Mahari bei gani

Mahari bei gani

Sasa uwezo unao, tatizo ni nini?

Punguzeni ubahili. Princess wa Spain aliutoa mji mzima wa Bombay kwa Mfalme wa Uingereza kama mahari, itakuwa milioni nne hata gari hununui!

Kwa hiyo bidada maisha yangekuwa hivyo miji yetu yote si ingetolewa mahari pindi wakubwa waoanapo? Huyo Princess wa Spain alikuwa na uchungu gani na Boombay?
Nyie oleweni bure bwana, mnafanya ngono inazidi kuwapo pamoja na kuzalia nyumbani kwa sababu vijana wanaogopa bei zenu hizo...
M4 ndogo kwani we uliolewa/utaolewa kwa shilingi ngapi?
Mi mbona wife alikataa kuolewa kwa mahari japo nililazimisha kutoa? Na nlitoa kidogo tu na sasa niko na wife.
 
Naomba kuuliza - sasa kwa mfano mimi YATIMA - hizo milioni 4 si inabidi nichukue mwenyewe??? SINA BABA - SINA MAMA - SINA MJOMBA WALA SHANGAZI - SIN BIBI WALA BABU

Sina hata Mama au Baba wa Hiyari - Nimekulia mitaani - nikafanya biashara ndogo ndogo - Mungu akanibariki - ikaukua kidogo - nikajua kununua mitumba - kuvaa - kusuka nywele - na NIMEPENDEZA - jamaa ndio anataka kunioa - MAHARI AMPE NANI?? SI ANIPE MIMI YATIMA AU???????????

Naomba ushauri wenu - Great Thinkers!!!!!:smile-big:
Mahari siku zote ni ya yule bint anaye olewa, wengi watu hawajui mahari ni kwa sababu ya kumprotect yule mwanamke from suffering abuse.

The prophet(a.s.) said; The best women of my community are those of less dowries 😛oa
 
4,000,000/-,mshahara wa degree ya procurement 511,400/- KUZICHANGA MPAKA ZIFIKE MILIONNNE MIAKA SITA MMH BY MPIGAMSULI
 
Aiseee baba yangu huyo mkeo inaonekana unamkamua sana ndi maana ameamua kukukomoa
lipa kadri unavyotumia kama luku

mimi nilitoa debe 3 za mbege tu
 
Bei gani is right. Maana unanunua mtumwa.

Kesho keshokutwa ukimtwika mkeo utumwa atakataa?

Halafu ndo wanawake hawahawa wanaodai usawa? Au hawa wengine?

The entire institution of marriage is disillusioned and in a state of collapse, what remains is utapeli na biashara.

Hakuna bei gani is right wal bei gani is wrong.(hata angetumia "kiasi gani kinafaa," dhana ni ile ile)

Mahari ni zawadi kimsingi kwa hiyo inaweza kuwa kumfundisha kusoma na kuandika, pete ya bati au shehena nzima abebeshwayo ngamia. Zawadi haiwezi kupangiwa kiasi

Mwanamme anampa zawadi mwanamke kwa kukubali kuwa wake wa milele, kumzalia watoto na hata kuchukua jina lake wakati mwingi mwengine

Hakuna suala la utumwa hapo, mbona mwanamke anabadili jina na kuwa la mwanamme na hawi mtumwa wake?
 
Kama unamnunua basi akiingia ndani afanye afanyalo kuhakikisha pesa inarudi hiyo.......
 
Kwa hiyo bidada maisha yangekuwa hivyo miji yetu yote si ingetolewa mahari pindi wakubwa waoanapo? Huyo Princess wa Spain alikuwa na uchungu gani na Boombay?
Enzi za zamani miji ilikuwa mali ya mtu, ndio hiyo ilikuwa ikitolewa kama mahari. Enzi za siku hizi watu hawamiliki miji mizima lakini matajiri wenye uwezo wao, watoto wao wakiolewa hao wanaume huanzishiwa biashara, kampuni, au kununuliwa nyumba na makorokocho mengine. Tofauti ni kuwa hawaiti mahari bali zawadi.

Nyie oleweni bure bwana, mnafanya ngono inazidi kuwapo pamoja na kuzalia nyumbani kwa sababu vijana wanaogopa bei zenu hizo....

Hao wasooa hawajafungwa na mahari, hawajataka tu. Mahari inaweza kuwa neno moja tu, kalamu, au hata pesa kidogo za kununulia chakula cha mchana mmoja. Ni maelewano tu na mapenzi ya kweli yakiwepo.

M4 ndogo kwani we uliolewa/utaolewa kwa shilingi ngapi?
Mi mbona wife alikataa kuolewa kwa mahari japo nililazimisha kutoa?

Hoja hapa sio mie nitaolewa kwa shilingi ngapi, maana inaweza isiwe pesa hasa nikaamua anifundishe ujuzi wake mmoja alonao, aniandikie shairi la beti tatu au hata kokwa moja ya tende.

