Mahitaji/malipo shule (sekondari) kwa mwaka wa masomo unaoanzia januari 2015

Mahitaji/malipo shule (sekondari) kwa mwaka wa masomo unaoanzia januari 2015

JituParaTupu

Member
Joined
Nov 20, 2008
Posts
92
Reaction score
9
Wadau, nauliza hivi bado kuna malipo kwa ajili ya watoto wetu wanaosoma shule za sekondari? Mtoto wangu ameniletea barua kutoka shule ikinitaka kulipia mahitaji kama nilivyoorodhesha hapa chini:-

1. Michango ta Walimu (PTT).............. Sh. 26,000/=
2. Ada ya shule..................................... Sh. 20,000/=
3. Mitihani ya kanda TAHOSSA........... Sh. 15,000/=
4. Ukarabati........................................... Sh. 15,000/=
5. Taaluma............................................. Sh. 10,000/=
6. Ulinzi.................................................... Sh. 5,000/=
7. Graduation/Mahafali....................... Sh. 5,000/=
8. Vifaa vya usafi................................... Sh. 4,000/=
9. Michezo.............................................. Sh. 2,000/=
JUMLA:................................................ Sh. 102,000/=

Nimekuwa nikisikia kauli mbali mbali za viongozi wetu wakisisitiza kutokuwepo na malipo katika shule za serikali.
Je, malipo haya ni halali? Nawasilisha.

 
Mwakan watafuta hiyo ada ya sh. 20'000 lkn michango mingine ni ya lazma na haikwepeki, maana ni utaratibu wa manispaa husika..serikali haiwez kupeleka shule mifagio, mafyekeo, dawa za choon, wala serikali haiwez kutoa pesa kwa ajili ya michezo, mahafar, mitihani midogo ya kujipima...
hivyo ada itayopungua kwa mwakani ile school fee yan (sh.20'000) tu
 
Back
Top Bottom