Elinazi A Baraka
New Member
- Jul 16, 2021
- 2
- 3
Habari zenu ndugu zangu, napenda nianze kwa kumshukuru Mungu kwa uzima anaotupa kila siku.
Napenda nishauri kwa uchache sana kuhusu 'Mapenzi' neno pendwa kabisa. Ni kweli mapenzi ni matamu haswa, Kuna mda unaweza ukahisi uko ulimwengu mwengine.
Ila kwa upande mwengine mapenzi na machungu jamani, kuna mda unajuta kwanini ulipenda, kuna mda yanafanya watu wanalazwa kwa magonjwa ya moyo na pressure, watu ni vilema kwa sababu ya mapenzi, kubwa zaidi kuna watu wako kaburini kisa mapenzi.
Mapenzi kuna mda yanaondoa Ila ladha ya sukari ambayo mda mwingine unaiona na kupelekea uchungu mkubwa sana.
Tufanye nini sasa ili kuepuka haya, zingatia mambo yafuatayo÷
1: Moyo ni wako sio wake
Jitahidi kumpenda kwa dhati Ila moyo wako baki nao, moyo ni wako hamna mwenye uwezo wa kukushikia.
2: Kumbuka mwanadamu anabadilika
Ni kweli Kuna mda mwanadamu anakuwa malaika haswa mda akiwa anakutaka Ila akikupata umalaika unatoka unabaki ubinadamu, usijisahau sana.
3: Tenda wema usingoje shukrani
Ndugu yetu Rapcha alitenda wema, nadhani unakumbuka nini kilifwata, ukiamua kutenda tenda shukrani ni majaliwa.
4: Jitambue
Hapa nataka ukae chini ujiulize ukiwa na hasira za kiwango cha juu unafanyaga nini ili zishuke bila kuleta maafa, kwa wale wenzangu wa sheria mkononi. Ndio kachepuka, umejaa mwenyewe unataka kupasuka, ukipiga husaidii, fanya chochote utoe hasira alafu ufanye maamuzi badae ukiwa huna hasira.
Mwisho, amua leo tafuta binadamu mmoja amua awe nae, usitafuta malaika sababu siku akilita tabia za binadamu utamuondoa Duniani.

Upvote
3