Victor Mlaki
JF-Expert Member
- May 1, 2016
- 4,151
- 4,277
Katika hali ya kipekee leo Rais katika zuara yake Masasi Mkoani Mtwara amepokea kero mbalimbali lakini kero hii ya mahusiano amewataka viongozi wakae. Ni kweli zipo kero nyingi lakini kero inapofikishwa kwa Rais inapata uzito.
Kero hii inaonesha bado tuna safari ndefu sana katika utekelezaji wa ilani ya chama Tawala. Hali ya mahusiano dhaifu ni changamoto katika maeneo mengi na Masasi ni kielelezo tu jambo ambalo linawafanya wanajamii kuona kama Serikali yao haichukui hatua za dhati.
Ikumbukwe viongozi mbalimbali ni sehemu ya kuonesha jitihada chanya za Serikali juu ya utatuzi wa kero mbalimbali za wananchi. Viongozi ni chachu ya imani na matumaini ya wananchi kwa Serikali yao. Viongozi mmeaminika, itendeeni haki imani ya waliowateua.