Mahari kubwa yamkosesha mke

Mahari kubwa yamkosesha mke

Acha bwana aliacha laki tano yake siku hiyo kuna watu wanna imani dunia hii yani kweli mim niache hela yangu nyuma..
 
Ni kijana mwenzangu sekta ya afya, mwaka huu mwanzoni aliamua kwenda kutoa posa kwa binti ambaye alipanga aanzishe naye familia.

Binti mwajiriwa wa serikali na asili yao ni kanda ya ziwa ila wanaishi na familia katika moja mikoa wa Pwani.

Mshenga alitumwa pamoja na baadhi ya wanafamilia wa kijana.

Kijana aliaandaa milioni 2 mfukoni siku hiyo ambayo alishika mjomba wake .
Kusikilizwa laki 2 , kishika uchumba laki 3 , wakatoa cash.

Mahari ikatajwa ng'ombe 10 @400,000/- jumla mil 4 na vitu vingine milioni 1, jumla ya mahari milioni 5 itolewe yote kwa pamoja bila kuacha deni.

Mshenga akabembeleza pale ila wapi. Wakajibiwa kwa mila za kwao kupunguza mahari ni dharau , hilo Jambo haliwezekani.

Basi ule msafara wake ukarudi bila muafaka.

Kabla ya hapo Kijana alipanga na mchumba wake kuwa mahari itakuwa milioni 2.5 so yeye alijua akitoa milioni 2 akibakisha deni la laki 5, kama tunavyooambiana mtaani mahari haimaliziwi.

Kijana akamtafuta yule binti akamuuliza vp mbona mambo yameenda ndivyo sivyo, alipanga 2.5 wametajiwa 5.

Binti akamjibu kuwa yeye yupo na ndugu zake lazima mila ifuatwe.

Kijana akasema sawa ngoja nikajipange tena nitarudi nikikamilisha.

Ila septemba hii jamaa ananimbia anafikiria kughairi lile swala lake.

Mimi nikamwambia hakikisha ili lak 5 yako unarudishiwa [emoji23][emoji23][emoji23] .
Wamezinguana......
 
Kwetu mahari ni kubwa lakini huwa kuna kujitetea na kumalizia badae,mfano 5 au 6 M unaweza kumaliza mbele ya safari tena kama mkeo ni mwajiriwa msaidizane kulipa hiyo mahari
Hao kwakweli hawatumii akili,vijana wenyewe walivyochoka na maisha nani amlipia hiyo 5M kwa mkupuo?

Sent from my HUAWEI MLA-AL10 using JamiiForums mobile app
 
Zamani vitu vilikuwa natural, bikra low body counts wazee wetu walioa kwa gharama ya kawaida. Ila siku hizi bikra hadimu, high body counts anazijua rungu za aina zote, anazijua style zote ila mahali bei ya kiwanja Kibaha.

Kwanza huyo mzee anabahati kupata mkwe ambaye yupo tayari kutoa, mahali kabla ya kumpa mimba. Huku mitaa tuliyo toka, watu wanatia mimba,mahali hawatoi na wanakaa mtaa mmoja na wakwe kila siku wanamuona kidume kilichompa mimba binti yao. Wanakomaa weee,baadae wanaongea na binti, amletee mzazi mwenzie japo ajitambulishe, ili amuoe binti yao kwa mahali ya kitonga au sometimes free kabisa,ili awaondolee aibu.
 
Ni kijana mwenzangu sekta ya afya, mwaka huu mwanzoni aliamua kwenda kutoa posa kwa binti ambaye alipanga aanzishe naye familia.

Binti mwajiriwa wa serikali na asili yao ni kanda ya ziwa ila wanaishi na familia katika moja mikoa wa Pwani.

Mshenga alitumwa pamoja na baadhi ya wanafamilia wa kijana.

Kijana aliaandaa milioni 2 mfukoni siku hiyo ambayo alishika mjomba wake .
Kusikilizwa laki 2 , kishika uchumba laki 3 , wakatoa cash.

Mahari ikatajwa ng'ombe 10 @400,000/- jumla mil 4 na vitu vingine milioni 1, jumla ya mahari milioni 5 itolewe yote kwa pamoja bila kuacha deni.

Mshenga akabembeleza pale ila wapi. Wakajibiwa kwa mila za kwao kupunguza mahari ni dharau , hilo Jambo haliwezekani.

Basi ule msafara wake ukarudi bila muafaka.

Kabla ya hapo Kijana alipanga na mchumba wake kuwa mahari itakuwa milioni 2.5 so yeye alijua akitoa milioni 2 akibakisha deni la laki 5, kama tunavyooambiana mtaani mahari haimaliziwi.

Kijana akamtafuta yule binti akamuuliza vp mbona mambo yameenda ndivyo sivyo, alipanga 2.5 wametajiwa 5.

Binti akamjibu kuwa yeye yupo na ndugu zake lazima mila ifuatwe.

Kijana akasema sawa ngoja nikajipange tena nitarudi nikikamilisha.

Ila septemba hii jamaa ananimbia anafikiria kughairi lile swala lake.

Mimi nikamwambia hakikisha ili lak 5 yako unarudishiwa [emoji23][emoji23][emoji23] .
Piga chini huyo Binti, mtashindwana.
 
Back
Top Bottom