Mahindi yangu nitauza wapi

Nimefurahi sana kuona jinsi watu wanaingia kwenye kilimo
Kilimo kina changamoto sana na moja ni kama unazozipata kwa sasa..Kwa ushauri wangu ni kwamba kwa sababu huna store ya kuhifandhi hayo mahindi ni bora uyauze yakiwa mabichi kwa ajili ya kuchoma na ukizingatia yatakupatia faida kubwa tofatuti kabisa na hata ukija kusaga na kuuza. Jaribu kwenda kwenye masoko kama kariakoo, Mabibo na tandika ukafaye utafiti mahindi mabichi ni bei gani, najua sio chini ya sh 350 - 400 kwa moja, halafu tafuta mtaji kidogo tu wa kukodisha gari ukayauze mwenyewe sokoni, epuka sana kutumia madalali kwani watakunyonya kama kupe watanunua mahindi kwa jumla 150 - 200 kwa kila moja na utashangaa wanayauza kwa 350-400 kwa kila moja
Kila la kheri.
 

Mkuu kwa dar soko la nafaka bila dalali utaumia, jamaa wameteka soko na wao ndo wanaompangia tajiri(mnunuzi) akikiuka basi hatapata mzigo siku nyingine.
Pia kwa muda huu mahindi mabichi sio dili tena, kwani kila kona mahindi yameshakomaa.
 
Mkuu maundumula awamu hii mahindi ni mengi sana kila mtu atapata, hivyo soko lake halitakuwa zuri.
Nakushauri msimu wa mavuno ukifika uza nusu ya utakachopata.
Tukisie utapata gunia 800, ukiuza kwa sh40k kwa magunia 400 utapata sh M16.
Then nunua mashine ya kusaga na kukoboa uanze ufugaji wa nguruwe (kama imani yako inaruhusu), tumia nusu ya stock(gunia 400) kulisha nguruwe na hela kidogo kwajili ya huduma mbalimbali.
Anza na nguruwe 20 majike waliopandwa. Baada ya miezi tisa utakuwa na wastani wa chini nguruwe 200 wenye wastani wa kg60 kila mmoja.
Ukiwauza kwa bei ya jumla ni SH6000/= kwa kg1. Hivyo 6000*200*60= TSHS 72,000,000/=
Fanya hivyo mkuu utafurahia kilimo na pengine usitamani tena kuwa mtumwa.
 

Wenye mifugo tutanunua tu haina shida, najindaa kununua ya kutosha,
 
Hongera kaka kwa kilimo.
Changamoto zipo kaka.

1. Kuuza mabichi itakuwa ngumu kwa sasa. soko la tandale wanauza 150-200 kwa mhindi tena yale marefu ya Iringa/Songea. Mahindi yanayolimwa kanda hii ya pwani ni mafupi,hayapo attractive sana kwa wachuuzi. Lakini nenda huko sokoni ukaone soko halisi!

2. Bei ya mahindi yaliyovunwa msimu huu ni tshs460-470 kwa kg hapo tandale wakati yale ya msimu uliopita ni 520-525. Sio ngumu kupata dalali atakaeweza kukusaidia. Je unajua utavuna ln?

3. Hiyo idadi sio kubwa sana. Gunia unalozungumzia ni la kg ngapi? Huwezi kuepuka storage completely. Kuna muda wa kupukuchua unless kama una machine ya kupukuchua. Kama alivyoshauri mchangiaji mmoja hapa ni vema ungeenda hapo mapinga kwenye kiwanga cha kutengeneza chakula cha kuku bei zao nadhani ni tshs 400-450/kg . Pesa utakayopata itakusaidia kutengeneza storage facility . Kama unalima mahindi ,changanya na alizeti. Halafu fuga nguruwe kama bwan mmoja alivyoshauri hapa. Idea ni kuuza kiasi kupata mtaji. Binafsi nalima na kufuga. Mahindi na alizeti sehemu inaenda kwenye mifugo

3.Waweza pia uza hapohapo shambani.Mm kwangu huwa wanananua hapohapo shambani kwa 50-60k/gunia. Ukiwa tayari nitaarifu nitakutafutia hao jamaa.
 

Mkuu kwa kiti moto tatizo imani hairuhusu ila ushauri wako mzuri kama uta apply kwa mifugo mingine pia.
 

Nitakutafuta wakati ukifika matumaini yangu ni kwamba watakuwa bado wanahitaji wakati ukifika.
 
Nipigie kwa namba hizi 0715405027 tuongee mi huwa nanunua mahindi . mi
 
Uza mapema iwezekanavyo, tatizo kutunza stoke ya mahindi ni changamotokubwa maake utapaswa kuyapiga dawa kila baada ya muda ukijisahau kidogo tu, yanabunguliwa na wadudu
 
Mkuu kwa kiti moto tatizo imani hairuhusu ila ushauri wako mzuri kama uta apply kwa mifugo mingine pia.

Haina shaka mkuu unaweza pia ukajikita kwenye ufugaji wa kuku na jamii nyingine ya mifugo kwani lengo kuu ni kufanya kilimo na ufugaji ndipo utaweza kuinuka haraka na masrahi utakayopata hakika yatakushawishi uzamie mazima ktk shughuri hii.
 
Mahindi yapo mengi sana msimu huu ila Weka number yako naweza kuchukua mzigo wote, 0714 522424 tuwasiliane
 
nikikupa 30 million kwa mzigo wote huo upo tayari tufanye biashara
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…