Mahusiano na dada wa kambo

Penzi la kificho huwa ni tamu kama nawaona[emoji23][emoji1787]
Yaani we acha tu just imagine toka tuna miaka 17 .Mapenzi kajifunzia kwangu na mimi mapenzi nimejifunzia kwake. Mwanzo tulikuwa tunafurahia mchezo tukasema tutaacha

Baadaye ndio hivyo hisia zikajiingiza. Tulijaribu kuwa na mahusiano tofauti tukashindwa maana tulianza kuoneana na wivu na kuumia tu
 
Hadi kulileta huku, means nafsi zenu ziwasuta na hamna amani. Sasa ya nini kung'ang'ana!!
Ni kweli Tupo kwenye denial . Halafu hii siri inanitafuna sina mtu wa kuzungumzia naye kuhusu hili ili huku ni kama safe space hakuna anayenijua nikimwadithia rafiki nitaonekana wa ajabu sana
 
Hakuna kosa kumpenda dada wa kambo na unaweza kumuoa bila kikwazo,msijiumize bure halalisheni uhusiano wenu,mie nipo tayari kuwa mshenga wako,iwapo utapenda
 
Muoe kwani ndoa ni ya wawili. Pia nyie sio ndugu. Ila ndio vizuri umelipiza kisasi cha baba yako usikute uyo Jamaa ndio sababu ya baba yako kuachwa na mama yako.
Ngoja tuone mkuu hisia zangu zikidi akili nitajua nafanya nini

Na chengine naangalia na maoni kama ya kuona niko sawa yapo mengi hata kama sio sawa hili jambo sina budi kufanya vile nilivyokusudia maana nipo kwenye denial

Naangalia mzani lakini bado hisia zimenitawala
 
Mimi kwakweli siwalaumu kabisa mapenzi ni upuuzi mno dah Muombeni tu Mungu awasaidie
 
Sawa kiongozi [emoji120]. Pengine nahisi pia nahitaji msaada wa kisaikolojia.
 
Ni kweli lakini huyo sio mwanamke wa kawaida ni dada wa kambo
sumu ya penzi ukishailamba hata kwa maziwa huwezi kupona...
Kuachana itakuwa ngumu sana na kuendelea pia ni vibaya hapo ndio pagumu mkuu
 
Kama wanapendana waoane tu, kwanza mpaka hapo tayari washaoana.
 
Ipo ndio kama hivyo tumependana na tumeshindwa kuwa na mahusiano na watu wengine
Tayari Mna Mahusiano Tangu Na Tangu Mnahitaji Mahusiano Na Watu Wengine Ya Kazi Gani??Boresheni Mahusiano Yenu Yenye Muunganiko Murua Na Historia za kuupa Moyo Furaha Na Amani Kila Mnapofanikiwa Kuwa Pamoja,,Let Love Lead,,,Msijibane Nyie Si Ndugu,,Ipeni Na Ionyesheni Dunia Pendo Lenu Lilivyomea Kwa Huba Na Hisia Bora Za Mapenzi.
 
Subirini wazazi wenu wafariki hafu muoane
Hili ni wazo zuri lakini kusubiri mpaka mzazi afe na umri ndio hivyo unakwenda je wasipotangulia nikifa mimi

Lakini bado huyo binti ana ndugu watachukuliaje hili swala unajua baba yake akikubali sitasemwa mimi tu hata wazazi watasemwa au kutengwa kwa nini wamekubali kidogo nahisi uzito wa jambo utapungua maana nitakuwa na support

Yaani hizi akili hizi saa nyingine nawaza hivyo
 
Kama wanapendana waoane tu, kwanza mpaka hapo tayari washaoana.
Sio kuoana tu, mfano nikuulize, wewe utakubali rafiki yako wa karibu aje kuoa mke wako uliye achana nae na umeishi nae kwa miaka na mlipata mtoto? kwa sababu mliachana na hakuna mahusiano ni sawa rafiki yako wa karibu aoe x wife wako? na je? utabariki hio ndoa pasipo shingo upande?

Marafiki wa kiume huwa wanatofautiana kupigiana ma ex na ushikaji hadi unakufa, sasa vipi kwa wazazi kuona wanao wanaoana?
 
Ndugu..jitahidi kuweka hisia pembeni - wewe hasa kama mwanamme. Yaani baba yake kamlala mama yako, na wewe unamlala mtoto wake..jamani...Hizi ny-e-g mshindo vipi?? Ukiona unafanya kitu lkn huna amani au unawasiwasi mpaka unaanza kuuliza watu ujue tayari nafsi yako iliishakuambia sio sawa - tii hiyo sauti...utamletea aibu mama yako....
 
Hakuna kosa kumpenda dada wa kambo na unaweza kumuoa bila kikwazo,msijiumize bure halalisheni uhusiano wenu,mie nipo tayari kuwa mshenga wako,iwapo utapenda
Yaani pamoja na kuandika huu uzi sipo tayari kumuacha na yeye hayupo tayari kuniacha mzani wa maoni ukizidi upande wangu sitajali chochote nitafanya nilichokusudia


Nipo kwenye denial mkuu na maoni ya huu uzi ukichanganya na hisia zangu mda si mrefu nitapata ujasiri wa kufanya kile ninachokusudia
 
Kwa mila za kiafrika hakuna dosari,muoane haraka,hiyo ndio destiny yenu,ni Mola ndio kawakutanisha
 
Ni kweli . Natamani ningepata wengi wakunipa maneno haya ya ukweli na uchungu maana hata kwa akili ya kawaida mahusiano yangu sio sawa kuendelea kuyaamini nazidi kujiumiza
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…