Maisha baada ya Kifo

Maisha baada ya Kifo

La Princesa

JF-Expert Member
Joined
Dec 21, 2013
Posts
1,049
Reaction score
1,160
Habari zenu wanajamvi ? Samahani kwa usumbufu, ninavyofahamu mimi kutokana na Imani yangu ya Kikiristo(Sijui kwa dini zingine ) Sipaswi kuogopa kifo kwa sababu lipo tumaini kuwa Yesu atarudi tena yaani Second Advent kisha atatuchukua nasi tutakwenda kuishi na kutawala pamoja naye...!

Swali linakuja, je! kabla ya ujio wake wa Pili, Mtu anapokufa kuna maisha yanayoendelea baada ya kifo? Nikimaanisha, kama roho huwa inamrudia muumba wake,

1) Ni kwa nini watu wengi huwa wanasema roho yake ipumzike kwa Amani?

2) Je ni kweli kuwa wakati mwingine wafu huwa hawapumziki kwa Amani, so Huwa wanaendelea na Maisha katika ulimwengu usioonekana?

3) Je mizimu ni sehemu ya Maisha hayo?

Nawasilisha
 
maisha baada ya kifo yapo na huanzia kaburini
 
Kwa imani yetu hiyo hiyo ya kikristo, nafahamu kuwa mtu akifa roho hutoka na hubaki ikielea hewani ( hear say)! Na mwili ukiwa kaburini huwa hakuna kinachoendelea sababu hakuna mawasiliano baina ya mifumo mbalimbali iliyopo mwilini sababu huwa imesimama/imekufa. Huwa tunaambiwa yesu akirudi atakuja kuwafufua wafu kisha wataungana na walio hai na kupelekwa mbinguni kwa ajili ya hukumu.
 
Mtu akifa roho yake hupewa mtu mwngn....ndo mana watu wanzaluwa upya na wanakufa daily...ni re cycling system tu. Imagn tungekua hatufi tungeenea uku duniani?
 
tunakufa, tunazikwa, tunaoza, tunarutubisha udongo, tunarutubisha mimea, tunaliwa na wanyama(akiwemo binadamu), N.K.

hiyo ndio small part of chain of our life

binadamu hana mwanzo, hana mwisho kama ilivyo energy
 
Kuna scholarship nyingi juu ya life after death. Nahili linakuwa reflected na Imani mbalimbali. Hivo kila imani inakuwa na mafundisho na msimamo wake. Mfano kuna Imani zinazofundisha kuwa ukifa ndo mwisho wako and no life after death. Kuna Imani zinazoamini kuwa Ukifa roho yako (soul) inakuwa transformed katika mnyama flani, mfano Hinduism wanaamini kama ulikuwa na matendo mazuri (Karma) ukifa roho yako itaingia kwenye mnyama mzuri mfano njiwa nk. Km Karma yako mbaya utazaliwa labda fisi, nyoka nk. Imani ya Buddhism inaamini pia kuwa ukifa roho yako itashift kuwa viumbe wengine.
 
Imani ya kikristo na ya Kipagani zinaamini kuwa ukifa there is a life after death, roho yako inatengana namwili roho inakuwa na conscious kama mtu unapokuwa amelala unaweza ukafanya lolote katika hali ya roho ndo mfano wakufa. Wapagani wanaamini kuwa ukifa ile roho inabaki ndo maana mababu hasa kule kijijini huwaga wanaperform some rituals kwenye makabuli yamababu kma ibaada flani kama wanataka kitu flani kitokee. Wanawaomba hao mababu kwasababu wapo kwenye hali ya roho wanaweza wakawasiliana namuumba maombi yao yakapatikana
 
Back
Top Bottom