SoC02 Mahari isiwe kikwazo, mtoto wa kike sio bidhaa

Stories of Change - 2022 Competition

Ralph Wapps

Member
Joined
Sep 14, 2015
Posts
18
Reaction score
41
Katika maisha tujifunze kuwa watu wa mabadiliko na sio watu wa kukomaa na misimamo isiyo na tija kwakuwa misimamo ya namna hii huwa inagharimu sana

Kuna mzee mmoja ana mabinti watano hakubahatika kupata kijana wa kiume sasa kama unavyojua maisha ikatokea siku ya siku binti yake mmoja akaja kuchumbiwa pale nyumbani kama ilivyo ada ya mila zetu za kiafrika alitumwa mshenga na barua ya posa kuja kuchumbia wazazi wakaipokea vizuri. Babaye wa kijana ikabidi siku aende kumtolea mahari kijana wake akapokewa vizuri kabisa. Katika mazungumzo wazazi wa binti wakafikia kuwa wanataka mahari itoke jumla Milioni 4 hapo ndo mvutano ukaanza mzee ana milioni 3 katika kuongea ongea pale ghafla yule mzee aliekuwa analeta mahari akaanguka kutokana na jazba akapata mshtuko presha ikapanda kumuwahisha hospitali wakaambiwa ameshafariki.

Sasa badala ya kuwaza ndoa ghafla ikaanza mipango ya msiba. Kila mtu aliesimuliwa ule mkasa alichukizwa na kushangazwa ni kwa muda mfupi kiasi gani tamu inaweza geuka chungu, furaha inaweza ikageuka huzuni.

Basi kila mtu akaogopa kwenda kuchumbia mabinti wa yule familia ile kutokana na yalyotokea mwishowe mabinti wake waliishia kutoroshwa na wanaume na kutokomea kusipojulikana na hata hawakutaka mawasiliano na nyumbani kwao

Ukiangalia sababu kubwa ya yule familia ile kudai milion 4 ni kisa jirani yao aliozesha binti kwa milion tatu kwahiyo alitaka amfunike tu. Tazama bint anavyotumika kama bidhaa

Wito wangu ifike mahala haya masuala ya wazazi kupanga mahari yapigwe marufuku kama mzazi usitegemee kupata malipo kwa kumlea bint yako pindi anapoolewa basi ukaanza kumtwisha kijana anaeanza kutafuta maisha gharama asizoziweza. Mahari iwe tu kma ishara ya kuridhia pokea chochote utacholetewa na Mungu atakubariki
 
Upvote 8
Mahari ni mila ya kipuuzi tuliyotakiwa kuachana nayo miaka mingi iliyopita.
 
Nimekupigia kula kabisa, hii imenitoke mimi hapa ninayecomment kwenye uzi wako, baada ya kuona hivyo ile hera nilienda kununua kiwanja na sasa najiandaa kujenga kama nipatapa pesa za kujenga, na sito kuja nitoe posa kabla sijaishi na binti kwenye ndoa, na nimepanga kutorosha,
ilimradi nina kwangu hata kama ni pagara nitaishi
 
Sizan km unahaki ya kuingulia maamuzi ya familia ingne ukitaka mahali ya nafuu zaa wako umuozeshe ata kwa Mche wa sabuni ila mtoto wa mwingne wacha waamue wenyewe na km ukishindwa ww wengne wapo watalipa iyo pesa
Aisee[emoji1787][emoji23][emoji1787][emoji23]
 
Mwanaume maskini hatakiwi kuoa anatakiwa kuwa padri au Bruda wa kanisa katoliki

Mahali ni kipimo.cha kupima kama aweza kutunza mkewe

Kama magari hawezi mtoto wa kike ni sawa na kumtupa porini afe njaa

Wazazi msikubali huo ujinga
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Back
Top Bottom