Anaandika Mohonia Joseph
Mwenyekiti Mstaafu BAVICHA Mkoa wa Mara.
Wenyeviti wa CHADEMA wa Mikoa.
Makatibu wa CHADEMA wa Mikoa.
Wenyeviti wa CHADEMA wa Majimbo.
Makatibu wa CHADEMA wa Majimbo.
Wajumbe wawakilishi wa kutoka Wilayani kwenda Mkutano Mkuu Taifa.
Nimewaandikia ninyi kwakuwa najua kundi lenu ni kubwa kuliko kundi la Wapiga wote wa Mkutano Mkuu, hivyo mkiamua kwa umoja wenu mnaweza kufanya jambo.
Ninyi ni Watu ambao mnatokea kwa Wananchi na Wanachama wa CHADEMA katika maeneo yenu. Mnaishi na Wananchi na kushiriki nao katika shughuli za Kisiasa na za Kijamii za kila siku.
Ninyi hamlipwi wala hamna posho hata "mia mbovu" ya kujikimu wala hampokei hata "Senti moja ya ruzuku" kutoka kwenye Chama. Ninyi mnatumia fedha zenu binafsi za mfukoni kufanya shughuli za Chama hiki.
Ninyi Makao Makuu ya CHADEMA mnaenda kwa shughuli maalum labda ikitokea kuna Mkutano Mkuu au Baraza Kuu au mafunzo ya Chama. Kwahiyo ninyi sio wanufaika wa Makao Makuu, kwahiyo msijisahau mkaingia mkenge na Watu wa Makao Makuu ya Chama au wafuasi wao kwakuwa wengine pale wameajiriwa wanalipwa mshahara hivyo ni lazima wasimame upande wa Boss anayewalipa mshahara. Wala sio ajabu.
Na wengine ambao ni wapambe wanaishi kwenye nyumba za Vigogo wa Chama na hadi kufikia hatua ya kuwa "chawa". Wala msijali.
Ninyi mnaujua uhalisia wa Wanachama wenu na Wananchi kwa ujumla. Miongoni mwenu, mligombea Ubunge na Udiwani katika maeneo yenu. Mnatambua ugumu wa mazingira mnayopitia wakati wa kampeni. Mnatambua kuwa Chama hakijawahi kutoa fungu lolote kwa ajili ya kutoa support kwa Wagombea.
Kwa kifupi, "mnachakalika wenyewe" wenyewe.
Mnatambua na kukumbuka vilio vya akina Mama wanaojitolea kila leo kwenye Chama huku Majimboni mpaka Senti za mwisho, wengine ndoa zao zimevunjika kwa ajili ya kukipambania Chama hiki. Wengine wamepigwa na kuumizwa na Waume zao kwasababu tu ya kuwa CHADEMA wakati huo Waume zao wakiwa CCM.
Lakini pamoja na yote haya, mnafahamu linapokuja suala la Ubunge wa Viti Maalum wanaonufaika ni wengine kabisa tofauti na wale waliopambana na hiki Chama.
Mkapige kura ili kuondoa "Ubunge wa kudumu wa Viti Maalum kwa Watu fulani".
Kumbukeni haya mambo yote.
Pigeni kura mkijua mnawakilisha mamia na maelfu ya Wanachama ambao hawawezi kuongea ama kuandika namna hii wote kwa pamoja.
Nawaomba sana, kwa kuwa ninyi ni Wawakilishi wa Wanachama wa Misingi, Matawi, Kata, Wilaya na Mikoa mnayoongoza. Kabla hamjaenda kwenye Uchaguzi wa CHADEMA Taifa tarehe 21/01/2025 wasikilizeni Wanachama na Wananchi wa maeneo yenu mnayotoka.
Ingekuwa ni Serikalini, tungesena ninyi ni “Wabunge" katika maeneo yenu na hivyo mnaenda Bungeni kufanya maamuzi kwa niaba ya Wananchi waliowachagua.
Ikiwezekana waiteni Wanachama wenu kwenye Ofisi za Chama muwape nafasi ya kusikia maoni yao, kwamba wao wanataka muwachagulie nani kati ya Wagombea waliojitokeza. Msifanye maamuzi kwa utashi wenu binafsi.
Kumbuka mkienda mkamchagua mtu ambaye Wanachama hawamuhitaji mtapata wakati mgumu "mno" kufanya siasa Mwakani 2025 kwenye Uchaguzi Mkuu wa Serikali.
Kuna Wajumbe wengi wa Mkutano Mkuu Taifa kwa mujibu wa Katiba ambao wengine sijawataja hapo lakini nimeamua kuchukua kundi lenu tu, kwakuwa ninyi ni Wawakilishi wa moja kwa moja wa Wanachama.
Uchaguzi huu wa CHADEMA unaenda kuamua kati ya "Uhai" wa CHADEMA au "Kifo" cha CHADEMA. Na hii ni kwasababu tumeruhusu mafahari wawili ndani ya Chama kuingia ulingoni kupambana. Na makundi yamekuwa makubwa sana kwasasa.
Hebu fikiria kwa mfano, unaingia kwenye Uchaguzi wa Serikali unawakosa Watu hawa kwenye Kampeni.
-Tundu Lissu
-John Heche
-Godbless Lema
-John Pambalu
Halafu mbadala wake unawakuta;
-Devota Minja
-Sugu
-Wenje
-Welwel
Ukweli ni kuwa, Chama kitakuwa cha kawaida sana. Sina maana ya kuwadogosha hao niliotaja lakini maana yangu ni kuwa, tunahitaji kuwa na Watu wenye mvuto kwa Jamii ambao tayari wameshajijenga Kisiasa.
Na hao wengine waendelee kujinoa ili nao kuwa na viwango vikubwa vya Kisiasa angalau kuitisha Mkutano na kupata Watu wengi Mikoani.
Ninyi Wenyeviti na Makatibu wa CHADEMA ngazi nilizotaja hapo juu, mtaingia katika historia ya Nchi hii na Chama hiki. Mkitaka kukizika Chama hiki Historia yenu itaandikwa kwamba Mkutano Mkuu wenu ndio uliasisi anguko la CHADEMA kwa kumchagua mtu ambaye Wanachama na Jamii hawakumtaka hivyo wakaisusa CHADEMA.
Ama mkubali kuandikwa kwa wema kuwa, Mkutano Mkuu wenu ndio uliotumika kuhuisha upya CHADEMA katika Taifa letu. Chaguo ni lenu, sisi ni watazamaji na washauri tu.
Juzi wakati Mwenyekiti anazungumza aliwaita Watu wasiokuwa na uwezo wa Kiuchumi kuwa ni "Wabangaizaji" akiwemo Tundu Lissu. Wala hata msijali, nataka kuwakumbusha busara moja ya Baba wa Taifa Mwl. J.K.Nyerere alisema; "Wanyonge wanatakiwa kuungana kuwakabili wenye nguvu"
Unganeni "Wabangaizaji" mkamkabili "Mfanyabiashara wa ndani na nje ya Nchi".
Mkishindwa kuungana katika hili, hakuna tena jambo litakuja kuwaunganisha.
Kheri ya Christmas na Mwaka Mpya