Herbalist Dr MziziMkavu
JF-Expert Member
- Feb 3, 2009
- 42,872
- 34,363

Recipe/Mapishi ya MAIDANA DEMARNY
Mahitaji
- Maharage 1/2
- Chumvi kijiko cha chai 1
- Nazi kopo 1/ nazi ya kawaida 1 kubwa.
- Kitunguu maji 1
- Kitunguu swaumu punje 2
- Binzari kidogo
1. Chemsha maharage hadi yaive ila yasipondeke .
2.Maji yakikaribia kukauka weka kitunguu maji,kitunguu saumu na chumvi acha hadi maji yakauke weka tui la nazi kidogo lile jepesi acha hadi likauke weka pembeni.
3. Chukua tui zito weka katika sufiria Tia binzari koroga hadi liwe zito usiachie mkono tui litakatika.
4. Likishakuwa zito epua acha lipoe halafu mimina juu ya yale maharage
Unaweza kula na maandazi,chapati au wali.