-Serikali iwe makini katika kuteua watendaji wakuu,wa mashirika makubwa yenye kuhitaji taaluma maalum Kama TANESCO hasa kwenye nafasi ya juu kama ya CEO.
-Mchakato wa kumpata CEO wa TANESCO,sijui kama ulifuata utaratibu,(kutangazwa,usaili na vetting)
-CEO wa TANESCO hafahamu vema majukumu na changamoto za kazi yake.
-Ninadhani CEO wa TANESCO Ni zao la Mamlaka ya uteuzi kupelekewa majina ya ma- CEO waliopo Tanzania,(wanaopeleka Ni ndugu na marafiki) na kura ikamwangukia Maharage wa DSTV.
-kosa lilianzia hapo DSTV na Shirika Kama TANESCO ni tofauti Sana.
-CEO wa TANESCO anapaswa kujua kuwa, Umeme wa shs27,000 ni majukumu ya REA na siyo TANESCO .
-watumiaji wa umeme wanachangia 3% kwenye REA,
-
Ushauri
1). Serikali ipitie upya maamuzi yake kuhusu hawa ma-CEO wanaopendekezwa kwa msingi ya undugu au urafiki na wasaidizi wa Mamlaka za uteuzi.
2).CEO wa TANESCO ameishiwa pumzi na uwezo mdogo,apangiwe majukumu mengine.
3). Serikali ichukue mkopo wa riba nafuu kutoka benki ya dunia au IMF au Exim bank ya China ili kuwekeza kwenye miundo mbinu ya umeme vijijini na Mijini.
4). iombe msaada kwenye taasisi za kimataifa,kutatua changamoto ya miundo mbinu ya umeme vijijini na Mijini.
5). Serikali iwe inatangaza na kushindanisha waombaji nafasi za watendaji wakuu wa Taasisi kwa watanzania walioko ndani na nje ya nchi yetu.
6). Rais SSH, wasaidizi wako,wanakuangusha,wanataka kukugombanisha na wapiga kura wako, umeme siyo anasa tena,ni huduma muhimu.
7). Shirika Kama TANESCO CEO wake, awe anaandaliwa kutoka ndani ya taasisi (badala ya kutoka nje ya taasisi,ikibidi baada ya kufanya kazi ndani,anaweza kupelekwa kwenye taasisi mbalimbali ndani na nje kwenda kujifunza zaidi).
8). TANESCO,iweke utaratibu wa kukoposha nguzo na nyaya kwa wateja wa mijini wanao hitaji zaidi ya nguzo moja, halafu walipe deni ndani ya miaka 3 kupitia Luku