Freema Agyeman
JF-Expert Member
- Mar 3, 2011
- 3,666
- 3,532
Ndio, kwani akiwa anaolewa mara ya pili au ya tatu ndio hafai kupewa zawadi?
Hata aolewe mara saba wa sabiini, ana hiari ya kuamua adai mahari au la
Unataka kutungiwa shairi ndiyo ukubali kufunga ndoa? Kama yeye si stadi wa utunzi je?
Ujuavyo wewe si sahihi. Jamii za nchi za Asia kama Indonesia, Malaysia, Brunei na Kiarabu mahari anapanga binti na anakabidhiwa yeye akishayapokea.
Namjua dada mmoja Mu-Indonesia, alidai mahari mwanamme ajifundishe Quran yote kwa moyo kisha ndio ende akamuoe (hili halikuwa na faida kwa mwanamke moja kwa moja, alidhani akiweza hilo maisha yake yatakwenda kwa taratibu za dini anayoiamini tu)
Kwa hiyo wasiodai mali wapo tele duniani.
Hmmmm....hapa sasa itabidi watu tuzame kwenye nyenzo zetu tulichambue vizuri hilo neno 'mahari'.
Manake huo mfano wa huyo Muindonesia kwangu mimi ni kama sharti na si mahari. Sharti ni kwamba, ujifunze kwanza quran tukufu ndiyo unioe (tuoane).
Na kwa mantiki hiyo binti anaweza kusema kapimwe kwanza magonjwa ya zinaa na kama vipimo vikirudi na kuonyesha huna ndiyo unioe (tuoane)...? Na hii iitwe mahari?
Duh, kumbe kuolewa mara nyingi dili.
Nikiolewa mara nyingine mahari yangu itakuwa shamba at least acre 1 lenye minazi na minanas
Hahaha kwa hiyo wadai mahari wote ni "chuna buzi"!!!
Nyinyi ndo mnaiharibu dhana nzima ya mahari, mie nataka kudai kutungiwa shairi, hapo chuna buzi imehusikaje?
Nasindikiza kwa muziki
"Si hasara asilani, nyuki kufa asalini
Tuchekeni, furahani haha haha haha haha
hahaha, ujue inategemea sheria gani zinafuatwa. Kama hapo kuna sheria za Kiislam zinahusika, ukijiachisha bila ya sababu ya msingi unatakiwa urudishe mahari ya watu.
Sasa dili linaweza kukutumbukia nyongo :lol:
Sina shida na mahari, shida yangu ni wanatumia vigezo gani kufika hapo kwenye Million 4 au Elfu 40
Gaijin naomba vigezo tafadhali
Mahari uzaramoni unaweza kuambiwa 25,000/=
Basi sikilizia vikolokolo vingine hivyo, sijui bakora ya babu, mkoja, sijui usinga vitu kibao.
Ambavyo hata 100,000/= havifiki.
Hapo sasa ukimwambia mtu hii ni zawadi tu ya kuonyesha upendo anaelewa.
Sio mahari milioni nne? Kwani ndio mmesikia mahari ndio mwisho wa kushukuru kwa familia?
Matokeo yake, ukichanganya huu upuuzi wa mahari za kukomoana na harusi za kifahari, mtakuta watu wanaamua kuishi pamoja tu.
Utambulisho wa kwanza kwa wazazi mamaa kabeba ujauzito tayari.
Sasa nyinyi mnataka kuharibu kwa kuharamisha dhana nzima ya mahari kwa ukosefu wa hikma wa watu wachache.
Mahari si lazima pesa na nawajua watu waliosema leteni chochote, wakaletewa mahari pesa nyingi wakazirudisha, wakasema haifai.
Harusi za kifahari mnataka wenyewe, kwani lazima? Mwanamke kama ana hamu ya kufanya harusi ya kifakhari si afanye kwa pesa zake? Wewe mwanamme imekuhusu na nini? Mengine mnajitakia wenyewe kisha mnalalama. Ati mwanamme amnunulie mwanamke shela sijui na mambo mengine.....why???
Alaa, sasa kama 'simuelewi' (nitakuwa naikalifisha nafsi yangu) kwa nini asiniache/nisimuache niolewe na yule 'ninayemuelewa'.
Hivi mantiki ya kutoa mahari ni nini?
Kama humuelewi unamuacha/anakuacha lakini ndo mahari jamaa akiyadai inabidi uyakabidhishe kwake pamoja na inflation. Hakuna kukalifisha nafsi, ila pia hakuna dili
As far as I know, ni zawadi. Kuonyesha upendo kwa mwanamke anaeolewa na familia yake.
Hivi mantiki ya kutoa mahari ni nini?
Kujitoa kumo na mahari inarudishwa pale ambapo hakuna jimai. Kama alishagusa mahari/zawadi haiwezi rudi; si keshafaidi bana.
Kuna mila nyingine mahari ni ya 'bi harusi', familia haina hati miliki kabisa na chochote kila. Hebu fikiria wewe umetaka 'zawadi' ya shairi au insha, familia hapo inapata nini?
Hawawezi kutaka vyote viwili kwa pamoja, la sivyo mahari itolewe na pande zote, kuwe na exchange of gifts tu.