Innocent Kirumbuyo
JF-Expert Member
- Jan 1, 2014
- 4,641
- 4,457
Maisha mapya yanaanza mara tu roho inapouacha mwili, yule uliyekuwa ukimuita Dear huku akisema hawezi kupata usingizi bila kulaza kichwa chake kifuani mwako, siku hiyo hata hawezi kukushika. Yule mama yako uliyemuona ni kero pindi alipokuletea shida zake, siku hiyo ndio atakuwa kakaa pembeni na ulipolazwa kwa huzuni huku akiwa kashika shavu na kuitikia pole za ndugu na jamaa kwa unyonge. Wale marafiki zako uliyokula nao bata kipindi upo hai, hao ndio watakuwa wakitazama saa kila muda huku wakiuliza tunazika saa ngapi maana wanawahi kwenye mambo yao.Hata wale jamaa zako wa karibu uliokuwa ukijinyima kwa ajili yao, siku hiyo ndio watatoa pesa za kununua karata ili wacheze na kujifurahisha, kipindi wewe upo ndani ukingoja kuzikwa wao nje ni vicheko kwa sana. Ile michepuko yako ya nje iliyokuwa akikudanganya kuwa ni ya kufa na kuzikana, siku hiyo ndio itakuwa jikoni ikiwahi kupika ili watu wale wakakufukie kisha wakuache peke yako. Ndugu zako wamegoma kutoa michango ya jeneza na sanda wakidai marehemu alipokuwa hai pesa yake ilikuwa ya kulia bata, wamesahau kuwa hukuwahi kuvumilia kukaa na pesa huku ndugu wakiwa na shida!! Tazama wale uliyokuwa ukiwadai wanakana kuwa huwadai,baada tu ya kugundua kuwa huwezi kuongea tena.Lakini japo wote watakutenga na kukusindikiza kwa mabaya, kamwe Yesu hawezi kukutenga. Hata watakapo kuacha makaburini peke yako,huyo Yesu atakufata kukuchukua#kuwa mjanja, nenda na wakati, kuna ujanja upi zaidi ya kumwamini na kumfuta Yesu????