Mambo Jambo
JF-Expert Member
- Jul 11, 2008
- 1,100
- 82
Mrembo,
Kelele za Chura hazimzuii ng'ombe kunywa maji. Wasikutishe hawa. Kama hujatukana mtu hapa basi ni poa tu. Watu wanaweka thread za ajabu sana hapa na hakuna anayepiga kelele. Mfano mtu kaweka eti Master P anaanzisha TV yake USA, so what?? Kwa sababu haikugusa Watz, ilikufa kimya kimya. Ila hii naona watu wameishabikia kweli kweli na huu ni ushahidi tosha kuwa hawa jamaa ni watu maarufu. Kama ni watu maarufu basi hii ni POA kabisa. Umaarufu una gharama zake eti. Ukipata na nyingine wee lete tu. Sana sana ziweke kwenye UDAKU au hata hapa Celebrities. Mtu ukishaingia tu hapa basi ujuwe umekubali kuanza kusoma UDAKU. Utaanza kusoma pumba kama Ohh, jamaa anavaa D&C feki, ohh gari lake la kuazima, ohhh Mzungu wake masikini nk nk. Hapa kama sehemu ya udaku au jokes, ni sehemu ya kuja kupunguza stress. Hakuna issue za maana hapa. Ukitaka za maana basi nenda kwenda siasa, elimu nk. Mrembo weeee, mie masikio yanawasha, lete nyingine 🙂
Hapa siyo sehemu ya udaku wala jokes, na kama una-stress nenda kamwone doctor, nani alikwambia udaku ni dawa ya stress....walewale wa uwazi.