GE2025 Maiko Salali Hosea atia nia kugombea Ubunge, Jimbo la Mpwapwa

GE2025 Maiko Salali Hosea atia nia kugombea Ubunge, Jimbo la Mpwapwa

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

DuaZaMama

JF-Expert Member
Joined
Jun 2, 2025
Posts
1,882
Reaction score
4,153
Kada wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Maiko Salali Hosea amechukua rasmi fomu ya kuomba ridhaa ya kugombea Ubunge wa Jimbo la Mpwapwa mkoani Dodoma kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM).
1751194304151.png
 
Mkurugenzi wa Shirika lisilo la kiserikali la Foundation for Disability Hope FDH Maiko Salali, ameingia rasmi kwenye kinyang’anyiro cha kugombea Ubunge kwa kuchukua fomu ya kuomba ridhaa ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) kuwania Jimbo la Mpwapwa katika uchaguzi ujao.

Salali alichukua fomu hiyo katika ofisi ya CCM Wilaya ya Mpwapwa, mkoani Dodoma, mbele ya viongozi wa chama, wanachama na wafuasi wake waliokusanyika kushuhudia tukio hilo.

Maiko Salali anajiunga na orodha ya wanachama wa CCM wanaowania ridhaa ya kugombea ubunge kupitia chama hicho kuelekea uchaguzi mkuu, huku Jimbo la Mpwapwa likitarajiwa kuwa na ushindani mkali kutokana na mvuto wake wa kisiasa.

Akizungumza baada ya kuchukua fomu hiyo Salali amesema kauli mbiu yake ni Ubunifu, ushawishi, ushirikishaji na uthubutu kuziendea changamoto na kuwa fursa.
 
Back
Top Bottom