POLE SANA, uliyefanyiwa hivi.
Hata kama unayetegemea akupe kila kitu lakin kwa bahati mbaya au kwa makusudi,
ameshindwa kukutimizia yale utakayo wewe,
BADO hautakiwi kumwacha aliyekuwa mpenzi wako kwa kashfa au kejeli.
kwanini umkashifu mwingine eti kisa ajakupa hitaji la moyo wako,
Kama unaona ameshindwa kukutimizia utakayo au umemchoka tu unataka kumwacha ,
basi wewe mwambie tu kiutaratibu ,kwa usalama kabisa pasipo kuleta vurugu yoyote,
Yawezekana leo mmeshindwana kimapenzi au hamjaelewana kimapenzi ,
lakin mkajakuelewana hapo baadaye kwenye mambo mengine,
huyo unayemkashifu leo na kumwacha kwa kejeli,
kesho,kesho kutwa au hata uzeeni akaja kukufaa kwa hitaji lingine kabisa la kimaisha.
Binadamu tumekuwa wepesi sana wa kukosoa wengine ili hali sisi wenyewe hatujichunguzi vizuri,
huyo unayesema eti ameshindwa kukupa kile utakacho,
je umejiuliza kwa nini yeye ameshindwa kukupa hicho utakacho?,
isiwe wewe mwenyewe labda ndiyo chanzo cha yeye kushindwa kukupa wewe upendacho kupewa??,
tusipende sana kutimiziwa ndoto zetu na watu wengine bila kuweka juhudi zetu,
bali tutimize ndoto au mahitaji yetu kwa michango,juhudi,kujituma sisi wenyewe kwanza,
na ikishindikana bado hatupaswi kuwapa wenzi wetu lawama na kuachana nao kwa kashfa.
KABLA HAUJAMFANYIA MTU JAMBO FIKIRI KWANZA JE WEWE BINAFSI UNGEPENDA KUFANYIWA HIVYO??
USTAARABU,HEKIMA NABUSARA HAVIUZWI ILI LABDA USEMA SINA PESA YA KUNUNULIA,
BALI NI JAMBO LA KUAMUA TU KUWA NAHITAJI KUWA MTU MWENYE HEKIMA NA BUSARA KATIKA MAAMUZI YANGU YOTE.
HAIJALISHI TUMEUMIZWA,TUMETESWA,TUMETENGWA,TUMELIZWA,TUMESHINDWA KUPATA MAHITAJI YA MIOYO,
BADO NASISITIZA HATUPASWI KUACHANA KWA UGOMVI,MATUSI NA KASHFA.