Mahusiano mengi ya kimapenzi yanavunjika kwa sababu wengi wameyafanya kuwa chanzo chao kikubwa cha furaha

Mahusiano mengi ya kimapenzi yanavunjika kwa sababu wengi wameyafanya kuwa chanzo chao kikubwa cha furaha

THE FIRST BORN

JF-Expert Member
Joined
Apr 24, 2019
Posts
2,224
Reaction score
4,472
Habari wana jukwaa.

Leo nataka niseme kitu kidogo sana.

Ushajiuliza kwanini mahusiano mengi yanavunjika, namaanisha mahusianoa ya mwanamke na mwanaume?
Jibu ni rahisi sana, sababu ni kuwa, wengi wa wale wanaoingia kwenywe mahusiano ya kimapenzi lengo kubwa ni kupata furaha kupitia mapenzi.

Yaani wanaamini kuwa, mpenzi aliyenae ndiyo atampa furaha. Hii ndiyo imekuwa chanzo kikubwa cha mapenzi kuvunjika, kwasababu ukimtumia mwenzako kama chanzo cha furaha yako mwishoni yeye atakuchoka atakuacha.

Mfano, kaka anaweza kuwa anapenda sana ngono hii mwishowe mwanamke itamkera na uhusiano hufa. Mfano mwingine, dada anakuwa anahitaji muda mwingi awe na jamaa, hii tabia mwanaume ataivumilia ila mwishowe ataichoka na uhusiano utakufa.

Kwahiyo kama tunahitaji mahusiano tuliyonayo yadumu hebu tusiyafanye kuwa chanzo kikubwa cha furaha yetu. Kuwa na kitu kingine cha kukupa furaha kubwa. Mfano mtu uwe unapenda sana kuangalia mpira, filamu, kucheza mpira au mpira wa kikapu, ama hata kucheza mziki.
 
Sasa wewe unataka kuanzisha kitu kisichokuwa na furaha au faida yoyote kwako!!?
Sijasema kisiwe na Faida nasema wengi tuna Tegemea sana kwenye mapenzi na ndio maana unaona hata mtu anapoachwa anapata mshituko sana.
 
Screenshot_20221014-135054.jpg
 
Kuna demu nilimtema juzi, ila leo naenda kumgegenda maana kwangu amekufa ameoza na mim ndo furaha yake. 😂

No way.
 
Back
Top Bottom