Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 5,383
- 18,776
Mwenyekiti wa BAVICHA Taifa, Deogratias Mahinyila amemjibu Msemaji wa Timu za Taifa Tanzania, Haji Manara, akisema Wanasiasa wana haki ya kutoa maoni yao kuhusu masuala yanayohusu taifa, ikiwemo maandalizi ya Michuano ya Mataifa ya Afrika (AFCON).
Mahinyila ametoa kauli hiyo leo, Julai 31, 2026, akizungumza na Waandishi wa habari ikiwa ni siku moja baada ya Manara kuwataka wanasiasa kutoizungumza vibaya Tanzania kuhusu maandalizi ya AFCON 2027, ambayo yataandaliwa kwa ushirikiano wa Tanzania, Kenya na Uganda.
Soma: Manara amuonya Heche, asema kama hamuwezi kuiongelea vizuri AFCON, kaeni kimya
Alisema kauli ya kuwataka Wanasiasa kukaa kimya haina msingi, akisisitiza kuwa hakuna mwenye mamlaka ya kuwanyima nafasi ya kutoa maoni kuhusu masuala ya kitaifa.
Mahinyila aliongeza kuwa kauli za aina hiyo zinaweza kutafsiriwa vibaya na kuibua maswali kutoka kwa taasisi za soka za kimataifa kama CAF na FIFA kuhusu hali ya uhuru wa kujieleza nchini.
Aidha, alieleza kuwa kuhusisha Vijana na tuhuma za ugaidi au kuwanyamazisha wanaotoa maoni kunaweza kuwa na athari kwa taswira ya taifa na kunahitaji kushughulikiwa kwa umakini.
Kauli za viongozi hao zinakuja baada ya Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA Bara, John Heche, kusema Chama hicho kina mpango wa kuandika barua kwa CAF na FIFA kueleza wasiwasi wake kuhusu hali ya usalama nchini kuelekea michuano ya AFCON 2027.