Mahusiano ya mtandaoni

Mlimani city enzi hizo,ukiwa na kideti pale dooooh ,unaoga mara mbili mbili[emoji28][emoji28][emoji28]
Hehe he 2016 nikiwa Udsm nilikuwa na date pale na pisi moja samaki samaki nilikuwa mjinga nilinunua ice cream kisado mlimani city full kubebishana na pisi na kuagiza chakula samaki samaki wahudumu wakaanza kutuomba tuwapimie ice cream kwa glass hahahah
 
Basi mtu kama wewe usije ukajaribu kuwa na mtu kama mimi [emoji23][emoji23]..Huombi hela? Na mimi sijigusi hataa ....utanuna mpaka unipige kibuti mwenyewe [emoji38][emoji38][emoji38][emoji38][emoji38]
Kwamba bila kuombwa hela hutoi?[emoji28]
 
Wanawake wenzio wamepata funzo kwamba "muache nyodo, msidharau kila DM ya mwanaume... malengo hayatofautiani, wengine wapo real!"

Nilipata demu anaishi Ireland, aliitwa Natasha kupitia Snapchat mnamo mwaka 2018... hatukudumu, kwa sababu wazungu wanaogopa long-distance ingawa sio wote, na hakuwa na mpango wa kuja Afrika mapema ile. We ended-up our relationship😊
 
Enzi za Facebook imetaradadi
Nilipost kapicha kangu by that time ndyo nmemaliza advance nasubiri kwenda chuo
Mkaka mmoja akaja messenger tukaanza kuchat chat
Simu niliyokuwa nayo ikaharibika nikawa naenda kwa jirani nachat weee halafu narudisha simu
Siku hiyo akaniomba no ya simu nilikuwa na kitochi
Mahaba yakahamia huko
Tulikuwa tunachat na kuongea the whole night
Enzi za chombeza time tunaongea sanaaa
Yeye alikuwa yupo kilimanjaro Same ni muhasibu wa chuo fulani mimi nipo Arusha.
Wakati naaply chuo akasisitiza niombe vyuo vya kilimanjaro ili tuwe karibu..
Nikawzaa nimesoma kilimanjaro na Arusha kwanzia chekechea hadi advance na chuo nisome kilimanjaro......nikamuitikia tu ila vyuo nikaomba Dar

Hapo hatujawahi onana ila tumeiva kwenye hubaa na maokoto alikuwa anatuma hadi pesa ya kuapply alinitumia nikaibana maana nilikuwa na mama akalipa
Nikachaguliwa chuo dar.. alimind sana kwamba nmefanya makusudi
Baadae tukapatana vizuri hadi siku naenda Dar tukachaguliana hadi nguo za kuvaa🀣🀣🀣
Nmefika chuo tukaendelea ila nikaona changes kwake
Kumbe kule nilikokuwa Naazima simu Kuna siku sikulogout huyo dada akaiba namba za simu kwenye chats za messenger wapo wanachat
Akampa uongo kibao kuhusu mimi hadi bwana yule akanichukiaa mwishowe tukaachana bila kuonana
Ikapita miaka bwana yule akanitafuta maana sijawahi badilisha number ndyo kunipa mkanda mzima alivyochat na jirani yangu hadi wakakutana na kunyaduana πŸ˜€πŸ˜€πŸ˜€
Akaomba turudiane hapo nshapata mupenzi nikamkatalia....sijui yupo wapi Johnson jamani πŸ˜†πŸ˜†πŸ˜†
 
πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚Nimecheka had nimepaliwa
 
Story nzuri πŸ˜…πŸ‘πŸΎ
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…