwa wew ni maskini Mnyonge?
Maharage uko sawa- tuambiane ukweli ili tufike
Mkuu tunaye mwongelea alipe 27, 000/- watu wa vijijini. Vitu ulivyo taja pamoja na bei zake wao hawana uwezo huo, sanasana tv inchi 14 ya 50 - 70, 000/- simu ya 10 - 12, 000/- hizo harusi kwa asilimia 90% - 99% ni MKEKA TU.
 
Ila kiuhalisia hiyo bei ni hasara kwa shirika
Kwanza elewa umeme ni huduma, huenda bei ni hasara, hivyo serikali inatakiwa kutoka ruzuku kwe Hali Kama hiyo,wkt wa Magu iliwezekana Leo pamoja na tozo za miamala na huu uombaomba inashindikanaje?
 
Kwahiyo wewe usiye maharage unaamini kuna umeme wa 27,000/=!

Tupe mchanganuo wa huo umeme kuanzia generation mpaka distribution ili tuone.
logically umeme kuingiziwa kwa tsh27000, ni siasa za mwendazake ili kujiandalia njia ya kukaa madarakani milele,
Ila kiuhalisia kuingiza umeme kwa elfu 27 ni impossible hata miradi ya REA wanaingiza umeme kwa tsh27000 kwa sababu gharama nyingi zinakuwa covered wanapofanya project estimation .
 
Wewe ndio mjinga hapa, ingawa sio kawaida yangu kuita watu hivyo humu.
Hivi hujui kabla hao abiria kuchangia collectively hizo gharama za uendeshaji kuna tathmini fulani imefanyika kuamua wachangie kuanzia kiwango gani ili hilo lengo lifikiwe?! Pamoja na kufugia nywele, kichwa ni cha kufikiria pia.
Bila shaka kichwa chako kimejaa kamasi! Unadhani hizi bili za umeme tinazolipa hazijumlishi hayo! Isitoshe miundombinu bado ni mali ya tanesco kwa hiyo wanapotoza nyaya na nguzo ni wizi wa mchana kweupe!
 
Ukinunua tv ya 1000,000/ na kuunganishiwa umeme kwa 27k Ni upuuzi kutumia kigezo hicho. Nikinunua tv inakuwa Mali yangu moja kwa moja,ukiniunganishia umeme nikagharamia nguzo,hizo nguzo bado ni mali ya Tanesco na nitaendelea kulipia umeme pasipo kupata exemption ya muda fulani kufidia nguzo nilizogharamia. Huyo mkurugenzi hoja yake ni mfu. Wanamdanganya Rais na kumchonganisha na wananchi.
Mkuu Mundaliku uko poa kabisa, mbaya na kichekesho ni kwamba unalipia nguzo 2 na unawalipa ths. 600, 000/- na zaidi alafu (then) nguzo hizo wanakuambia sio zako bali ni za TANESCO na wanaanza kuzitumia kwa kuwaunganishia wengine wakati nguzo hizo nimenunua mimi, sasa hapo nani anaibiwa au ANADHURUMIWA?
 
Mkuu Crocodile umekuje siku hizi? Kwani hujui kwamba TANESCO ni shirika la Umaa ambalo pamoja na kuwakamua Watanzania pia linatumia fedha zetu kutoka HAZINA? Hao akina Dstv na wa aina yake wao ni mashirika ya Watu binafsi, hawali kodi zetu kutoka HAZINA.
Tunafanya kosa kusahau kuwa gharama haziko kwenye kuunganishia wateja wapya, tu, kuna ku-maintain na wale waliopo. Je hizo kodi zetu zinatosha au waongeze tozo?
 
Leo tarehe 23.02.2022 mkurugenzi wa TANESCO, MAHARAGE CHANDE ameongea na vyombo vya habari kwa kueleza umma kuwa hakuna umeme wa tsh 27, 000/= tuache kupeana maneno matamu matamu katika kuendesha shirika hilo. Amesema ni vigumu sana kutofautisha mjini na vijijini kwani wote wanahitaji huduma hiyo kitu ambacho inasababisha shirika hilo kujiendesha kwa hasara kubwa!

Aidha kwa maoni yangu waziri wa nishati na Naibu wake je wakati wakiwasilisha taarifa mbalimbali za utendaji wa shirika hilo hawakai na wataalamu wakaambiwa kuhusu bei hizo za kuunganishiwa umeme?

Kutokana na kauli hizo kati ya waziri na mkurugenzi wa Tanesco ni kauli zipi ambazo umma utakuja kuziamini kutokana na mkanga'nyiko huo ambao hauleweki wa umeme wa tsh 27,000/=?

Ni hatari sana kwa mkurugenzi wa Tanesco kuambia umma kuwa unawezaje kununua tv ya sh 1,000,000/= halafu uhitaji umeme wa tsh 27000/= akumbuke kuwa hii nchi ni ya kwetu sote hata hivyo kutokana na nyakati tulizopo tulihitaji umeme wa gharama ya chini na siyo kukatisha tamaa umma kuwa hakuna umeme wa tsh 27,000/=.

Kwa hali hiyo Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ana kila sababu kufatilia kwa karibu utendaji wa shiraka hilo na Wizara ya Nishati kwa ujumla kwani tayari wananchi wameshaanza kutokuwa na imani na watendaji wa Tanesco na wizara husika.
Pamoja na shirika hili kutakiwa kujiendesha kwa faida lakini ijulikane kuwa umeme ni moja ya huduma za kijamii inayopaswa kutolewa kwa gharama nafuu.

Huduma za jamii hazipaswi kufanyika kibiashara.
 
Back
Top Bottom