Maisha baada ya kifo

Maisha baada ya kifo

Innocent Kirumbuyo

JF-Expert Member
Joined
Jan 1, 2014
Posts
4,641
Reaction score
4,457
Maisha mapya yanaanza mara tu roho inapouacha mwili, yule uliyekuwa ukimuita Dear huku akisema hawezi kupata usingizi bila kulaza kichwa chake kifuani mwako, siku hiyo hata hawezi kukushika. Yule mama yako uliyemuona ni kero pindi alipokuletea shida zake, siku hiyo ndio atakuwa kakaa pembeni na ulipolazwa kwa huzuni huku akiwa kashika shavu na kuitikia pole za ndugu na jamaa kwa unyonge. Wale marafiki zako uliyokula nao bata kipindi upo hai, hao ndio watakuwa wakitazama saa kila muda huku wakiuliza tunazika saa ngapi maana wanawahi kwenye mambo yao.Hata wale jamaa zako wa karibu uliokuwa ukijinyima kwa ajili yao, siku hiyo ndio watatoa pesa za kununua karata ili wacheze na kujifurahisha, kipindi wewe upo ndani ukingoja kuzikwa wao nje ni vicheko kwa sana. Ile michepuko yako ya nje iliyokuwa akikudanganya kuwa ni ya kufa na kuzikana, siku hiyo ndio itakuwa jikoni ikiwahi kupika ili watu wale wakakufukie kisha wakuache peke yako. Ndugu zako wamegoma kutoa michango ya jeneza na sanda wakidai marehemu alipokuwa hai pesa yake ilikuwa ya kulia bata, wamesahau kuwa hukuwahi kuvumilia kukaa na pesa huku ndugu wakiwa na shida!! Tazama wale uliyokuwa ukiwadai wanakana kuwa huwadai,baada tu ya kugundua kuwa huwezi kuongea tena.Lakini japo wote watakutenga na kukusindikiza kwa mabaya, kamwe Yesu hawezi kukutenga. Hata watakapo kuacha makaburini peke yako,huyo Yesu atakufata kukuchukua#kuwa mjanja, nenda na wakati, kuna ujanja upi zaidi ya kumwamini na kumfuta Yesu????
 
Mmmh Maisha baada ya kifo..? Kwani mtu akifa kuna Maisha mengine yanaendelea? Labda mimi mshamba ebu nisubiri comments za wadau wengine labda watajitokeza na wadau waliowai kufa wakafufuka watuambie ni maisha gani Yapo baada ya kufa
 
Aseeeh ata mimi nawasubiri hawa wadau waliokufa wakafufuka tena wkaja Julio's story za maisha baada ya kifo jinsi yalivyo na sisi waje watusimulie jinsi hali ilivyo uko kwenye maisha baada ya kifo
 
4 Kwa kuwa liko tumaini kwa yule aliyeambatana na wote walio hai; (maana ni afadhali mbwa aliye hai kuliko simba aliyekufa);
Mhubiri 9 :4

5 kwa sababu walio hai wanajua ya kwamba watakufa; lakini wafu hawajui neno lo lote, wala hawana ijara tena; maana kumbukumbu lao limesahauliwa.
Mhubiri 9 :5

6 Mapenzi yao na machukio yao, na husuda yao, imepotea yote pamoja; wala hawana sehemu tena katika jambo lo lote lililofanyika chini ya jua.
Mhubiri 9 :6
 
Nikifikiria hali ya kaburi kulivyo napata hofu na woga sana. ila nikikumbuka faraja na ahadi za bwana Yesu kristo naruka ruka kwa furaha kwani ndiye mwema na mwenyekupendeza tena hadanganyi.

-Sala ya Matumaini......
 
maisha baada ya kifo?

Pliz andika nutrients circulation hapo maana hayo ndo maisha baada ya kifo na yanathibitika!
 
Back
Top Bottom