Mahojiano ya mwenyekiti wa bodi ya simba yabainisha hali ilivyo Simba

rodrick alexander

JF-Expert Member
Joined
Feb 12, 2012
Posts
18,360
Reaction score
26,244
🚨Magori anasema Barker alisema Uza.

Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya klabu ya Simba, Crescencius Magori, amefichua siri nzito ya jinsi klabu hiyo ilivyolazimika kufanya biashara ngumu ya kuwauza mastaa wao watatu, Jean Charles Ahoua, Kibu Denis, na Steven Mukwala, wakati wa dirisha dogo la mwezi Januari. Magori ameeleza kuwa uamuzi huo ulitokana na ukata wa kifedha uliokuwa unaikabili klabu hiyo kwa wakati huo, huku kukiwa na uhitaji mkubwa wa kuboresha kikosi ili kukidhi matakwa ya kiushindani.

Amesema kuwa baada ya bodi kuketi na Kocha Mkuu, Steven Barker, mwalimu huyo alisisitiza kuwa timu iliyopo haina uwezo wa kushindana na kubeba makombe, jambo lililowafanya waangalie ofa zilizokuwa mezani. Magori amebainisha kuwa kocha mwenyewe alibariki mauzo ya Ahoua, Kibu, na Mukwala kwa kutoa kauli fupi ya "Uza!", hatua iliyosaidia kupatikana kwa fedha za kianzio zilizotumika kusajili majembe mapya yaliyoingia kikosini hivi karibuni.

Kiongozi huyo amehitimisha kwa kusema kuwa usajili wa wachezaji walioingia kuchukua nafasi hizo ulifanyika kwa kufuata misingi ya kisayansi kupitia mfumo wa scouting (uchunguzi), ambapo takwimu zao zilichambuliwa na wataalamu watatu tofauti kabla ya kocha kupitisha ripoti yake. Amewatoa hofu mashabiki wa Simba kwa kueleza kuwa mbinu hiyo imesaidia kutengeneza timu imara, na maboresho zaidi yatatua mwezi Juni na Julai bajeti kuu ya usajili itakapofunguliwa.
Kutokana na maelezo yake zile tetesi kuwa tajiri aliwazimia simu zilikuwa kweli.
Baada ya timu kufanya vizuri tajiri anakuja na ahadi ya kutoa bilioni 1 wakitwaa ubingwa ili mradi timu ikifanya vizuri aimbwe yeye.
Haohao ndio walikuwa wanazuia wanachama wapya kuingizwa huku timu haina mapato, pia hawataki wawekezaji wengine waingie wakati aliyepo hawezi kusaidia timu.
 
Ulichoandika kinaonyesha ufinyu wako kwenye biashara....Tajiri atatoa vipi hela kuongeza wachezaji wengine wa kigeni wakati waliokwepo walishindwa kuonyesha ubora wao na timu nyingine zilikubali kuwanunua??
Kumbuka dirisha kubwa lililopita alitoa pesa za usajili,nani alikosea kufanya usajili?

MO ataendelea kuwa tajiri kwa jinsi anavyoheshimu pesa zake.
 
Watu wanakula sana pesa za MO pale Simba.
 
Uamuzi wa kuuza wachezaji furani kwenye dirisha dogo ili kuimarisha timu ulikuwa sahihi, lakini kama umemuelewa Magori anasema timu huwa inetenga bajeti bada msimu kumalizila.
Timu haina bajeti katikati ya msimu.
Hakuna tatizo hapo mkuu
 
Back
Top Bottom