Hivi mantiki ya kutoa mahari ni nini?
Originally ilikuwa a token of appreciation (chauvinist some may say) but several factors zimeibadilisha kabisa.
Kwanza zamani ilikuwa si nadra kukuta hata mahari kubwa inapotajwa, huwa haimalizwi. Mtu anatoa kiasi kidogo tu kinaitwa "kishikia mke" halafu anabaki forever indebted kwa familia ya mke wake. Na wengine hata walipokuwa na uwezo wa kuimaliza hawakuimaliza kama ishara kwamba shukurani ya kulelewa mke haiwezi kumalizwa.
Kuna baadhi ya jamii, kama Wasukuma kwa mfano. Mwanamme ukioa bila mahari huhesabiki kama umeoa, na mwanamke mzuri zaidi (some say mweupe zaidi) ndiye ana haki ya kudai mahari kubwa zaidi.
Kwa hiyo ungeweza kukuta baba anadaiwa mahari ambayo kashailipa kama mara mia kwa misaada mingine kwa upande wa wazazi wa mke.
Sasa siku hizi hizi habari za "mahari milioni nne" halafu tunapewa picha kwamba milioni nne isipokamilika hakuna ndoa, inaonekana imekaa kibiashara zaidi.
Wanawake inabidi wakubali moja.
A.Kuendelea kutolewa mahari na kuwa subservient kwa wanaume (wao wanaolewa, wanatolewa mahari, hawawezi kuwa sawa na wanaume, essentially utumwa fulani hivi).
B.Kukataa mahari na kudai usawa na wanaume.
Hawawezi kutaka vyote viwili kwa pamoja, la sivyo mahari itolewe na pande zote, kuwe na exchange of gifts tu.
Na wasituambie habari zaunyumba ni exchange kwa mahari kwa sababu that will just be prostituting the entire institution of marriage.
Sometimes I wonder if there is much of a difference anyway.