Me tulikutana marafiki.com enzi hizo sasahivi ni mume wa ndoa 10years, kwa kweli sijawahi juta kukutana na huyu kaka, it was fate. Japo halikuwa lengo langu kuwa na mtu kutoka kwenye mtandao na nilikuaga naponda sana hilo swala jamani maisha haya😛, kweli usitukane mamba kabla hujavuka mto 😀 na kwenye profile yangu niliandika nina mahusiano so nisisumbuliwe, na nilikuaga sijibu msg za dm wala sizisomi nikifungua nafuta zooote. Sasa kuna jina lilikuwa linajirudia sana, yani kila nikisema nifungie kufuta msg lazma nione msg yenye hilo jina, siku moja nikaamua kufungua msg yake, nikakuta salam tu, nikaijibu then nikafuta, sasa ikawa kila nikifungua lazma nikute kanisalimia, na mimi najibu salam basi. Siku moja akaniomba namba ya simu nikamwambia sina simu, alijua nimemdanganya ila hakulazimisha tukaendelea na salam tu dm, kuna kipindi akapotea i ddnt bother kumtafuta nikamsahau. Akaja akaibuka tena, akaniomba tena namba nikakataa tena, akaomba atleast email address, hiyo nikampa, enzi zile za yahoo messenger, so tukawa tunawasiliana huko japo si sana, mana hakuwa muongeaji sana, tukaenda hivyo for almost a year, akaniomba tena namba ya simu akasema hii ni mara ya mwisho kama kweli sina simu yuko tayari kununulia ila kama namnyima tu namba basi hatanisumbua tena kuhusu hilo, baada ya siku 2 nikampa namba, mawasiliano yetu yakaanzia hapo,it took me 6 months kukubali kuonana nae, mana nilikuaga muoga sana. But that day nilipokutana nae, katika kuongea akaniambia i will marry you next year tarehe fulani na mwezi fulani, i thout he was joking. But he wasnt joking, kweli mwaka uliofuatia tarehe ile ile na mwezi ule ule aliosema tukafunga ndoa Takatifu pale St. Joseph, and it has been an amaizing 10 years of marriage. Bcz he is everything i ever wanted, huwa nasema ni Mungu tu sio hivi hivi.