Mahudhurio ya wagonjwa wa moyo yapungua JKCI kwa hofu ya COVID-19

Mahudhurio ya wagonjwa wa moyo yapungua JKCI kwa hofu ya COVID-19

Magimbi

JF-Expert Member
Joined
Oct 18, 2011
Posts
1,434
Reaction score
1,211


Wagonjwa wenye matatizo ya moyo, kisukari, shinikizo la juu la damu, figo na saratani wameshauriwa kuhudhuria kliniki zao bila kukosa ili kuepuka kupata madhara ya kiafya ikiwa ni pamoja na kupoteza maisha.

Rai hiyo ilitolewa jana Dar es Salaam na Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Prof. Mohamed Janabi wakati akizungumza kuhusu kupungua kwa idadi ya wagonjwa wanaotibiwa katika Taasisi hiyo tangu virusi vya Corona vilipoingia nchini.

Prof. Janabi alisema hivi sasa idadi ya wagonjwa wanaotibiwa katika Taasisi hiyo imepungua kutoka 300 kwa siku hadi kufikia 50 kwa siku na wagonjwa wanaolazwa idadi yao imepungua kutoka 150 kwa siku hadi kufikia 30.

Kwa upande wa wagonjwa wanaofanyiwa upasuaji mkubwa wa kusimamisha moyo idadi yao imepungua kutoka wagonjwa wanne kwa siku na kufikia mgonjwa mmoja .

Wagonjwa wanaofanyiwa upasuaji wa bila kufungua kifua kupitia tundu dogo wamepungua kutoka kumi kwa siku na kufikia watatu.

Mkurugenzi huyo Mtendaji alisema wao kama madaktari bingwa wa magonjwa ya moyo hawaelewi hivi sasa wagonjwa hao ambao hawahudhurii kliniki wanatibiwa wapi.

Alisema kama mgonjwa ataogopa kwenda Hospitali kwa kuhofia kupata maambukizi ya ugonjwa wa Corona ambao ukiupata na kupona haukuachi na madhara yoyote wakati kuacha kliniki za magonjwa ambayo kama usipotibiwa yatakusababishia madhara makubwa katika mwili wako.

Alisema wagonjwa wa moyo wanatakiwa kuondoa hofu kutokana na taarifa mbalimbali wanazozipata kuhusiana na ugonjwa wa corona jambo la muhimu wafuate maelekezo ya wataalamu wa afya kwa kufanya hivyo wataweza kuepuka kupata maambikizi ya ugonjwa huo na siyo kuacha kuhudhuria kliniki.

“Wote tunafahamu kuwa kutokana na tafiti mbalimbali zilizofanyika ulimwenguni zinaonesha wagonjwa wenye matatizo ya moyo, kisukari, shinikizo la juu la damu, figo, saratani na watu wenye umri mkubwa wa zaidi ya miaka 60 ndiyo wanaoathirika zaidi na ugonjwa wa Corona ikiwa wagonjwa hawa hawatahudhuria kliniki kama walivyopangiwa na madaktari wao wakipata maambukizi ya virusi vya corona ni rahisi kwao kupoteza maisha,” alisema .

“Wagonjwa wa moyo, kisukari, shinikizo la juu la damu, figo na saratani kama hawatahudhuria kliniki kwa kuhofia kupata maambukizi ya Virusi vya ugonjwa wa Corona wanaweza kupata madhara ya kupoteza uhai, kupata kiharusi, kupoteza baadhi ya viungo vya mwili kwa mfano mguu, kupofuka macho na kupoteza nguvu za kiume lakini ukipata maambukizi ya virusi vya corona na ukapona hutaweza kupata madhara yoyote,” alisisitiza Prof.Janabi .

Prof. Janabi alisema ni muhimu wagonjwa hao kwenda Hospitali kutibiwa kwa kuwa mgonjwa akiwa na magonjwa hayo hawezi kujitibia nyumbani.

Alisema jambo la muhimu ni kufuata ushauri wa wataalamu wa afya hii ikiwa ni pamoja na kuvaa barakoa, kunawa mikono kwa maji safi yanayotiririka na sabuni, kukaa umbali wa zaidi ya mita moja kati ya mtu na mtu na kuepuka mikusanyiko isiyo ya lazima.

“Taasisi yetu inatuma ujumbe wa kuwakumbusha wagonjwa wetu kuhudhuria kliniki zao kutokana na tarehe walizopangiwa na madaktari lakini wengi wao hawaji kutibiwa.

“Ninaendelea kuwasisitiza waje kutibiwa kwani tumechukua tahadhari zote za kuhakikisha hawapati maambukizi ya virusi vya ugonjwa wa Corona wawapo katika eneo la Hospitali”,.

“Wagonjwa wanaofika kutibiwa hapa wanapimwa joto la mwili kabla ya kuanza kupata huduma ya matibabu, tumefunga mabomba ya maji pamoja na kuweka vitakasa mikono katika maeneo mbalimbali ya Taasisi yetu hii inawafanya kupata nafasi ya kunawa mikono mara kwa mara pia wanakaa umbali wa mita moja kati ya mgonjwa mmoja na mwingine,” alisema Prof. Janabi.


My take. Inawezekana watu wanajiuguza Convid 19 majumbani wakihofia kupelekwaa karantini. Wanatumia dalili kujigundua wameathirika na kujitibu. Take precautions convid19 is
 
Hata mimi nilijiuguza nyumbani,sasa karibu napona dalili zacovid 19.

