Mahitaji haya ya waya kwa ajili ya wiring ni sahihi?

Mahitaji haya ya waya kwa ajili ya wiring ni sahihi?

Udochi

JF-Expert Member
Joined
Jul 25, 2015
Posts
787
Reaction score
1,056
Waheshimiwa, baada ya kukamilisha hatua ya kuchimbia bomba ukutani,
Sasa Fundi umeme amenipa mahitaji ya wiring kama ionekanavyo hapa chini.

Kwa nyumba ya vyumba vitatu, sebule, dinning room na jiko,
Kiasi Cha wire wa milimita 1.5 = mita 250,
Na milimita 2.5 = mita 70,
Ni sahihi?

View attachment 2172402
 
Muda mwingine jiongeze mkuu. Fundi anayefanya kazi ndie anafahamu mpangilio wa nyumba yako. Sie tutaishia kupiga porojo tu. Kama humuamini hakikisha kunakuwa na usimamizi wa vifaa endapo kama unachohofia ni wizi. Vifaa vikibaki ni vyako.
 
Mbona makadirio yako chini sana?
Au Kuna vyumba vitaachwa?
 
muda mwingine jiongeze mkuu. Fundi anayefanya kazi ndie anafaham mpangilio wa nyumba yako . sie tutaishia kupiga porojo tu. kama humuamini hakikisha kunakuwa na usimamizi wa vifaa endapo kama unachohofia ni wizi . vifaa vikibaki ni vyako
Kwenye usimamizi nitakuwepo mkuu.
 
Waheshimiwa, baada ya kukamilisha hatua ya kuchimbia bomba ukutani,
Sasa Fundi umeme amenipa mahitaji ya wiring kama ionekanavyo hapa chini.

Kwa nyumba ya vyumba vitatu, sebule, dinning room na jiko,
Kiasi Cha wire wa milimita 1.5 = mita 250,
Na milimita 2.5 = mita 70,
Ni sahihi?
View attachment 2172402
Kasahau waya wa kutoa umeme Toka kwenye mita na wa jikoni fundi wako mdwanzi hata wa earth hajaweka.... mkumbushe aongeze usije kupata hasara kesho...
 
Hiyo itakuwa ni Banda la kuku na sio nyumba ya kuishi
 
Waheshimiwa, baada ya kukamilisha hatua ya kuchimbia bomba ukutani,
Sasa Fundi umeme amenipa mahitaji ya wiring kama ionekanavyo hapa chini.

Kwa nyumba ya vyumba vitatu, sebule, dinning room na jiko,
Kiasi Cha wire wa milimita 1.5 = mita 250,
Na milimita 2.5 = mita 70,
Ni sahihi?
View attachment 2172402
Kwenye 2.5 yuko sahihi ila hapo kwenye 1.5 wire utabaki kidogo
 
Jua unataka nini na nini kinatumia umeme kwako, kama vipi pima mwenyewe futi unayo, ila mafundi waya hupiga mahesabu ya kubakiza waya ili wauze
Lokaly estimation
Chukuwa futi
Pima kimo cha nyumba hdi ktk kenchi juu kabisa,*idadi ya vyumba, pima upana wa nyumba mara idadi ya vyumba, pima urefu wa nyumba mara idadi ya vyumba, jumlisha alafu zidisha kwa 2
 
Waheshimiwa, baada ya kukamilisha hatua ya kuchimbia bomba ukutani,
Sasa Fundi umeme amenipa mahitaji ya wiring kama ionekanavyo hapa chini.

Kwa nyumba ya vyumba vitatu, sebule, dinning room na jiko,
Kiasi Cha wire wa milimita 1.5 = mita 250,
Na milimita 2.5 = mita 70,
Ni sahihi?
View attachment 2172402
Mkuu wewe unaona kama umepigwa au?
 
Inategemea na raman yako ya umeme kama ni hizi za kisasa inawezekana kabisa raman yako ya nyumba ni kama yangu

Ilikula rola za kutosha

2.5 zimetembea sana rola 2
1.5 rola 2

Zilibaki kidogo sana ambavyo hata chumba hukamilishi Kusuka
 
Waheshimiwa, baada ya kukamilisha hatua ya kuchimbia bomba ukutani,
Sasa Fundi umeme amenipa mahitaji ya wiring kama ionekanavyo hapa chini.

Kwa nyumba ya vyumba vitatu, sebule, dinning room na jiko,
Kiasi Cha wire wa milimita 1.5 = mita 250,
Na milimita 2.5 = mita 70,
Ni sahihi?

View attachment 2172402
Bomba ziliingia ngapi?
 
Muamini fundi wako Mkuu hapa utadanganywa Sana cz nyumba zimetofautiana Sana mahitaji, mf nyumba za kisasa Zina MA shocas ambayo yanakuwa na taa za kutosha, Kuna ua la sebuleni Kuna mengine yanahitaji taa za kutosha so fundi na ww ndo mnajua mahitaji gani yapo kwny nyumb yako
 
Back
Top Bottom