Maharage Chande wa TANESCO ameingiaje utumishi wa umma akiwa na umri zaidi ya miaka 45?

Maharage Chande wa TANESCO ameingiaje utumishi wa umma akiwa na umri zaidi ya miaka 45?

Verrazanno

JF-Expert Member
Joined
Sep 15, 2021
Posts
454
Reaction score
1,011
Maharage Chande, Mkurugenzi Mtendaji mpya wa TANESCO ana umri zaidi ya miaka 45. Ameingiaje kwenye utumishi wa Umma ?

Au ni urafiki wake na Waziri wa Nishati January Makamba (cronyism) ndio umempa upendeleo huu ? Makamba ndio amepeleka jina kwa Rais. Rais hamjui Maharage.

Matokeo ya cronyism ndio haya: Chande hana background au experience ya utumishi wa umma, wala kazi za shirika la nishati wala shirika la fani yeyote lenye ukubwa na ugumu wa uendeshaji kama TANESCO. Ametokea DSTV na kabla ya hapo Vodacom.

Kituko cha kwanza cha Chande alikitoa kwenye hotuba yake ya utambulisho mbele ya hadhara, waandishi, wateule wenzie wapya pamoja na Waziri.

Akasema anataka PAY-FOR-PERFOMANCE, mfumo wa ulipaji kulingana na ufanisi kiutendaji. Toka lini kwenye public sector mtu analipwa tofauti na salary scale yake ??? Huyu jamaa hana clue na mifumo ya ujira za utumishi wa umma. Speech yake ya kwanza anatueleza ndoto za Alinacha za jinsi watakavyolipana badala ya matatizo ya upatikanaji umeme wa uhakika.

Tunaomba January Makamba ujali na uwe serious na kazi yako. Tunajua huna sana uchungu na wananchi na kuhuwahi kusota kupata kazi hizi kwa vile ulibebwa na majina ya baba zako Yusufu (nepotism) na Jakaya (cronyism), na siku zote vyeo vimekuwa vikikujia, kuondoka na kurudi kirahisi rahisi. Jisafishe, tunaomba uanze kujali.
 
Kweli hakuwahi kuwa mtumishi wa umma ,ila aliwahi kuwa COO NBC bank na huku serikalini kumeoza kunahitaji watu wenye energy na vision kutoka private sector ,age sio tatizo kwa level ya cheo chake.
 
Kweli hakuwahi kuwa mtumishi wa umma ,ila aliwahi kuwa COO NBC bank na huku serikalini kumeoza kunahitaji watu wenye energy na vision kutoka private sector ,age sio tatizo kwa level ya cheo chake.
Kwa nini age sio tatizo kwa age ya cheo chake ?

Unajua ni kwa nini huwezi kuingia kwenye utumishi ukishazidi miaka 45 ?
 
Maharage Chande, Mkurugenzi Mtendaji mpya wa TANESCO ana umri zaidi ya miaka 45. Ameingiaje kwenye utumishi wa Umma ?

Au ni urafiki wake na Waziri wa Nishati January Makamba (cronyism) ndio umempa upendeleo huu ? Makamba ndio amepeleka jina kwa Rais. Rais
Majungu tu! Ufanyaji kazi kwa mazoea ndiyo unakusumbua!
 
kwa nini age sio tatizo kwa age ya cheo chake ?

unajua ni kwa nini huwezi kuingia kwenye utumishi ukishazidi miaka 45 ?

Wakurugenz wa halmashauri walioteuliwa na mama samia karibu wote hawajawai kuwa watumishi wa uma.

Pili nafasi za ukurugenzi ni nafasi za mkataba. Tangu zamani hazinaga kufata umri wa miaka 45.

Nafasi za chini ndio wameweka umri sababu makato ya mifuko ya pensheni uweze kuchangia kwa miaka isiyopungua 15
 
Ukurugenzi wa Halmashauri ni kazi ya Mkataba ?
 
Kwani mkurugenzi aliyeondoka aliingia Tanesco akiwa na umri gani?
Tumeona watu hawajawahi kua class monitors lkn wakaleta matokeo chanya. Unamkumbuka Prof. Luhanga VC UDSM?
Acheni hizo. Maharage piga kazi. Prove them wrong.
 
Umezoea kufanya kazi kwa mazoea unaogopa kuambiwa utalipwa kutokana na performance! Amka dogo, acha mazoea yasiyo na tija. Fanya kazi.

Unashangaa Beans kuingia utumishi wa umma at 45, hao makada ma DED wameingia na umri gani? Waziri wa ulinzi kaingia akiwa na miaka mingapi?
 
Back
Top Bottom