Mahindi tani 260 kutoka Tanzania yakwama mpaka wa Holili upande wa Kenya

Mahindi tani 260 kutoka Tanzania yakwama mpaka wa Holili upande wa Kenya

johnthebaptist

JF-Expert Member
Joined
May 27, 2014
Posts
97,869
Reaction score
171,716
Takribani tani 260 za mahindi kutoka Tanzania yamekwama katika mpaka wa Holili upande wa Kenya yakihofiwa kuwa na sumu kuvu

Meneja wa TRA kituo cha Holili amesema mahindi hayo yamepimwa upande wa Tanzania na kuonekana ni salama kwa chakuka lakini yapofika Kenya yalizuiwa na kuchukuliwa sampuli kupelekwa kwa mkemia mkuu wa serikali yao kwa uhakiki.

Chanzo: ITV habari

Pia soma >
RC Shigella: Hakuna mahindi yaliyozuiwa kuingia Kenya kupitia mpaka wa Horohoro, Jana na leo tumevusha tani 570

Maendeleo hayana vyama!
 
Wewe Jana si ulifungua Uzi ukisema shigella kakwambia mahindi hayajazuiliwa wamepitisha tani 570, mbona sikuelewi tena kwa Uzi huu. Very contradictory bwashee
Holili siyo Holoholo bwashee!

Holili RC ni mama Mghwira!
 
Corona, Nzige, mahindi kukwama mipakani. Ninashauri tena na tena Prof Adolf Mkenda waziri wa Kilimo maliza hii jam ya mahindi kukwama mipakani. Sasa hili ni Rombo na ni jimbo lako.kazi kwako
Hivi Tanzania kuna waziri wa biashara?!
 
Nimefurahi kusikia " yalipimwa Tanzania yakaonekana yapo salama"

Na hii si kweli!! Sijui uongo unasaidia nini!! EAC customs zina model ya OBP (one border post) so mambo yote ya customs yanafanywa na upande amabzo bidhaa zinaingia. Na kawaida mwenye dhamani na quality assurance ni anayefanya importation! Tanzania haiwezi kupima mahindi yaliyo katika magari yaliyo upande wa Kenya!!
 
Kwani kuna ugumu gani kuelewa.

Malori si yanatokea Tanzania.

Hapo mpakani maofisa wa Tanzania hawapo, hawawezi kuchukua sampuli za mzigo kabla haujavuka na kupima?

Hata kama sio hao maofisa wa hapo mpakani kupima, kwani kuna zuio gani kwa Tanzania kupima kabla ya kusafirisha mzigo ili kuwa na uhakika na ubora wa bidhaa hiyo. Hii inaweza kufanyika mbali na mpaka huo kwenye hiyo OBP, la ajabu hapo ni lipi?

Malori yakishavuka, hao Kenya wanapima/wanachukua sampuli, wakati malori yamesimama hapo mpakani. Baada ya majibu yanazuiwa kuendelea na safari; shida ya uongo ipo wapi hapo!

Ngoja nikuulize. Kenya hawawezi kusema uongo kuhusu vipimo vyao?
 
Back
Top Bottom