Mahusiano

Mahusiano

Hapana aisee. . . bora niogope niponee chupu chupu. Wanaume wenyewe ukisema unataka waliotulia wenyewe wanadai hamna. . . ya nini matatizo?
Raha ya ngoma uingie ucheze mwenyewe..lol
 
Because love is dangerous, insecure.... And nobody knows where love will lead. It is just like a cloud -- moving with no destination. Love is a hidden cloud, whereabouts unknown. Nobody knows where it is at any moment of time. Unpredictable -- no astrologer can predict anything about love.
kungekuwa na uwezekano wa kusoma moyo wa mwenzako, pangechimbika
 
Hapana aisee. . . bora niogope niponee chupu chupu. Wanaume wenyewe ukisema unataka waliotulia wenyewe wanadai hamna. . . ya nini matatizo?
ukitaka aliyetulia utasubiri mpaka uzee ukukute, cha maana ni kama anakupenda
 
Hivi jamani mahusiano magumu sana,
Wakati mwingine unaona umeula your the luckiest woman,
Unaona kama dunia umeiweka mkononi,
Wakati mwingine unajiona looser tu,
kama huna thamani yoyote duniani,
wakati mwingine unapenda kuwa benet na partner wako kila mahali ,
wakati mwingine unaona bora uwe peke yako,
wakati mwingine unapenda anavyoongea,
wakati mwingine akiongea unamuona kama analalama,
wakati mwingine unamwona anapendeza mzuri sana,
wakati umechukia unamuona kama kituko fulani hivi

hivi mwalimu wa mahusiano ni nani,mi naona hakuna
mwalimu ni wewe mwenyewe, kutatua matatizo yako
kuongea na mwenzako kwa kila linalokukera
embu tupeane uzoefu ndugu zangu
nawatakia siku njema

mapenzi hayana formula kamili! Cha muhimu ni kubadilika kulingana na yanavyotaka! Namaanisha kuna wakati yatakuwa matamu au machungu ila bado utayaita mapenzi maana hayatakuwa na jina lingine tena
 
Ni kubadilika kutokana na wakati kila siku najifunza mwenzio na macho yote nikiwa nimefungua lakini bado najikwaa kweli hamna mwalimu wa mapenzi.
 
Hata kuangalia ni burudani tosha.

Sasa si bora uzee unikute kuliko mtoto wa mtu anipeleke kaburini kabla hata sijaozesha mwa/wanangu?
wewe ingia tu, uzuri ni kwamba hakuna aliyekufa kwa kuachwa/kuumizwa, waliofanya hivyo ni walijiua.
 
Ni kubadilika kutokana na wakati kila siku najifunza mwenzio na macho yote nikiwa nimefungua lakini bado najikwaa kweli hamna mwalimu wa mapenzi.

mwalimu wa mapenzi ni mpenzi wako ulienae tu! Kama unajifunza halafu humfundishi unakuwa unafanyia kitu kinaitwa kalai! Inabidi wote mjifunze pamoja na mpeane homework za kutosha!
 
Ila wapo waliokufa kwa magonjwa waliyoletewa, wengine wanahesabu siku tu.
tungekuwa tunawaza hayo, dunia ingeshaacha mahusiano zamaaaaaaaaaaaaaani, na soon binadamu wangeishia hapa duniani
 
tungekuwa tunawaza hayo, dunia ingeshaacha mahusiano zamaaaaaaaaaaaaaani, na soon binadamu wangeishia hapa duniani

Kwasababu wote hatuwazi hivyo hamna ubaya. . . wa kuokoa kizazi wapo, na waoga tupo.
 
Back
Top Bottom