Hoja iliyopo ni mahari yana kikomo? Uchaguzi wangu binafsi hauwezi kuhalalisha au kuharamisha mahari kwa wengine.
 
kwa maana hiyo bei halisi ya ng'ombe sio muhimu, muhimu uwapelekee ng'ombe wao tu.
Vyote vina umuhimu maana vinatumia vyote.
Kuna wakati unaambiwa utalipa ng'ombe 5 wa miguu(kwa maana ya walio hai) na ng'ombe 15 (in term of money)

Hii inatumika maana si kila mtu maeneo hayo ana ng'ombe, kwa hiyo anapewa unafuu wa kulipa kwa fedha. Wakisema wafanye kwa bei ya soko inaweza kuwa gharama kubwa zaidi.

Note: siwezi sema saana maana sijawahi uliza why ngombe hao huwa na thamani pungufu ukilinganisha na ya soko, but ndio nachoona kinafanyika

[/QUOTE] Au ukienda kununua ng'ombe ukisema ni kwa ajili ya mahari unauziwa kwa bei ya chini?[/QUOTE]
Ng'ombe wa kulipa mahari hanunuliwi, kama huna ng'ombe ndio unapewa option ya kulipa ng'ombe hao kwa kutoa pesa

Wenye nazo ng'ombe, ni baba wa binti anaitwa kuja zizini kujichagulia ng'ombe atakaye hadi idadi waliyokubaliana inapotimia. Na ni fahari kweli kwa mzazi wa binti akipokea ng'ombe na si pesa.

[/QUOTE]
*nipo katika kutafuta kuelewa kwa nini ng'ombe wa mahari tuambiwe ana thamani ndogo ya ng'ombe mwengine[/QUOTE]
Nadhani ndio 'utamaduni wa biashara' ya mahari kwa pande hizo, japo sina hakika
 
Sasa uwezo unao, tatizo ni nini?

Punguzeni ubahili. Princess wa Spain aliutoa mji mzima wa Bombay kwa Mfalme wa Uingereza kama mahari, itakuwa milioni nne hata gari hununui!

wee GAJIN au SACHOO?? watu hapenda mteremko bure kabisa wako tayri kunana SAPPORO 10.000.000/kwa mwaka lakini kununua jiko muuu!!!!!kazi kidogo pole
 
Wana Jamii Forum naomba kuwasilisha hapa mbele ya jukwaa hili
Nina mpenzi wangu kamaliza chuo now nataka nioe kabisa!! Tukiwa katika maongezi ya kawaida tu nikamdokezea
Hivi mahari yako ni kiasi gani mchumba wangu kaniambia millioni nne!!Kiukweli na mpenda sana lkn naona hio pesa nyingi japo uwezo wa kuitoa nianao Je Ndio mahari za siku hizi zilivo? Naomba ushauri wenu wana JF

Wanataka mtaji inawezekana biashara yao imeyumba, gangamala
 
Mwanamme anampa zawadi mwanamke kwa kukubali kuwa wake wa milele, kumzalia watoto na hata kuchukua jina lake wakati mwingi mwengine

Mtoto mnazaa wote na siyo mmoja wenu anamzalia mwenzake. Dhana ya kumzalia mwanaume mtoto inaendeleza yale yale ya mfumo dume.

Hakuna suala la utumwa hapo, mbona mwanamke anabadili jina na kuwa la mwanamme na hawi mtumwa wake?

Watumwa wa Marekani walibadishiwa majina yao na kupewa majina ya wamiliki wao. Binafsi sioni ubaya wa mwanamke aliyeko kwenye ndoa kubakiza jina la ukoo wake.
 
Mtoto mnazaa wote na siyo mmoja wenu anamzalia mwenzake. Dhana ya kumzalia mwanaume mtoto inaendeleza yale yale ya mfumo dume.

Mimi nazaa mtoto ila yeye namzalia, hivyo sote kuwa na huyo mtoto wetu kwa pamoja. Kukubali kubeba mbegu zake, tukachanganya vinasaba tukatoa mtoto, tayari mwanamke anafaa kupewa zawadi 😛oa

Watumwa wa Marekani walibadishiwa majina yao na kupewa majina ya wamiliki wao. Binafsi sioni ubaya wa mwanamke aliyeko kwenye ndoa kubakiza jina la ukoo wake.

