Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Sumbawanga gunia sh 35,000-40,000. Subira yavuta kheri. Dar imefika bei gani?
tumesikia, asa mapema yote hii ulikuwa unawahi nini 4.13 AM.au ndo mambo ya sumbawangaSumbawanga gunia sh 35,000-40,000. Subira yavuta kheri. Dar imefika bei gani?
Vipo songea Bei ya mahindi imekaaje nataka niongeze hekari za mahindiTatizo mahindi yako na walanguzi hivi sasa. Mkulima hana hata punje. Wakulima daima, hutumia mazao yao kwa kila kitu. Kuugua, kusomesha, kula, na starehe nyingine. Kutumia mazao ili kujipatia mahitaji sio tatizo. Tatizo huja pale BEI,inapokuwa ndogo halafu still, wanauza kujikimu. Wanauza hadi ya kula wao wenyewe. Na asikuambie mtu wakulima wana njaa. Hawana mahindi, walishauza. 'Mamidomani' ndio wenye mahindi kwa sasa na ikitokea yanapanda mkulima hana chake. Nimetembelea vijiji vya mkoa wa Ruvuma vinavyozalisha mahindi kwa wingi na nimejionea hili. Fedha ya mbolea hawana. Hivyo uzalishaji sipati picha msimu ujao utakuwaje. Sijafahamu kuhusu huko sumbawanga, lakini always , tabia na hali za wakulima wetu(mimi nikiwemo) hufanana.