Maisha baada ya Uchaguzi TFF: Mwakalebela Uchaguzi haukuwa huru na wa haki

Maisha baada ya Uchaguzi TFF: Mwakalebela Uchaguzi haukuwa huru na wa haki

Kurzweil

JF-Expert Member
Joined
May 25, 2011
Posts
6,621
Reaction score
8,411
Pamoja na kuambulia kura tatu katika uchaguzi mkuu wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), aliyekuwa mgombea wa nafasi ya urais, Fredirick Mwakalebela amesema uchaguzi huo hakuwa huru na haki ila anajipanga kugombea tena uchaguzi ujao.

Mwakalebela alipata kura tatu kwenye uchaguzi uliofanyika Jumamosi iliyopita mkoani Dodoma huku wapiga kura wakimpa ridhaa hiyo, Wallace Karia kura rais kwa kumpa kura 95, akiwaacha kwa mbali sana wapinzani wake Shija Richard, Ally Mayay waliopata kura tisa kila mmoja , Iman Madega kura nane, Mwakalebela 3 na Emmanuel Kimbe kura mmoja.

Mwakalebela aliyewahi pia kuangushwa katika uchaguzi wa TOC baada ya kupata kura 10 dhidi ya 45 za Filbert Bayi alisema uchaguzi wa TFF haukuwa huru wala wa haki huku akiainisha sababu nne za kwanini uchaguzi huo anaona haukuwa huru na wa haki.

"Najipanga kwa uchaguzi ujao, nitaogombea tena tukijaliwa kufika, tumeangalia mapungufu na mwisho wa uchaguzi huu ndiyo mwanzo wa uchaguzi ujao, lazima nigombee tena," alisema Mwakalebela.

"Kwanza mchakato ulivyoanza tu, kitendo cha kuvunja kamati ya uchaguzi ilikuwa ni kinyume na katiba ya TFF kwani katiba inasema kamati inapaswa kuwa madarakani katika kipindi cha miaka miwili.

"Pili ni kitendo cha Kamati ya utendaji kukutana ndani ya siku mbili kuzungumzia uchaguzi badala ya kutoa notisi ya siku 14, tatu Simba ilipeleka mjumbe asiye sitahili kupiga kura na akapiga na uchaguzi umefanyika wakati kukiwa na rufaa ya Iringa ambayo haijatolewa majibu," alisema Mwakalebela.

Chanzo: Mwananchi
 
Hana uwezo, ajipime ameshiriki chaguzi ngapi za kimichezo naza kisiasa kote anapigwa kwa kuambulia kura za aibu!. Namshauri atafute biashara nyingi na si hiyo biashara ya kupitia box la wapiga kura maana yeye ni shahidi, Iringa mjini kapigwa kwenye chaguzi za kisiasa akaishia TAKUKURU, TOC alipigwa akaishia kulialia na juzi TFF kapigwa tena kwa kura za aibu na sikumbuki vizuri hata nafasi ya uteuzi ya UDC huko Mkoani Njombe nayo hakuto akawekwa pembeni na JPM, ajipime ukweli ndio huo!.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
mwakalebela aachane ana hizi mambo sio siasa wala mpira kote anabwagwa
 
Uyo gundu lake lilianza toka 2010 baada ya kutandikwa na comrade msigwa

Angerudi akaendelee na kazi yake mtibwa

mchana toch ,usiku magogo tufanyaje?
 
Back
Top Bottom