Nilipoona hatuna vipimo vya maana vya covid,sikuona sababu za kwenda huko hospitalini,na vilevile tuliambiwa hakuna matibabu ya huu ugonjwa,ila wanapambana na magonjwa yaliyojitokeza.

Inawezekana hata wengine walifanya kama nilivyofanya mimi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Dah Ugonjwa hauna dawa kila mtu anapambania afya yake kwa akili yake
 
Hata mimi nilijiuguza nyumbani,sasa karibu napona dalili zacovid 19.

Nilipoona hatuna vipimo vya maana vya covid,sikuona sababu za kwenda huko hospitalini,na vilevile tuliambiwa hakuna matibabu ya huu ugonjwa,ila wanapambana na magonjwa yaliyojitokeza.

Inawezekana hata wengine walifanya kama nilivyofanya mimi.

Sent using Jamii Forums mobile app
Umetumia dawa gani ?
 
Ndio faida ya kutishana hiyo mwisho wa siku watu wakifa huko nyumbani tunasema corona kumbe watu wana magonjwa ya moyo na hawahudhurii klinik kwa uoga wa corona.
 
Ndio faida ya kutishana hiyo mwisho wa siku watu wakifa huko nyumbani tunasema corona kumbe watu wana magonjwa ya moyo na hawahudhurii klinik kwa uoga wa corona.
Kweli kiongozi. Watu wanaweza fariki kwa maradhi mengine kabisa lakini ikahusishwa convid19.
 
Naona leo madaktari wanaita wagonjwa waje hospitali!!
Hivi pale Muhimbili matibabu ni bure eeeeh!!

Nikiunganisha mawazo naona suala hapo ni mapato ya hospitali yamepungua sana, kiasi ambacho yanahatarisha uendeshaji wake. Hivyo mkurugenzi wa taasisi ya moyo hapo Muhimbili ameamua kukwepa tu lawama

Moral of the story.
Ukiona wagonjwa hawaji tena hospitalini kwako, basi tambua
-Huenda wamepona
-Huenda wamepata nafuu.
-Huenda wamekata tamaa na tiba zako.
-Huenda hawana uwezo wa kumudu gharama
-Huenda wanatibiwa kwenye hospitali nyingine.
-Huenda wameshakufa.


Kwa utafiti wangu mdogo nimegundua baadhi ya wagonjwa waliokuwa wanafika Muhimbili kutibiwa, kwa sasa bado wanaendelea na matibabu yao lakini katika hospitali zingine za binafsi ambazo madaktari hao hao wa Muhimbili wanatumika kuwatibu. Huko kwenye Private hospitals na Kliniki binafsi, hakuna msongamano kama wa Muhimbili (hivyo hatari ya Covid hakuna), kuna usiri mzuri ambao kila mgonjwa anaupenda. Tena kuna tetesi zinasema madaktari wengine wa Muhimbili kwa sasa wako Chato kuwahudumia wagonjwa wao! Hali zao zikiwa mbaya ndio wanawaleta chap chap Muhimbili. Katikati ya vita ya Corona na kuna watu wengine wanavuna pesa nzuri sana.
 
Ukienda appointment muhimbili unatumia muda mrefu kuhudumiwa. Tiba ni kwa mtandao, madaktari wa muhimbili Wana clinic zao binafsi na hapo huenda kupata wagonjwa wapya kwenda kuwahudumia na kutimiza wajibu kulinda pension zao.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Prof. Janabi alisema hivi sasa idadi ya wagonjwa wanaotibiwa katika Taasisi hiyo imepungua kutoka 300 kwa siku hadi kufikia 50 kwa siku na wagonjwa wanaolazwa idadi yao imepungua kutoka 150 kwa siku hadi kufikia 30.

Wagonjwa wanaofanyiwa upasuaji wa bila kufungua kifua kupitia tundu dogo wamepungua kutoka 10 kwa siku na kufikia 3.


Hii ni hatari sana...



Cc: mahondaw
 
Huyu Janabi si alijiuzulu! Au nimechanganya mafaili?
 
Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete imeshtushwa na kupungua kwa kiasi kikubwa kwa wagonjwa wanaohudhuria kliniki za moyo katika hospital hiyo.

Akizungumza na Azam TV Mkurugenzi wa Taasisi hiyo Prof Mohamedi Janabi amesema kwamba kabla ya tatizo la corona walikuwa wanapokea hadi wagonjwa 1500 kwa wiki lakini sasa wanapokea wagonjwa 300 tu.

Hali hii imewashangaza na hivyo kuwahimiza wagonjwa wanaohudhuria kliniki kwenye taasisi hiyo kuendelea na kliniki zao bila hofu kwani hatari zaidi kuacha kliniki katika kipindi hiki cha ugonjwa wa COVID-19 kwani wao wapo hatarini zaidi!

Nimejiuliza, Je, kupungua kwa wagonjwa pale JKHI inawezekana pia wagonjwa wamepona?

Je, kuna uwezekano wagonjwa wengi sasa hivi wanaogopa kwenda hospitali hivyo kufanya hospitali nyingi kutokuwa na wagonjwa?

Hili la JKHI litufungue macho. Kuna kitu hakiko sawa mahali!
 
Back
Top Bottom