Mahusiano na dada wa kambo

Mahusiano na dada wa kambo

Habari wa ndugu, Heri ya mwaka mpya natumaini wazima ,

Nimekuja na hii mada sio kwa lengo la kujisifia au kutangaza dhambi ya zinaa ninazofanya nimekuja na huu uzi sababu nahitaji ushauri pengine msaada wa kimawazo maana nahisi sio kawaida

Nisikuchoshe nipunguze maneno ni hivi kipindi nipo sekondari mama aliachana na baba baada ya kipindi kupita akaolewa tena na huyo mume aliyemuoa alikuwa ana binti yake alizaa na mwanamke mwengine mimi na mama wote tuliamia kwenye familia hiyo ambapo ni baba anaishi na binti yake makamu yangu hata kidato tulikuwa kimoja, Sasa sijui kuishi ndugu wawili wakike na wakiume wasio wa damu inachangia au shetani au ni tamaa zetu mbovu tulijikuta mimi na huyo binti ambaye ni dada yangu wa kambo tunaingia kwenye mchezo mchafu.

Tulifanya kwa siri . Kipindi wazazi walikuwa hawapo tulikuwa tunafanya mapenzi sana saa nyingine binti ananyata usiku anakuja chumbani kwangu saa nyengine naenda chumbani kwake saa nyengine sebuleni ikawa ndio michezo yetu mpka tukanogewa tukajikuta tunapendana maana hizi constant casual sex na mtu mmoja lazima mcatch feelings . So ikaenda ikaenda ye akapata mahusiano mapya na mimi pia lakini bado roho zetu hazikuridhika ilibidi dada yangu aachane na mtu wake na alikuwa na wivu na mimi na hakutaka kujihusisha na mahusiano ikafikia kipindi nikaenda chuo na yeye mkoa tofauti bado tukawa tunafatana kitendo cha mimi na yeye kuwa mbali kinatuumiza moyo in short tunapendana sana

Mama yangu hakufanikiwa kuzaa na huyo baba wa kambo na walikuja kuachana lakini sisi hatukuacha mawasiliano na mahusiano wote tumekuwa na mahusiano na watu mbalimbali lakini tumeshindwa maana kila mmoja moyo wake yupo kwa mwenzake .sasa tunajitegemea kila mtu yupo kwake lakini tumeshindwa kuachana

Natamani kumuoa lakini alikuwa dada yangu wa kambo na tayari baba yake alishaachana na mama yangu natamani tusipendane lakini tunashindwa , mahusiano yetu ya siri toka tuna miaka 17 na sasa ni watu wazima jamii itanichukuliaje ikijua ?nifanye nini nimsahau? nimchukie au pengine tunahitaji msaada wa kisaikolojia hata sielewi maana wote tulipanga tuachane lakini imeshindikana sometimes najuta kwa nini nilikutana naye au kwa nini mama yangu alikubali kuolewa na baba yake .


Natamani nimkimbie nibadili mawasiliano lakini atafanya juu atanipata saa nyengine nashindwa kujificha kuna kipindi tuliachana tulishindwa maana tulikuwa katika hali mbaya sana kiufupi tunapendana sana na tunatamani uhusiano wetu uwe wazi tuoane lakini ndio hivyo sio sawa katika jamii.

Ni hayo tu samahani kwa ambao bandiko hili litawakwaza
Yakobo alioa Binamu zake, hiyo ya kwako na Ya Yakobo ipi mbaya zaidi?
 
Kama unavyojua uhusiano wetu ulikuwa wa siri na bado ni wa siri hivyo tulikuwa makini changamoto kama hizo ikiwemo kufumwa au kupeana ujauzito zisijitokeze na binti alikuwa anajua mzunguko wake vizuri hata ukibadilika.


Hapo kwenye kuanza kuwaambia mzazi ndio mtihani sasa hapo ndipo kichwa kinauma

Nimfuata huyo baba yangu nimwambie nina mahusiano na mtoto wake ambaye anajua kwangu ni dada wa kambo amenilea naye toka nina miaka 17 yaani hapo ndipo changamoto
Nenda kwa baba yako wa kambo akikuuliza imekuaje mwambie niliwasiliana na fulani akanambia hadi sasa hajaolewa na mimi pia sijaoa nikamuuliza kama yupo tayari tuoane sababu tunajuana tangu wadogo na tumekuzwa na wazazi wenye maadili mazuri, akakubali ndio nimekuja kwako mzee kupata baraka zako, easy tu,
Unaweza kwenda na mzee mmoja wa busara akusaidie kumpanga mshua
 
Sio kuoana tu, mfano nikuulize, wewe utakubali rafiki yako wa karibu aje kuoa mke wako uliye achana nae na umeishi nae kwa miaka na mlipata mtoto? kwa sababu mliachana na hakuna mahusiano ni sawa rafiki yako wa karibu aoe x wife wako? na je? utabariki hio ndoa pasipo shingo upande?

Marafiki wa kiume huwa wanatofautiana kupigiana ma ex na ushikaji hadi unakufa, sasa vipi kwa wazazi kuona wanao wanaoana?
Sasa hapo unakua hujaachana nae.
Kama umeachana nae ana uhuru wa kua na yeyote.

Wazazi hawatakubali ila haitaondoa ukweli kua wanapendana na wameshanjunjana.
 
Sasa hapo unakua hujaachana nae.
Kama umeachana nae ana uhuru wa kua na yeyote.

Wazazi hawatakubali ila haitaondoa ukweli kua wanapendana na wameshanjunjana.
Kwa hio utaruhusu ex mkeo aolewe na rafiki yako wa karibu na urafiki wenu ukaendelea?
 
Back
Top Bottom