Mahari kwa Wakristo Afrika ni utamaduni wa kimila au wa dini?

Mahari kwa Wakristo Afrika ni utamaduni wa kimila au wa dini?

Yoda

JF-Expert Member
Joined
Jul 22, 2018
Posts
48,475
Reaction score
70,102
Jamii za Wakristo za Afrika mahari ni jambo la msingi sana kwao katika mchakato wa kuoa. Mwanaume lazima alipe mahari kwa familia ya mwanamke anapotaka kuoa, mahari yenyewe huwa ni kubwa tu.

Huko magharibi, hasa Marekani, Canada na Ulaya katika jamii za Wakristo hakuna suala la kulipa mahari katika ndoa.

Huu utofauti unamaanisha mahari ni mila za makabila tu, utamaduni nje ya dini Kikristo au Wamagharibi tu waliamua kuupuza na kuupotezea huu utaratibu?

Vipi huko India, Wakristo wanaume wanalipiwa mahari na familia ya mwanamke kama ulivyo utamaduni kwa jamii kubwa ya Wahindi?
 
Kwenye suala la usawa wa kijinsia inabidi wanaume wasilipe kitu sababu mwanaume na mwanamke ni sawa!!
Au kama mwanaume akitajiwa mahari ukweni basi na mwanamke nae anatakiwa atajiwe mahali na yeye alipe.

Kwahyo wazungu wamefanikiwa kuleta usawa wa kijinsi
 
Ukristo hauna sheria ya mahari iweje ama apewe nani ?

Bali ni mila ama traditional za muolewaji ndizo zinaongoza utaratibu wa mahari

Ndio maana mkristo mpare analipiwa mahari kwa utaratibu ulio tofauti na mkristo mkurya ama mkristo mhaya

Kabila la binti ndilo linatoa mwongozo na utaratibu wa mahari ya huyo binti, gharama haziletwi na ukristo
 
Sasa kwa nini unakuta suala la mahari kwa Wakristo wanaotoka hizi jamii linakuwa kubwa na tofauti sana na Waislamu wanaotoka jamii hizo hizo?!
Ukristo hauna sheria ya mahari iweje ama apewe nani ?

Bali ni mila ama traditional za muolewaji ndizo zinaongoza utaratibu wa mahari

Ndio maana mkristo mpare analipiwa mahari kwa utaratibu ulio tofauti na mkristo mkurya ama mkristo mhaya
 
Sasa kwa nini unakuta suala la mahari kwa Wakristo wanaotoka hizi jamii linakuwa kubwa na tofauti sana na Waislamu wanaotoka jamii hizo hizo?!
Labda sababu kwa waislamu kuna option ya kuachana ( Talaka ) lakini kwa christians option hiyo hamna kwa ni kama unauza bidhaa jumla jumla
 
Sasa kwa nini unakuta suala la mahari kwa Wakristo wanaotoka hizi jamii linakuwa kubwa na tofauti sana na Waislamu wanaotoka jamii hizo hizo?!

Waislamu wanafata mwongozo wa dini yao. Hawafati utamaduni wa kabila zao. Maana wao wanaamini wao ni sehemu ya muslim ummah hivyo lazima wafate utamaduni wa mtume.. ama kwa lugha nyingine wanafata sunnah za mtume.

Mfano mmasai wa kike akiwa muislamu anakatazwa kuvaa mashuka na kulazimishwa avae Hijab , niqab, burka.

Huku mmasai wa kike akiwa mkristo ataendelea kuvaa mashuka yake bila kuulizwa na mtu yeyote maana ukristo unatambua utamaduni haufanani kwa wote.

Kwenye tamaduni za makabila yote za asili mahari inapokelewa na jamii nzima ya mwanamke. Ndio maana unakuta jembe la babu, blanket la bibi, pombe ya ukoo,

Ila kwenye uislamu wanaiga utamaduni wa mtume ambapo mahari anapokea mwanamke mwenyewe muolewaji.. na pombe ni haram hata kama kabila lake lina utamaduni wa pombe toka enzi na enzi
 
Waislamu wanafata mwongozo wa dini yao. Hawafati utamaduni wa kabila zao. Maana wao wanaamini wao ni sehemu ya muslim ummah hivyo lazima wafate utamaduni wa mtume.. ama kwa lugha nyingine wanafata sunnah za mtume...

You nailed it...!

🙏🏾
 
Sasa kwa nini unakuta suala la mahari kwa Wakristo wanaotoka hizi jamii linakuwa kubwa na tofauti sana na Waislamu wanaotoka jamii hizo hizo?!
Kwa wakristo wengi bado suala la mahari wanalipeleka kimila yaani huona kama chanzo cha mapato ndio maana hutaka dau kubwa ila waislamu wanalipeleka kidini.
 
Jamii za Wakristo za Africa mahari ni jambo la msingi sana kwao katika mchakato wa kuoa. Mwanaume lazima alipe mahari kwa familia ya mwanamke anapotaka kuoa, mahari yenyewe huwa ni kubwa tu...
Suala la mwanaume kumlipia mahali mwanaume ni kwa mujibu wa sheria za dini ya kihindu, wakristo wenye asili ya kihindi hawana utaratibu huo.
 
Kwa wakristo wengi bado suala la mahari wanalipeleka kimila yaani huona kama chanzo cha mapato ndio maana hutaka dau kubwa ila waislamu wanalipeleka kidini.
Wana maisha yao nje ya Ukristo, hicho ndicho watu huwa wanadhani ndiyo Ukristo
 
Hamna watu wasumbufu kwenye suala la ndoa kama wakristo kuna jamaa alikuwa anataka kuoa sasa alipita ofisini kwetu hatujuani wala hatujawahi kuonana hta siku moja ila ilikuwa kila baada ya mda anapita kuulizia mchango wa harusi ikabidi tumpe maana ilikuwa usumbufu tu tokea siku hayo hata ukikutana nae barabarani hana time na ww hata Salam hakupi kiufupi wakristo ni wasumbufu kwenye ndoa wanalazimisha vitu vilivyo nje ya uwezo wao.
 
Tamaa tu za wazazi.

Mi mahali nilitoa ndogo sana
 
Back
Top Bottom