Mahusiano na dada wa kambo

Kwa hio utaruhusu ex mkeo aolewe na rafiki yako wa karibu na urafiki wenu ukaendelea?
Mzee unatumia hisia sana, hutaki wenzio wafurahie maisha.

Mmeachana na mkeo, huyo rafiki yako anajua mmeachana. Mmeenda mpaka mahakamani kupeana talaka.
Si ajabu mkagawana mpaka mali kumaanisha kua hamuwezi kua pamoja tena, wazazi washaridhia nk.

Sasa kutakua na tatizo gani akiolewa huko kwingine, ni kawaida tu kutokua sawa na huto rafiki wala haihitaji utaalamu kung'amua hilo ila haimaanishi urafiki utakufa au nitamkasirikia. Nitakaa mbali nao kulinda ndoa yao.
 
Kuna muujiza gan Tena 😀😀 mkuu nimefika chap
 
Mbona umekuwa emotional...?
Kwanza umejivuta sana kujibu hilo swali, ndipo ujue usizungumze kitu upo nje na hauna uhusika, fikiria ingekuwa upande wako...
Hilo suala kwa wazazi haitakuwa vyepesi..
 
Mbona umekuwa emotional...?
Kwanza umejivuta sana kujibu hilo swali, ndipo ujue usizungumze kitu upo nje na hauna uhusika, fikiria ingekuwa upande wako...
Hilo suala kwa wazazi haitakuwa vyepesi..
Wengi wenye mawazo kama yako hawawezi kukubali ila mimi siwezi kasirika/kuona wivu labda huyo rafiki awe kamuiba kwangu.

Na hiyo scenario ni tofauti ya ya baba, baba hakua anakojoa kwa mwanae na hao madogo sio ndgu, hawaunganishwi na chochote.
Baba wa binti na mama wa jamaa hawakua na mtoto si ajabu ni sogea tuishi na sio ndoa rasmi ya kimila/kiserikali au kidini!!

Mimi nikiwa ndio baba wa binti, aloo ni chap tu nampa mke dogo maana sio ndgu yake kabisa.
 
Basi tunatofautiana katika maamuzi, nihitimishe hivyo.
Na siamini undugu hadi muwe damu moja, naweza kulea mtoto wa rafiki yangu na nikamchukulia kama mwanangu wa kumzaa.
 
Basi tunatofautiana katika maamuzi, nihitimishe hivyo.
Na siamini undugu hadi muwe damu moja, naweza kulea mtoto wa rafiki yangu na nikamchukulia kama mwanangu wa kumzaa.
Undugu haupo namna hiyo.
Hata huyo mama wa jamaa na baba wa binti wangekua na mtoto bado huyo dogo huyo binti sio ndgu wa damu, coz hamna kitu wameshare sio baba wala mama.

Ni basi tu ile sijui kuogopa aibu, sijui jamii itakuonaje na vitu kama hivyo ila hamna tatizo juu ya hilo mkuu.
 
Sio kwl mkuu.

Dini ya Islam ni halali mtoto ambaye hujanyonya nae ziwa Moja.
Ila kama amenyonya ziwa Moja ni haramu.
Kama mtoto wa shangazi au baba mdogo unaoa kwann ushindwe kuoa dada wa kambo?

Mtoto wa baba wa kambo hakuhusu wala huna damu naye.
Hivi mtoto wa baba mdogo siunakuwa na Nasaba nae mkuu?japo najua kwa uislam inaturuhusu
 
Huyo mdogo wao angezaliwa atawaita dada na kaka? au mashemeji? au
Anyway kila mmoja ana maamuzi yake mkuu...
 
Hivi mtoto wa baba mdogo siunakuwa na Nasaba nae mkuu?japo najua kwa uislam inaturuhusu
Shangazi na baba mdogo au mkubwa wote sawa.
Sasa kama mtoto wa shangazi unaoa kwann wa baba mdogo usioe?

Kama ushawahi sikia waswahili wanasema ameoa mtoto wa Simba Kwa Simba,
Ndy hyo Sasa,kuoa mtoto wa baba mdogo au mkubwa..

Hivyo ndivyo waarabu wanavyooana mkuu.
 
Mtoto wa shangazi hauna nasaba nae,maana ye amezaliwa na koo ya baba mwingine,nadhani nasaba ipo kwa baba.
 
Siyo nduguyo huyo, hakikisha mnaoana
Mkuu labda useme kingine lakini dada wa kambo ni dada yako ni ndugu yako uliza utaambiwa. Unadhani kama sio ndugu ningelileta hili swala huku linalonitafuna rohoni .
 
Mkuu labda useme kingine lakini dada wa kambo ni dada yako ni ndugu yako uliza utaambiwa. Unadhani kama sio ndugu ningelileta hili swala huku linalonitafuna rohoni .
Ooh,sawa,kwahiyo mkipimwa vinasaba vinafanana kwa kile kitendo tu cha mama kuolewa na baba wa huyo binti,nilikuwa sifahamu.
 
Mtoto wa mjomba ( binamu)
Baba mkubwa ,baba mdogo ni ruksa

Kasoro dada wa kambo sio ruhusa kuoa au mwanamke ambaye alioa baba yako au mwanamke aliyekunyonyesha
 
Mwana mpumbavu ni huzuni kwa mamaye..
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…