Mahitaji haya ya waya kwa ajili ya wiring ni sahihi?

Mahitaji haya ya waya kwa ajili ya wiring ni sahihi?

Jua unataka nini na nini kinatumia umeme kwako, kama vipi pima mwenyewe futi unayo, ila mafundi waya hupiga mahesabu ya kubakiza waya ili wauze
Lokaly estimation
Chukuwa futi
Pima kimo cha nyumba hdi ktk kenchi juu kabisa,*idadi ya vyumba, pima upana wa nyumba mara idadi ya vyumba, pima urefu wa nyumba mara idadi ya vyumba, jumlisha alafu zidisha kwa 2
kukuelewa hapa kaz ipo
 
Waheshimiwa, baada ya kukamilisha hatua ya kuchimbia bomba ukutani,
Sasa Fundi umeme amenipa mahitaji ya wiring kama ionekanavyo hapa chini.

Kwa nyumba ya vyumba vitatu, sebule, dinning room na jiko,
Kiasi Cha wire wa milimita 1.5 = mita 250,
Na milimita 2.5 = mita 70,
Ni sahihi?

View attachment 2172402
Hapo kwenye mita mita 250 ni sawa na rola 2 na nusu yake,ila hapo kwenye waya wa 2.5 kwa mita 70 ni kama ndogo kwa vyumba vitatu.....ila inawezekana unataka tu kuingiza umeme kisha baadae ndio uje ufanye finishing ya mwisho
 
Duh nimefika stage hio, bajeti ya waya peke yake naona inagonga 700,000/-. Nahitaji waya
1.5 kijani roller mbili, nyekundu roller mbili na nyeusi roller mbili
2.5 kijani,neykundu na nyeusi roller moja moja
6 inahitajika mita 70.
Market price ikoje mtaani? Huku nilipo 1.5 africab 65,000 roller moja, 2.5 95,000 roller moja na 6 mita moja 4,500
 
Binafsi ni fundi wa umeme majengoni, kwa makadrio haya fundi amekadiria kidogo sana kulingana na vyumba ulivyotaja!

Lakini pia raha ya kazi ni kuaminiana ukiona una mashaka na mtu unayefanyanae kazi achana naye!!

Mimi sifanyagi kazi kabisa na mteja asiyeniamini au anayenishuku kijingajinga kama hivi!!

Mtu hata kazi yenyewe hamjaanza unaona jinsi anavyojistukia!!!
 
Jua unataka nini na nini kinatumia umeme kwako, kama vipi pima mwenyewe futi unayo, ila mafundi waya hupiga mahesabu ya kubakiza waya ili wauze
Lokaly estimation
Chukuwa futi
Pima kimo cha nyumba hdi ktk kenchi juu kabisa,*idadi ya vyumba, pima upana wa nyumba mara idadi ya vyumba, pima urefu wa nyumba mara idadi ya vyumba, jumlisha alafu zidisha kwa 2
hana haja ya kuzunguka na futi kama nyumba yake inaraman yenye vipimo ,kupitia raman tu utajua unahitaji waya kiasi gani
 
Muamini fundi wako, ushauri wa humu hatuwezi kuendana na uhalisia wa nyumba yako. Kikubwa kuwe na usimamizi wa karibu
 
Kwa ukubwa wa hiyo nyumba waya hautotosha haijalishi ramani ya nyumba yako...

Hapo zinahitajika roller 6 za 1.5mm ( 2pair za red 2,bluu2 , green 2) za ukubwa wa 100m kila roller 1

Roller 3 za 2.5mm (1pair)

Waya wa 6mm wa kuchukulia umeme

Waya wa earth wa 4mm
 
Back
Top Bottom