Mahindi bei yaanza kupanda!

Tatizo mahindi yako na walanguzi hivi sasa. Mkulima hana hata punje. Wakulima daima, hutumia mazao yao kwa kila kitu. Kuugua, kusomesha, kula, na starehe nyingine. Kutumia mazao ili kujipatia mahitaji sio tatizo. Tatizo huja pale BEI,inapokuwa ndogo halafu still, wanauza kujikimu. Wanauza hadi ya kula wao wenyewe. Na asikuambie mtu wakulima wana njaa. Hawana mahindi, walishauza. 'Mamidomani' ndio wenye mahindi kwa sasa na ikitokea yanapanda mkulima hana chake. Nimetembelea vijiji vya mkoa wa Ruvuma vinavyozalisha mahindi kwa wingi na nimejionea hili. Fedha ya mbolea hawana. Hivyo uzalishaji sipati picha msimu ujao utakuwaje. Sijafahamu kuhusu huko sumbawanga, lakini always , tabia na hali za wakulima wetu(mimi nikiwemo) hufanana.
 
Vipo songea Bei ya mahindi imekaaje nataka niongeze hekari za mahindi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…