Ndio hapo nilipokusudia mie, kuwa watumwa walikuwa wakibadilishwa majina ya kuwa ya wamiliki wao lakini wanawake wanaobadilishwa majina kuwa ya waume zao mbona hatuwaoni kuwa watumwa? Kama hatuwaoni basi na mwanamke kulipiwa mahari hakulazimishi kuwa ndio kanunuliwa na hivyo kuwa mtumwa

Nakubaliana na wewe kuwa hakuna ubaya kwa mwanamke kubakiza jina la ukoo wake kabla ya kuolewa. Akijitambulisha akasema ni mke wa Fulani ila yeye binafsi ni kutoka Ukoo Kadha
 
Mimi nazaa mtoto ila yeye namzalia, hivyo sote kuwa na huyo mtoto wetu kwa pamoja. Kukubali kubeba mbegu zake, tukachanganya vinasaba tukatoa mtoto, tayari mwanamke anafaa kupewa zawadi 😛oa

Bado sikubali kuwa unamzalia. Ni unazaa mtoto wenu. Ukisema unamzalia inakuwa kama vile huyo mtoto si wako bali ni wake peke yake.

Ndio hapo nilipokusudia mie, kuwa watumwa walikuwa wakibadilishwa majina ya kuwa ya wamiliki wao lakini wanawake wanaobadilishwa majina kuwa ya waume zao mbona hatuwaoni kuwa watumwa?

Utumwa una sura nyingi. Wanawake kubadilisha majina yao na kuchukua ya waume zao inakaribiana na utumwa.

Kama hatuwaoni basi na mwanamke kulipiwa mahari hakulazimishi kuwa ndio kanunuliwa na hivyo kuwa mtumwa

Kulipiwa mahari ni kuendeleza dhana ya mwanamke kuwa object. Mahari ina objectify wanawake na ina-run counter na juhudi za kuleta usawa na wanaume.
 
Bado sikubali kuwa unamzalia. Ni unazaa mtoto wenu. Ukisema unamzalia inakuwa kama vile huyo mtoto si wako bali ni wake peke yake.
Sarufi uwanja mpana. [Kumchekea] haina maana kuwa wewe mwenyewe hucheki, unacheka kwa niaba yake au badala yake. Hivyo hivyo kwa [kumchezea]. Haina maana kuwa wewe huchezi, ni kuwa unacheza na unajichezesha mbele yake. Kwa hiyo kumzalia haina maana kuwa wewe mwenyewe huna chako. Unazaa kwa ajili yako na yake.

Utumwa una sura nyingi. Wanawake kubadilisha majina yao na kuchukua ya waume zao inakaribiana na utumwa.

Inaweza ikawa si utumwa lakini kuna kupoteza identity. Si jambo linalonipendeza.
Kulipiwa mahari ni kuendeleza dhana ya mwanamke kuwa object. Mahari ina objectify wanawake na ina-run counter na juhudi za kuleta usawa na wanaume

Hapa nadhani suala ni unalipa kwa nani? Kama baba wa mtoto na mume mnabadilishana mtoto kwa mahari, inaweza kuwa na mantiki hiyo uliyotaja. Lakini ikiwa ni binti mwenyewe ndie anaepanga mahari, na ndie anaekabidhiwa hicho alichopewa kama tunzo au tunu kutoka kwa mume wake mtarajiwa, sioni ila hapo.

Ni njia moja wapo ya kuonyesha mapenzi tu. Pata picha mwanamke kadai atungiwe shairi, linaletwa linasoma....how romantic is that?! :redfaces:

Tukumbuke kuwa mahari si lazima yawe mali.
 
Sarufi uwanja mpana. [Kumchekea] haina maana kuwa wewe mwenyewe hucheki, unacheka kwa niaba yake au badala yake. Hivyo hivyo kwa [kumchezea]. Haina maana kuwa wewe huchezi, ni kuwa unacheza na unajichezesha mbele yake. Kwa hiyo kumzalia haina maana kuwa wewe mwenyewe huna chako. Unazaa kwa ajili yako na yake.

Inaweza ikawa si utumwa lakini kuna kupoteza identity. Si jambo linalonipendeza.

Hapa nadhani suala ni unalipa kwa nani? Kama baba wa mtoto na mume mnabadilishana mtoto kwa mahari, inaweza kuwa na mantiki hiyo uliyotaja. Lakini ikiwa ni binti mwenyewe ndie anaepanga mahari, na ndie anaekabidhiwa hicho alichopewa kama tunzo au tunu kutoka kwa mume wake mtarajiwa, sioni ila hapo.

Ni njia moja wapo ya kuonyesha mapenzi tu. Pata picha mwanamke kadai atungiwe shairi, linaletwa linasoma....how romantic is that?! :redfaces:

Tukumbuke kuwa mahari si lazima yawe mali.
Mwalimu Gaijin upo
 
Last edited by a moderator:
Bado sikubali kuwa unamzalia. Ni unazaa mtoto wenu. Ukisema unamzalia inakuwa kama vile huyo mtoto si wako bali ni wake peke yake.

Utumwa una sura nyingi. Wanawake kubadilisha majina yao na kuchukua ya waume zao inakaribiana na utumwa.

Kulipiwa mahari ni kuendeleza dhana ya mwanamke kuwa object. Mahari ina objectify wanawake na ina-run counter na juhudi za kuleta usawa na wanaume.
Loud and Clear Nyani Ngabu
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom